Abdallah Bulembo awe wa kwanza kufukuzwa CCM

CCM OYEEE! KWA SAUTI YA BULEMBO...

HUYU KADA NI MWIBA MKALI SANA KWA LOWASSA NA WAFUASI WAKE!
 
Najitokeza kwa mara ya pili leo kumzungumzia Alhaji Abdallah Bulembo,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM na kada mbobezi. Mara ya kwanza ilikuwa alipohusishwa na kukwamisha uchaguzi wa Meya Dar. Nilimshauri ajitenge na uchaguzi huo.Uchaguzi ukafanyika.

Leo,natoa wito wenye mvuto kuwa kada huyu awe wa kwanza kufukuzwa toka CCM. Ameharibu mchoro wa chama. Chama kinajichora kiubora kuwa kipo makini na pamoja. Kinajichora kuwa imeamuliwa bila kulalamikiwa kuwa Rais Magufuli akabidhiwe uenyekiti wa chama hapo Julai 23.

Kusema kuwa wanaopinga Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti waondolewe chamani,ni kuharibu msimamo wa chama. Ndani ya CCM,kimchoro usio na kihoro,hakuna wanaopinga. Wote wanashangilia bila kulia kwa kadhia. Wote wanataka kukabidhi badala ya kuchagua.Hakuna anaowasema!

Kwakuwa amesema lisilokuwepo,Bulembo awe wa kwanza kufukuzwa CCM.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Mkuu umesahau kinacho muua kambale ni mdomo wake mwenyewe, bulembo tayari kesha twambia kuwa ndani ya ccm kuna makundi mawili yanayo pingana juu ya uenyekiti wa ccm.
 
Hivi huyu Bulembo pia ni msemaji wa chama au amejisahau kuwa bado cheo chake cha meneja wa kampeni wa Magufuli kinaendelea?!
Inawezekana labda msemaji yupo kwenye kundi pinzani huwezi kujua
 
1468347225196.jpg
 
Bulembo amepiga sana hela katika teuzi za Magu. Kama unataka Udc, uDas, Ded nk wewe "mtulize" Bulembo unalamba dume.
 
Najitokeza kwa mara ya pili leo kumzungumzia Alhaji Abdallah Bulembo,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM na kada mbobezi. Mara ya kwanza ilikuwa alipohusishwa na kukwamisha uchaguzi wa Meya Dar. Nilimshauri ajitenge na uchaguzi huo.Uchaguzi ukafanyika.

Leo,natoa wito wenye mvuto kuwa kada huyu awe wa kwanza kufukuzwa toka CCM. Ameharibu mchoro wa chama. Chama kinajichora kiubora kuwa kipo makini na pamoja. Kinajichora kuwa imeamuliwa bila kulalamikiwa kuwa Rais Magufuli akabidhiwe uenyekiti wa chama hapo Julai 23.

Kusema kuwa wanaopinga Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti waondolewe chamani,ni kuharibu msimamo wa chama. Ndani ya CCM,kimchoro usio na kihoro,hakuna wanaopinga. Wote wanashangilia bila kulia kwa kadhia. Wote wanataka kukabidhi badala ya kuchagua.Hakuna anaowasema!

Kwakuwa amesema lisilokuwepo,Bulembo awe wa kwanza kufukuzwa CCM.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Tuanze kwanza na viongozi wa kinachojiita chama cha demokrasia. Wako waliohubiri kuwa Lowassa ni fisadi. Baada ya msimamo juu ya Lowassa kubadiika, at the minimum, walipaswa kujuzulu uongozi. Simamia kwanza hilo kabla hujavuka mipaka.
 
Huyu Bulembo yule aliyekuwa FAT enzi ya Ndolanga ,FAT ile iliyokuwa na Migogoro kila kukicha, alafu CCM ikampa dhamana ya Uenyekiti wa Wazazi bila Uchungu chini yake Shule Moja ya Wazazi kule Tarime Mara ikapigwa mnada kwa sababu ya deni la Vitabu,uwa napata shaka sana na uongozi wa huyu jamaa sijui tatizo ni elimu ama ni kutojitambua, suala la kuondolewa katika chama ni mambo ya kusubiri ni muda ndio utaamua.
 
Back
Top Bottom