Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,920
Nilimtembelea jamaa yangu mmoja,wakati naingia getini kwenye nyumba anayoishi,nilimuona akikurupuka na kuingia ndani,nilipokaribia eneo alilokua nikaona kuna vyombo jamaa alikua anaosha,kuingia ndani nilimkuta jamaa pamoja na mkewe,mkewe alikua anapika,nilifanya kilichonipeleka pale ambacho ni salamu na baadae nikaondoka.Jana jumapili,nikiwa na jamaa yule aliekimbia aliponiona,tulikwenda kumsabahi jamaa anaefanya nae kazi,tulipofika tukamkuta jamaa yake huyo anafua nguo zake pamoja na za mkewe,tulimsabahi kisha akatukaribisha ndani,tukaingia ndani na kumkuta mkewe anapika,akatukaribisha na mazungumzo yakaendelea,muda ulipofika wa kuondoka jamaa akatusindikiza,tulipotoka getini,jamaa yangu ilibidi amulize jamaa yake,"hivi inakuaje unafua wakati mkeo yupo?"jamaa akamjibu,"mimi na mke wangu ni waajiriwa,nachoka nae pia anachoka,so lazima na nyumbani tusaidiane" jamaa akauliza huoni aibu kufulia nje watu wanakuona,si watasema umewekewa limbwata?Jamaa akajibu "yule ni mke wangu,si nampenda bana?Ya nini nione aibu au niogope watu ambao ndoa yangu haiwahusu?Ndipo jamaa yangu aliposema kuwa huwa anaogopa sana watu kumsema na ndo maana alikurupuka aliponiona nilipomtembelea. . . . Sio siri huyu jamaa alinishangaza sana,iweje aogope macho ya watu kumsaidia mkewe?Nilimpongeza yule anaemsaidia mkewe bila kuficha,aibu ya nini bana?Si mkeo?Si unampenda?Achana na akina Asprin na The Boss watakaokuambia "umeshikwa na mkeo we msaidie bana,watasema mchana usikuwatalala!
Last edited by a moderator: