A vivid metaphor on the war on corruption (Picha) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

A vivid metaphor on the war on corruption (Picha)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 23, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 23, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mkazi wa Mtoni Kijichi akishiriki kuzima moto uliotekeza makazi ya mama mmoja hivi. Nilipoiangala picha hiyo nilibakia kujiuliza kama juhudi zetu katika mapambano haya zinalingana na uzito wa kazi iliyopo mbele yetu au we are fighting the proverbial "losing battle"? Kweli tunaweza au tuache magari makubwa kufanya kazi hii (assuming the get there on time na wana maji ya kutosha!)
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Picha inatia huruma mno. Tatizo hata wakija huwa wanakuwa eti hawana maji, ila siku hizi huwa hawaji kabisa, manake wakija wakisema hawana maji ni mawe mtindo mmoja. Sielewi kikosi cha zimamoto kiko kwa kazi gani?, WIZI MTUPU.
   
 3. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji,
  Ukiona Chiligati na Kikwete wanatishia watu 'Nyau', ujue kuwa ingawa uzimaji wetu moto umetegemea ka-kikombe, usichoona ni huko juu angani ambako kuna wingu limesheheni kumwaga mvua ya enzi za Noah.

  Ndio maana ule moto wa akina Kikwete, Lowassa, Rostam n.k, unaanza kuwewesuka kupitia akina Chiligati n.k.
   
 4. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
   
 5. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Japokuwa chanzo cha 'MOTO' huu wa kutisha ni mchanaganyiko wa Nishati ya 'ememe,gesi,mafuta' in-shallah Mi-naelekea kufikiri tutauzima tu,swali ni je moto huu umedhoofisha kiasi gani Paa,kuta au hata msingi wa nyumba yenyewe??kama hatuja chelewa sana twaweza anza 'nyumba mpya 2010??'
   
 6. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Hii picha inaonesha jinsi viongozi wetu wasivy juu Priority za wananchi wao na hili ndiyo tatizo ya hata kutotusikiliza sisi
   
 7. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Kuna hii ya Michuzi pia ni kule Bagamoyo, eti gari ya zimamoto imetumwa kutoka Dar!! Imefika hakuna cha kuzima.
  [​IMG]
   
 8. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbogela mkuu salam;
  Kwa hali hii uliyofafanua tutegemee USHIDI WA DAVID (DAUDI) dhidi ya GOLIATH eeeeeeeMUNGU TUSAIDIE>
   
 9. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Gembe,

  Nilisoma kwenye thread moja jamaa kuna jamaa amesema kuwa unasomeshwa na fisadi mmoja masters SA (sijui ya tatu maana ulishawahikutamba humu kuwa unayo). Sijaona ukikanusha wala kukubali sasa hapa unauliza kuhusu priority kama hizo tuhuma ni za kweli jibu si unalo? Nikikusaidia mafisadi wanaiba hela na priority zao ni kujenga mahekalu, magari ya kifahari pamoja na kuwachukua watoto wa maskini wachache na kuwasomesha ili waje walinde mali zao kwenye jeshi letu la polisi, takukuru na waandishi wa habari yes waandishi wa habari.
   
 10. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe kabisa, lakini ndhani hatuwezi kukaa kusubiri Mungu ashushe baraka zake kuja kuamulia ugomvi huu na kumpa mwenye haki haki ya kumiliki nchi. Nadhani Tunahitaji Moyo wa yule Mama Ross Park wa miaka ya 60 huko marekani iliyozaa movement kubwa ya civil rights na baadaye martin Luther King Jr kuonekna kinara. Tunataka akina Ross Park Tanzania, Madagascar leo imekombolewa na mcheza disco, angalia historia ya Ulaya Mashariki inaonyesh kuwa watu simple ndio wakuwategemea kila siku, hawana conflict of interest, hawana cha kupoteza, tuingie huko waliko tuwaamshe waje kusima moto, hawaogopi nguo zao za thamni kunuka moshi wala kuchafuka, wana nguo simple hata zikungua hapo hakuna shida.
   
 11. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji,

  Huko nyuma niliwahi kusema tatizo letu kubwa ni kuwa wengi wetu watanzania, baada ya kuzoea maisha ndani ya hili bonde la kashfa na uchafu, sasa tunaanza kuliona kama makao yetu ya kudumu. Wengine, baada ya kuathirika na uvundo kwenye hili bonde, wamepoteza kabisa uwezo wao wa kunusa, kusikia wala kuona na hivi sasa wanachapa usingizi humo bila wasiwasi - thubutu ufikirie kuwaondoa humo !!

  Kosa kubwa wanalofanya wachache ambao hawajaathirika ni kule kuwa na imani potofu eti wako mashujaa ambao pamoja na kuogelea kwenye uvundo huo, hawanuki kwa sababu wanaweza kujipaka manukato ya muda. Kwa kuendelea kuwakumbatia watu kama hao na kuwapa sifa wasizostahili, tunazidi kulipalilia na kuliwekea mbolea hili shamba ambalo zao lake kuu ni ufisadi - sasa hili zao lingine latoka wapi ?

  Je kuwaita wasafi tukijua wazi wanaishi ndani ya dampo kwenye uchafu, tutakuwa kweli hatuhalalishi maisha ndani ya dampo ? Mafisadi tumewashika pabaya lakini kuwakumbatia washiriki wao kwenye maamuzi mbalimbali yanayoididimiza nchi na kuwaita mashujaa, ni ujinga. Sasa inabidi tubadilishe mbinu ya mapambano na kama hatuwezi kuwatenganisha kwa sababu wameshikamana, lazima tuwaangamize wote.

  Kama unaoga mtoni, ukitaka kukauka ni lazima utoke kwenye maji. Hivyo hivyo tuwakatae kwa nguvu zote wanaooga kwenye tope halafu wanajiita wasafi huku wanaendelea kubaki kwenye tope. Hizi ni mbinu za danganya toto na koleo tuwe tayari kuliita kwa jina lake halisi - hakuna cha Sita. Kilango, Mwakyembe - wote ni hao hao Mkapa, Lowassa, Rostam, Serukamba wakiongozwa na kamanda wao mkuu,
  Jakaya Mrisho Kikwete.​
   
 12. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu solomon salam.
  Mkuu unamaana MAFIA stail (MAFIOSO) basi kazi ipo ya kupambana na watoto wa MAGOD FATHERS kwanza. si mchezo mkuu................!!!!
   
 13. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2009
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkjj,

  Wewe ni Kamanda acha kuonyesha dalili zozote za kuingiwa na wasiwasi! Kumbuka vita za Majimaji na za akina Mkwawa! Starling hauawi - labda ajinyonge mwenyewe. Tutashinda ila tukaze buti maana hawa mafisadi wamesambaza agents wao sehemu nyingi sana ili kujaribu ku -dilute nguvu zetu! Aluta continua Kamanda na tutashinda tu, kwa sababu hakuna option ya pili!
   
 14. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  It won't be easy, lakini tusikate tamaa, sasa ndio tunahitaji ushirikiano wa viungo vyote vya mwili, ubongo ukichukua nafasi kubwa, huenda kikombe ndio silaha kubwa sana ya kuuzima moto kuliko magari ya hawa jamaa wa fire, lakini kama wote tutashika hicho kikombe na kuumwagia moto kwa wakati mmoja kwa uwingi wetu moto utazimika. Tatizo letu wengi tunapenda kuwa watazamaji, huku tukitamani kuwa na nchi ya asali na maziwa waliyoitengeneza watu wengine, we do not want to be part of the picture in the making, happy to enjoy the cake!! Kama huu uchungu tulionao hapa ungekuwa contagious huko mitaani na vijijini, hatungehitaji gharama kuuzima huu, huenda pumzi zingetosha!!
  Dk.Slaa alivyoanza kuuwasha pale Mwembeyanga, wengi walimwona kachanganyikiwa, lakini mpaka leo facts zinaeleweka, huenda tunahitaji kuonekana kama tumechanganyikiwa watz wote, wakija na pumba zao washangae.
   
 15. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sikubaliani na wewe, wananchi kwenye nafasi zao wanajitahidi. Vijana wamanzeshe wemepurukushana na mapolisi. Wananchi vijijini wanalia ardhi, wanafunzi vyuoni wanalia cost sharing. Walimu wanataka kugoma kila leo. Tatizo sio wananchi, wananchi wapo tayari kama simba. Tatizo sisi watu wa katikati, ambacho tunachokidogo, ndio tunahofu ya kupoteza. Lakini sio walalahoi hata kidogo. Kwanza, wao wapo vijijini wanaendelea kulima na kutulisha, wapo kariakoo wanabeba magunia, wapo majumbani ni wasafisha nyumba. wapo mitaani hawana kazi - kila siku wanaongea matatizo waliyonayo. Ni sisi wa katikati, ambao hatujui tunataka kutetea haki za walalahoi ama kuendealea kutembea na walionacho! Tupo njiani panda, basi hofu imetutanda! msukumo wa maisha unatukimbiza, mwaka unapita! unahofu oh! sina kibanda, gari, hadhi na mambo kibao. Basi fikira zimejazwa mahitaji ya nyakati. Ndio sisi, tujitizame sisi!
   
  Last edited: Mar 24, 2009
Loading...