Abarikiwe aliyemleta Rais Samia Duniani

Abarikiwe aliyemleta Rais Samia Duniani

Rais Samia Ni Kama maji Usipoyanywa utayaoga tu,pia sipo hapa kumnanga mtu Bali kuwasilisha mawazo yangu juu ya Rais Samia na uchapa kazi wake uliotukuka na ulioteka mioyo ya watanzania ambayo imeridhishwa na utendaji kazi wake
Usisahau kuweka cv yako mkuu mwezi wa 5 kuna ajira serikali itatoa
 
Mama amekuja Kutatua hizi shida

Hakika Rais Samia ni jibu la matatizo na kero zilizokuwa zinaleta changamoto katika maisha ya watanzania, Ni mama aliyeleta matumaini na Tabasamu Katika Mioyo ya watanzania,kila mmoja ameguswa na kufikiwa na juhudi za mh Rais katika kututumikia na kutuinua kiuchumi watanzania,Hakuna anayeachwa nyuma Wala kupitwa na mipango ya serikali ya Rais Samia
 
Mama amekuja Kutatua hizi shida

Hakika Rais Samia ni jibu la matatizo na kero zilizokuwa zinaleta changamoto katika maisha ya watanzania, Ni mama aliyeleta matumaini na Tabasamu Katika Mioyo ya watanzania,kila mmoja ameguswa na kufikiwa na juhudi za mh Rais katika kututumikia na kutuinua kiuchumi watanzania,Hakuna anayeachwa nyuma Wala kupitwa na mipango ya serikali ya Rais
 
Nilivyoona umeweka hadi namba ya simu, nimeahirisha kukupa like japo umeandika vitu vinavyofanana na ukweli.
 
Ndugu zangu watanzania,

Kwa hakika libarikiwe sana tumbo lililombeba mama Samia, lilibeba mtoto aliyekuja kuwa kiongozi wa Tanzania, kiongozi mwenye upendo, hekima, busara, ukarimu, huruma, unyenyekevu na usikivu.
Yote kwa yote mm napenda sana kwa jinsi alivyo mkweli ktk serikali yk.

Hapo nyuma rulikuwa runadanganywa sana sana.
 
Nilivyoona umeweka hadi namba ya simu, nimeahirisha kukupa like japo umeandika vitu vinavyofanana na ukweli.
Nashukuru ndugu yangu Kama ujumbe Wangu umeeleweka na kuunga mkono juu ya upekee wa Rais wetu na mama yetu mama Samia kwa juhudi zake za kujenga Taifa letu,Tunaweza kutofautiana kimtizamo na kisiasa lakini naamini Ni lazima wote tutakubaliana na ukweli kuwa Rais Samia Ni mchapa kazi asiye na wa kufananishwa Naye Barani Afrika kwa Sasa, Ni kiongozi aliyeleta matumaini na Tabasamu kwa watanzania wa vyama vyote na kuleta Furaha katika maisha ya watu wote kutokana na ucha Mungu wake na hofu ya Mwenyezi MUNGU aliyo jaa katika kifua chake
 
Yote kwa yote mm napenda sana kwa jinsi alivyo mkweli ktk serikali yk.

Hapo nyuma rulikuwa runadanganywa sana sana.
Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani Ni mcha Mungu na mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu ndio sababu husem ukweli na haogopi kuusema ukweli kwa watanzania
 
Ishiliniishilininatanonitampa.
IMG-20230219-WA0003.jpg
 
Tunapoandika tuwe makini tusifanye kufuru.

Ufalme wa Mwenyezi Mungu ni wakipekee hauingiliwi.
 
Huwa tunapongeza baada ya kuona matokeo na sio mipango, usimamizi bora ndio unaleta positive results, ukifeli kwenye usimamizi hakutakuwa na positive results tutakachoona ni total failure.

Tulipongeza sana "Kilimo kwanza" lakini matokeo yake tukaletewa "Kagoda" na kutajirisha waasia na waarabu na kuendelea kuwaacha watanzania mafukara.
 
Ngonjera nyingi hadi umesahau kuweka namba ya simu na unako patikana labda utafikiriwa mkeka ujao
 
Hivi hamuoni umeme unakatika Kila siku, tozo hamzioni Benki, Tigo pesa, Bei ya vyakula kuwa juu Kama unga 2,000, Michele 3,600, maharage 4,000, Deni la Taifa Tilion 100, je mnajielewa kweli. Kila siku kusifia.
 
Ndugu zangu watanzania,

Kwa hakika libarikiwe sana tumbo lililombeba mama Samia, lilibeba mtoto aliyekuja kuwa kiongozi wa Tanzania, kiongozi mwenye upendo, hekima, busara, ukarimu, huruma, unyenyekevu na usikivu.

Kiongozi asiye na makuu wala makidai, kiongozi mwenye kujishusha na kujua kuwa pamoja na madaraka yake makubwa kiuongozi lakini bado anabaki kuwa mwanadamu aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu.

Kiongozi ambaye pamoja na uwezo wake mkubwa kimamlaka lakini anatambua kuwa yupo Mungu ambaye ndiye anayepaswa kuabudiwa na kupewa sifa na utukufu, kiongozi ambaye wakati wote madaraka yamemfuata yeye kutokana na kupewa kibali na Mwenyezi Mungu.

Kiongozi ambaye mikono yake ameinyoosha katika kuwafuta machozi na kuwapatia haki wenye kuonewa, kiongozi ambaye ulimi wake umewaponya na kuwafariji wenye majeraha na makovu.

Ni kiongozi ambaye hajawahi kufurahi wala kuwa tayari kuongoza taifa la watu wanaolia na kububujikwa machozi kwa kuonewa, hajawahi kuwa tayari kimaneno na hata kimatendo kuhubiri uonevu, ukatili, ubaguzi na hata chuki kwa watu.

Ni kiongozi ambaye ulimi wake muda wote ni wenye kutoa maneno ya upendo mshikamano na kujenga umoja wa taifa.

Ndio sababu ya kuungwa mkono na Watanzania wote, ndio sababu ya kupendwa na kuombewa afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia Watanzania, ndio sababu ya kusikilizwa na kufuatiliwa sana kwa hotuba zake, ndio sababu ya kuteka hisia na mioyo ya Watanzania, ndio sababu ya kukubalika kwake na makundi yote, ndio sababu ya umaarufu na ushawishi wake kuwa mkubwa sana Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania.

Rais samia ni nuru katikati ya giza, ni tumaini katikati ya waliokata tamaa, ni faraja kwa waliao, ni mpatanishi wa kweli, mpenda haki na mtenda haki, ni Nyota ya alfajiri iletayo matumaini ya pambazuko lililojema.

Ndio sababu ya kila Mtanzania kuwa na matumiani ya pambazuko katika maisha yao na ndoto zao, kila mmoja anao uhakika wa kutimiza ndoto zake na kufikia mafanikio anayoyataka.

Serikali yake imekuwa kwa ajili ya kuwasaidia watu, kuwawezesha na kuwashika mkono katika kufikia malengo yake. Serikali yake haipo kwa ajili ya kumuonea mtu, kumdhuru mtu, kumtesa mtu, kumliza mtu.

Ni serikali safi ya haki yenye matendo mema na hatua njema, ni serikali yenye dhamira ya kuwatumikia watu kwa upendo na uzalendo mkubwa.

Ndio sababu ya kuona mioyo ya Watanzania ikiwa haina hofu wala wasiwasi, kila mmoja anayo amani moyoni mwake, kila mmoja anayo imani na serikali hii, kila mmoja anaridhishwa na utendaji kazi wa serikali ya Rais Samia.

Viongozi aina ya Rais Samia hawazaliwi kila siku wala hawapatikani kila mahali, maana wenye moyo kama wake wa kuweza kumsikiliza kila mtu, kumvumilia kila mtu mwenye kutofautiana nao, wenye kifua kama chake, wenye kusikiliza sauti zote hata zikwaluzazo kwa lugha za ukakasi, kukaa mezani na yeyote, kujumuika na yeyote ni wachache sana.

Viongozi aina yake huja kama mitume kwa ajili ya kuwatumikia watu kwa haki na upendo. Huja wakiwa wameandaliwa na Mwenyezi Mungu, hawaandaliwi na wanadamu wala kwa mipango ya wanadamu, huja wakiwa wamepewa maaarifa na njia za kuongaza.

Mwenyezi Mungu huwapa kila kitu kama ilivyokuwa kwa Musa, huja wakiwa na kibali mkononi cha Mwenyezi Mungu katika ulimwengu wa kiroho. Huja kwa makusudi maalumu, huja kama nyota katikati ya giza, hung'aa na mwanga wao huwa tumaini la watu waitazamayo nyota hiyo, huja wakiwa na majibu ya maswali.

Ndio sababu ya kuona Rais Samia akiwa kipenzi cha Watanzania, ndio sababu ukiona Rais Samia hakauki midomoni mwa Watanzania kwa mema. Amejiandikia ukurasa wake na anaendelea kuandika kitabu chake kitakachosimuliwa vizazi na vizazi kwa mema mengi na makubwa aliyolifanyia Taifa letu yanayobaki kama alama katika mioyo ya watu.

Rais Samia kwake haki ndio kipaombele kwa kuwa anatambua ya kuwa haki huinua taifa. Ni heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi na ufahari wa kidunia.

Rais samia amechagua jina jema kwa kutenda mema kwa Watanzania, yanayomfanya kuwa chaguo la Watanzania kwa muhula wa pili, yanayomfanya apendwe na kuzungumzwa vyema na watu wa makundi yote, rika zote, jinsia zote na vyama vyote.

Rais Samia pamoja na madaraka yake makubwa, ukubwa wa kimamlaka alionao mikononi mwake na katika ulimi wake kikatiba na kisheria, lakini bado anatambua ya kuwa yeye ni mwanadamu na kwamba anayestahili kuabudiwa na kupewa sifa na utukufu ni Mwenyezi Mungu pekee na siyo mwanadamu.

Ndio sababu ya kuwa mnyenyekevu muda wote, mwenye kujishusha na kuwasikiliza watu wote pasipo ubaguzi wala kuwagawa kwa misingi ya ukabila, udini na ukanda, ndio sababu ya kuongoza taifa kwa haki na upendo.

Libarikiwe tumbo lililombeba Rais Samia, maana matumbo mengine yanaleta watu Duniani wanaokuja kuleta mateso kwa watu, uchungu katika maisha ya watu, simanzi kwa watu, machozi kwa watu, maumivu kwa watu, giza katika mioyo ya watu, majeraha na uvuli katika mioyo ya watu, kumwaga damu za watu, kunyonga watu, kuua watu, kukatisha na kuzima ndoto za watu, kushindana na Mwenyezi Mungu anayewapa watu pumzi ya kuishi.

Tujitahidi kutenda mema tukiwa hai kwa kadri tuwezavyo ili matendo yetu yasimame kututetea tukiwa hatuna uwezo wa kujitetea wala kufungua vinywa vyetu. Ya Duniani ni ya kupita tu, yanini kuumizana, kutesana, kukatishana ndoto, kujengeana chuki, kuuwana kwa sababu ya mali au madaraka au vyeo?, nani anazikwa navyo?

Kazi iendelee, Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627

Tangu umesikia ana account jf kijana Una mwanga masifa tu
 
Tangu umesikia ana account jf kijana Una mwanga masifa tu
Mimi naandika ukweli siku zote juu ya Rais wetu mpendwa mama Samia katika uchapa kazi wake na aina ya uongozi wake katika kuwatumikia watanzania,Kama unaona nimepotosha mahali waweza nipinga kwa hoja
 
Back
Top Bottom