Junior. Cux
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 5,319
- 3,798
Nimeona tukumbushane mambo muhimu kidogo katika jumapili ya leo. Taifa bila virusi vya ukimwi inawezekana, jitahidi kufanya haya:
Sio mbaya tukaelezea changamoto mbalimbali tunazokutana nazo katika jitihada za kujikinga na ugonjwa huu na jinsi gani tunaweza kukabiliana nazo, ushauri wako leo unaweza kuwaokoa mamilioni ya watu siku za mbeleni.
sharing is caring....
- Tumia kinga kila mara unapokutana kimwili. huwezi kumjua muathirika kwa kumuangali, wala usimuamini mtu kwa macho kwa vile kasema yuko vizuri, matumizi ya kinga yanaweza okoa maisha yako kwa kiasi kikubwa.
- Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu. baadhi ya watu hawafurahii tendo wakitumia kinga either kwa michubuko au maumivu, ni vema ukatafuta mpenzi mmoja muaminifu mtakaeweza kushiriki nae.
- Acha kujamiiana. kama hujapata hata mmoja mwaminifu basi ni vizuri ukasubiri na kuacha kushiriki tendo mpaka pale utakapofanikiwa kumpata.