A Golden Opportunity! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

A Golden Opportunity!

Discussion in 'Jamii Photos' started by MNDEE, Nov 22, 2009.

 1. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Documentary ya wachimbaji wadogo wadogo - maisha bora kwa kila mtanzania!

  [ame="http://vimeo.com/7690704"]http://vimeo.com/7690704[/ame]
   
 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  MNDEE,

  Shukran kwa video hiyo

  Hapa najiuliza sasa eti JK anaenda kumuambia Mugabe ashughulikie mambo ya wananchi wake..........i mean what a joke........

  Kinachonishangaza zaidi ni kuona wananchi wa mameneo hayo hayo wanzidi kukpigia kura Chama Kilichowaletea maafa ya kila aina.............safari ni ndefu sana
   
 3. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Tatizo wananchi ni wepesi kusahau, na hudanganyika kirahisi kwa ahadi hewa zinazoambatana na takrima.
   
 4. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Tatizo uelewa na ujasiri wa kuthubutu watanzania wa sasa ni waoga sana na hawajali ni sawa na watoto hudanganywa kiurahisi kwa kupewa kofia na kanga,ukiangalia angalau kidogo mijini kuna muamuko wa kujua mazuri na mabaya,huko vijijini ndiko kuna ukosefu mkubwa wa huduma na ndiko kuna watu wengi lakini unapowaambia CCM ndio imewafikisha hapo na angalieni upande mwingine hawakuelewi wanakuona mhuni sasa watu wavijijini mpira ndo huo uko kwenu,chagueni kusuka au kunyoa
   
 5. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Hakuna mabadiliko lakini mwaka nenda mwaka rudi viongozi wale wale wanarudi kuomba kura na wanachaguliwa. Tatizo linaanzia kwenye chombo kinachopitisha wagombea, wenye nazo na 'wenzetu' ndio wanapitishwa. Pia kukosekana kwa upinzani serious nako ni tatizo, wananchi wakitupiwa pilau, fulana na doti ya kanga mchezo umekwisha.
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Bado Vyama vya ushindani havijafanya kazi nzuri huko vijijini. wao hufika huko wakati wa uchaguzi zaidi kulik nyakati za kawaida........hili ni tatizo na wasipoli-address CCM wataendelea kushinda....kwani wao wanaonekana sana kuwa wako karibu na wananchi.....
   
 7. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa nao ni yale yale uroho wa madaraka, ubinafsi na ufisadi ndio kinachowapeleka ikulu. Kama wako serious na wana uchungu na nchi hii hata kama hawaungani wangesimamisha mgombea mmoja anayekubalika na mwenye sifa aende sambamba na CCM.
   
Loading...