Tulipata mgeni kijijini kwetu akitokea huko pande za kusini mwa nchi yetu. Akajitambulisha kuwa anaitwa "Saa nane" na wote kijijini tukamjua kwa jina hilo. Akajiunga na sisi ktk kazi za kilimo na vibarua vya kutengeneza barabara. Siku moja akaja mgeni mwingine lakini huyu alikuja kwa nia ya kumtafuta mjomba 'ake anayeitwa "Jua kali". Hakukuwa na mtu anayeitwa jua kali kijijini kwetu. Kila aliyeulizwa hakumfahamu mtu anayetafutwa.
Akiwa amekata tamaa ya kumpata mwenyeji wake akamwona mjomba 'ake anapita ikawa hivi:-
Mgeni:- (akaita kwa sauti ya juu kabisa) njombaaaa, njombaaaa, njomba Juakaliiiiiiii.
Wenyeji:- Huyo mbona sio Juakali huyu anaitwa mzee Saanane.
Saanane:- Nyinyi nchindanganye mwenjenu. Kwani kila chiku jua kali linawaka chaa
ngapi chi chaa nane, nnajifanya hanjui eeh. Baaaa njini hapaa.