Sakata la Harmonize & RayVanny: Ni utoto, sema tatizo wana hela

Coloneli

Member
Aug 24, 2020
35
151
YES, kwa vigezo vyovyote, hawa wasanii wawili, Konde Boy na Ran Vany, ni watoto. Sio kiumri pekee, lakini hata kimuziki.

Katika umri, ni daraja moja na watoto weeeengi waliopo Bongo Fleva hivi sasa, ambao nyakati zinawabeba kwa sababu ya mitandao ya kijamii na tofauti na kaka zao, wana hawana bughudha yoyote kutoka kwa Wahindi. Sina uhakika ninaposema wahindi kama wananielewa hawa watoto. Wasanii wa siku hizi wanapata hela hata kama wasipopata nafasi ya kupanda jukwaani.

Kaka zao iliwalazimu kutengeneza albamu kama watataka kupata hela na zaidi, hawakuwa na uwezo wa kuidhibiti albamu hiyo sokoni. Na ndiyo maana kuna watu walijitengenezea 'ufalme' wa sanaa ya muziki japo hawakuwa wanamuziki. Kama hupati nafasi ya kuperfom jukwaani, utapataje hela? Wameikuta sanaa katika mteremko, kiasi kwamba kwao imekuwa rahisi mno kutoka. Wakongwe waliopo katika muziki, sidhani kama wanayo furaha wakiona jinsi hawa watoto wanavyopiga hela kirahisi wakati wenyewe walihenya kwelikweli.

Leo hii, Profesa Jay anakwenda kufanya mahojiano katika redio na televisheni inayomilikiwa na Diamond Platnumz, mtoto ambaye wakati Jay akiwa katika zama zake, alitamani hata kushika tu pale aliposhika ili kuipa furaha nafsi yake. Kama muziki ungetenda haki bila kujali nyakati, leo hii Sugu angekuwa anamiliki kiwanda kikubwa tu cha kutengeneza vinywaji vikali vinavyouzwa zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Lady Jaydee leo hii, pengine angekuwa ndiye mkulima mkubwa zaidi wa nafaka kwa nchi za Sadc, hivyo kuingiza mamilioni ya shilingi akiwa na ofisi katika nchi zote hizo.

Wachache waliofanya vizuri wakati huo, walifanya hivyo pasi na kuwa na kile leo wanachokiita menejimenti, maana wengi wa namna hiyo walikuwa ni wanyonyaji.

Na bifu hazijaanza leo, zilianza zamani tu ndani ya Bongo Fleva. Ingawa nyingi ya bifu za zamani zilitengenezwa ili kuwanyoosha walioenda kinyume na walioushika muziki, lakini zilikuwepo. Watu walishindana kwanza kwa kuandika mistari mikali na yenye funzo ndani yake, ndipo zinakuja tambo.

Hawakufikia hatua hii ya hawa watoto wawili kuanza kuanikana na kujipa aibu inayozuilika. Licha ya utoto wao, lakini kinachowapa jeuri ya kuuleta utoto wao mbele ya watu wazima, ni uwezo wao wa kifedha pia. Watoto wana hela. Wanaweza, bila wasiwasi wowote, kusafiri na kwenda kutanua popote duniani. Unapopata uwezo huu, halafu ukiwa bado mtoto, ni mara chache busara inakuwa upande wako.

Wangekuwa na akili baada ya kupata hizo fedha zao, wala tusingesikia ujinga huu unaoendelea. Baada ya Konde Boy kutoka pale Wasafi, kama watoto wote walivyo, anaamini lebo kama lebo haijapenda na hivyo itamfanyia mizengwe mingi kumkwamisha. Ukisikiliza nyimbo za Konde Boy baada ya kutoka Wasafi, utabaini hiki ninachokisema. Ana madongo flani hivi ya waziwazi na mlengwa wa hizo jumbe ni Diamond.

Bahati nzuri, Diamond ni next level. Anajua yeye kama yeye hadhi yake kimuziki ni kubwa kuliko Konde Boy, so ili kutompa mileage, hajibishani naye. Kazi hiyo inafanywa na menejimenti yake. Harmonize analazimisha jamii ione WCB ni wabaya wake. Kama kuondoka kwenye chama lao ni sababu ya chuki, mbona hatusikii hayo mambo yakifanywa kwa Rich Mavoko, ambaye mimi binafsi naamini Mavoko ni msanii mkubwa kuliko Harmo?

Baada ya kuona Diamond hajibishani naye, akageukia kwa wasanii wa levo yake. Nani haelewi jinsi Konde Boy alivyokuja juu, baada ya Ran Vanny kuleta utoto wake kwa kuvujisha video akiwa na yule mtoto mwenzie kimahaba? Na utoto wao ulianzia hapo. Hakukuwa na sababu yoyote kwa Ran Vanny kuwaambia watu kuwa anatoka na yule mtoto mwenzie. Ninafahamu kuna wasanii wenzake walijua, akiwemo Harmonize, lakini hawakuwa na ushahidi.

Kitendo chake cha kuvujisha ile video kiliwapa watu nafasi ya kuongea. Mimi nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa Kajala hakuwa akijua kama mtoto wake yupo na huyu dogo wa WCB. Kitendo cha kusema sijui Mobeto ndiye aliyempeleka huko lanchi, ni kutafuta huruma tu kwa jamii na vile yeye ni mama lazima awe na kitu cha kuongea. Harmonize hakupaswa kuja juu namna ile alivyokuja. Mbona kwa wasanii ni jambo dogo na la kawaida tutu? Anaweza kusimama na kuapa mbele ya mola kwamba yeye hajawahi kutoka na under 17? Nitakuwa wa mwisho kulikubali hili!

Paniki yake na nia yake ya kutaka vyombo vya sheria vifanye kazi yake, ilithibitisha chuki yake kwa WCB, na ndiyo maana menejimenti ilikuja juu sana kumpinga kwenye hii ishu. Walijua dogo anataka kuharibu image ya lebo yao. Utoto mwingine ni wa Harmonize mwenyewe. Unapigaje picha za utupu na kumtumia mpenzi au mwanamke unayetamani awe mpenzi wako? Well, inawezekana pengine hakutuma picha za utupu wake au wa mtu mwingine, lakini meseji iliyo wazi hapa ni kuwa Harmonize alikuwa na mawasiliano ya kimapenzi na kile kitoto cha Kajala!

Na upo ushahidi wa kimazingira kuwa meseji hizo alikuwa anapewa RanVanny. Bahati mbaya, kwa utoto wake, alishindwa kutuliza kichwa chake kufanya kazi sawasawa. Angeweza kuvujisha picha hizi bila kutumia akaunti yake. Lakini aliamua kutumia akaunti yake kwa sababu tu alitaka Harmonize ajue kuwa yeye ni nani! Ni utoto tu unaowafanya hawa watoto wafikie hatua hiyo.

Unashangaa ni vipi Baba Levo, Diwani mstaafu naye aliweza kuingizwa kwenye utoto huu na hawa watoto. Haya yote yanafanyika kwa sababu ya kuwa wana fedha. Wanajua mwisho wa siku watapelekana mahakamani na kutakiwa kulipa faini. Watalipa.Wasichojua ni kwamba sheria ina kawaida ya kutotulia. Kosa na hukumu ya jana, siyo itakayohukumu kosa lilelile likifanyika kesho.

Ndiyo maana wasanii wengi huko mbele wanafungwa jela kwa sababu wanajua wanao uwezo wa kulipa faini, hivyo njia pekee ya kuwafanya waheshimu sheria ni jela.

ce[�&��
 
Mimi huwa nashangaa mnaolaumu Hawa wasanii wa zamani kutokuwa sawa kifedha na mali kulinganisha na Hawa wa sasa.

Mimi ninachoona mtu yeyote anayefanya kazi akishindwa kuwekeza matokeo yake huwa sio mazuri kwa maisha yake ya baadae.

Unapopata chance wekeza kwa kadri ya kipato unachopa ili usije juta badae
 
Kweli Mkuu,mbona mr nice alipata pesa kibao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom