Tatizo la Uke Kuwa Mkavu: Chanzo, Suluhisho na Ushauri

stable woman

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
3,887
4,467
2391014_Dry.jpg


Habari zenu?

Jamani ningependa kufahamishwa nini kinachopelekea ukavu sehemu za uke wakat wa tendo. Je, ni vyakula duni, uchache wa maandalizi au upungufu wa nguvu za kike?

Nawasilisha


WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUFAHAMU UNDANI WA TATIZO HILI
Ushawahi kukutana na mwanamke ana uke mkavu sana yani hana ute, tatizo linasababishwa na nini? Tiba yake ni ipi? Maana unatumia mate weeee kulainisha njia mpaka yanakauka mdomoni.
Naomba kujuzwa juu ya hili tatizo kwa wanawake, tatizo la kuwa na uke mkavu. YaanI hata aandaliwe vipi anakuwa mkavu japo inafikia hatua yeye analegea kabisa na anaomba aingiliwe lakini bado uke unakuwa hauna hata unyevu.

Kipind cha ujauzito alienda hospitali kumbe ni kawaida kwa wanawake kutokwa na uchafu kipindi wakiwa wajawazito lakini yeye huyu hamna hata uchafu uanaomtoka, yaani ni mkavu kweli.

Wakuu nini husababisha hyo hali?


MICHANGO YA WADAU
SI JAMBO GENI, JARIBU KUZINGATIA HAYA

Siyo jambo geni sana hili. Wapo ambao siyo wakavu wakati wengine ni wakavu. Lakini ziko sababu ambazo zinaweza kumfanya awe mkavu au asiwe mkavu.

Sexual stimulation ya kutosha kupitia foreplay inasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa ukavu. Aina ya vidonge vya uzazi anavyotumia vinaweza kuchangia kuongezeka kwa ukavu.

Zipo pia sababu nyingine kama mabadiliko kwenye hormones za kike, premature menopause, kuwa katika dozi ya dawa fulani, allergy na aina za kemikali zilizopo kwenye vitu kama sabuni, perfume, n.k na mwanamke kujikita zaidi kwenye kulea mtoto.

Pia sababu inaweza kuwa ni psychological au emotional related kama stress, woga, wasiwasi, bond aliyonayo kwako, wewe mwenyewe, n.k.

Treatment inategemea na sababu ya huo ukavu. So, the first thing ni ku-diagnose cause ya ukavu.

Usianze tuu kutumia lubricants na vaginal moisturizers kama baadhi walivyopendekeza. Tafuta kwanza chanzo cha kuwa mkavu.

Na katika kutafuta chanzo kunahitaji ushirikiano mkubwa baina yenu, ikiwa ni pamoja na kwenda kwa wataalam pamoja kama nyie wenyewe mkishindwa ku-diagnose chanzo.

Labda anza kwa kumfanya aji-feel more loved and wanted than ever kama bado hufanyi hivyo. Hapa naama kuwa kugegedana iwe sehemu ndogo sana badala ya sehemu kubwa kila mnapofanya mapenzi.

Wengine wanakuwa so turn-in na kulowa kwa kuambiwa genuinely ni jinsi gani they are wanted or desired and how good they make you feel.

Badilisheni sehemu na style za kegegedana. Siyo lazima mgegedane maskani too au kwenye kitanda hicho hicho.

Pia don't forget the tale of woman's confidence. Some like it veeeeeery dirty than most men would think of. Na mwanamke who like it dirty does not necessarily mean that she is a slut.
JARIBU KUFIKIRI HAYA

Demu huyo anaweza kuwa hivi:
  • Ana upungufu wa Estrogen
  • Ana mawazo kibao (usikute alikua anawaza kukupiga mzinga kidding ..ila kweli huenda ana mawazo.
  • Ndo wale walikua wanasafisha K kwa sabuni, fulu kuzipaka lotion na kuzinyunyuzia unyunyu, fulu kuziwekea poda). Sasa kaua Normal Flora wote ukeni
  • Au demu wako yupo katika matumizi ya dawa kwa muda mrefu.
  • Au anasumbuliwa na Sjogrens syndrome

Tiba
Inategemea na kisababishi chake, hivo basi, kiondoa Suala la Estrogen na Utumiaji wa madawa na tatizo la Sjogren's yanayohitaji kufika hospitali.

Hayo mengine ni masuala yako na wewe kukaa na kuhakikisha uke unakua na maji ndo ule mzigo kiroho safi.

Nimeandika kisela ila ndo ivo!!.
SABABU ZA KUKAUKA KWA UKE

Swala la kukauka kwa uke mara baada ya mwanake kufika kileleni ni la kwaida kwa wanawake wengi na huwa na sababu mbali mbali ambazo mimi nitakutajia kwa kifupi tu kamaifuatavyo:

1. Mwanamke huitaji kunyegeshwa tena baada ya bao la lake la kwanza, inategemea lilipopatikana kama kwenye Kipele G, Kwenye Kisimi, Mwisho wa Uke au kuta za uke. Ikiwa amepata bao "via" kisimi hapo lazima atahiji muda kidogo wa kupumzika kama dakika kumi 5+ kisha wewe mpenzi wake ni wajibu wako kumnyegesha tena kwa kucheza na sehemu nyngine za mwili wake mbali na Kisimi. Inaweza kuwa kum-busu, kumla denda huku unamshika-mshika na kadhalika.

2. Mwanamke kuwa na uwezo mdogo wa kungonoana (low sex drive/libido) ni wazi kuwa hamjuani hivyo yawezekana yeye yuko hivyo na mara baada ya wewe kupiga bao la kwanza ksiha kurudi na "kumpigisha" yeye bao lake ndio ilikuwa mwisho wa "game" mpaka kesho au labda wiki ijayo kama sio mwezi mwezi ujao. Kama ulihitaji tena kwenda basi ulitakiwa kumfaya aendelee kuwa "interested" kiakili nakimazingira zaidi ya kimwili na pia ungepaswa kutumia kilainisho kwa ajili ya Condom au hata K-Y Jel.

3. Mwanamke kutokuvutiwa na ufanyaji wako, kama ulivyosema kuwa ilikubidi uache nje-ndani, swala l a kungonoana ni pana na sio kusimamisha kisha kupiga nje-ndani mwanzo mpaka mwisho >>( Kuna wanawake kibao baada ya kibaruti cha kwanza inabidi uanze upya kuwatuliza a.k.a kuwa NYEGELESHA.

Dawa yake kwa wengi usikazanie NJe ndani Nje ndani sana kama ushambarutisha tayari. Cheza sindimba au msondongoma katika mduara bila kuvuta filimbi nje wakati unaASALISHA mambo mengine!Baada yamuda kadhaa wakati unahisi au unasikia pumzi fulani ndio endeleza pupa kama navyohisi unafanya.Hii hasa kama unacheza mkao wa kimishenari).

4. Mwanamke kutokuwa na mapenzi pia inaweza kuwa sababu ya Uke wake kuwa mkavu mara baada ya zile nyege mshindo kumalizika/kumtoka (baada ya yeye kufikia Mshindo), mwanamke kama hana mapenzi huishiwa hamu ya kuendelea kungonoka haraka sana mara tu baada ya bao lake la kwanza.

5. Kuchoka au Uvivu, mwanamke kama kachoka au mvivu hali hiyo ya ukavu ukeni hujitokeza kwa vile akili yake inakuwa haipo/haizingatii kilekinachofanyika bali saa ngapi atapata nafasi ya kwenda kulala/pumzika.

Condom huwa hazisababishi Uke kukauka tena japokuwa inashauriwa kubadili au kutumia kilainisho kilichotengenezwa kwa ajili hiyo. Makampuni mengi ya bidhaa hzi yanatoa mafuta maalum kabisa kwa ajili ya kukuongezea ile hali ya ulaini amabo unakulinda wewe kwa kuzuia Condom kupasuka/chanikakutokana na ukavu wa Uke na vilevile kumuongezea mwanamke raha ya tendo.

Condoms hazimsababishii mwanamke maumivu bali ile hali ya wewe kumfanya mwanamke mwenye uke mkavu kwa muda mrefu ndio inasababisha maumivu.Ili ufurahie Ngono basi ni vema ukatafuta mwanamke mmoja umpendae na yeye akupende na mfanye tendo kwa ushirikiana na kumbuka ku-focus kwenye kufurahia tendo zaidi kuliko kupiga mabao na mambo yatakuwa bomba kabisa.
CHANZO, MATIBABU NA USHAURI

Kwa kawaida kwa kila mwanamke,uke wake unapaswa kuwa na hali ya unyevunyevu kutokana na ute mwepesi unaozalishwa ili kusaidia kuuweka uke katika hali hii.

Hormone inayojulikana kama estrogen ndo inayofanya kazi ya kufanya ute ute huu kuzalishwa ili kufanya uke kuwa na unyevunyevu na kuta za uke kuwa zinavutika(elastic). Pia ute huu husaidia kuweka sawa mazingira rafiki kwa mbegu za kiume,ili zinapokuwa zimeingia zisiweze kufa hadi zinapolifikia yai.

Kushuka kwa kiwango cha hormone ya estrogeni ni chanzo kikubwa cha kupungua kwa ute huu na kufanya uke kuwa mkavu.Kiwango cha hormone kinaweza kushuka kutokana na sababu mbali mbali kama tutavyoona katika makala hii.

Inaweza kuonekana ni jambo dogo,lakini kutokua na unyevunyevu wa kutosha inaweza kuathiri maisha ya muhusika haswa katika swala la kujamiiana.Ikiwemo kusababisha tatizo la maumivu wakati wa tendo la ndoa, na kupata tatizo la fangasi za ukeni mara kwa mara

CHANZO CHA TATIZO
Tatizo la uke kuwa mkavu linawakumba sana watu waliofikia ukomo wa hedhi (Menopause) Kutokana na sababu kwamba mwanamke anapofikia kipindi hiki mwili unapunguza au kuacha kutengeneza hormone hii ya estrogen. Hali hii hupelekea kuta za uke kuwa nyembamba na hazivutiki tena hali ambayo kitaalamu inajulikana kama Vaginal Atrophy.

Kiwango cha estrogen kinaweza pia kushuka kutokana na vitu vifatavyo:

1.Kuzaa na kunyonyesha. Kipindi hiki mwili unazalisha hormone ya maziwa (prolactin hormone) ambayo pia inazuia kuzalishwa kwa hormone ya estrogen.
2.Matibabu ya saratani. (Tiba ya mionzi na dawa za saratani)
3.Kutolewa mifuko ya mayai( ovaries)
4.Dawa zinazozuia uzalishwaji wa hormone ya estrogen kwa watu wenye tatizo la Uvimbe kwenye kizazi, (fibroids na endometriosis)

SABABU NYINGINE ZA UKE KUWA MKAVU NI:
SJOGREN SYNDROME ,Huu ni ugonjwa ambao kinga ya mwili inaharibu cell zinazotengeneza huu unyevunyevu
Dawa kutibu mzio( allergy) na mafua
Kusafisha uke hadi kwa ndani (douching)
Kusafisha uke kwa kutumia sabuni zenye kemikali
Kutoandaana kabla ya kufanya ngono.

UCHUNGUZI
Unapopata muwasho,au maumivu wakati wa tendo la ndoa na kuona uke wako ni mkavu vyema ukafika hospitali au ukawasiliana na daktari.Daktari atakuuliza maswali muhimu ili kubaini chanzo cha tatizo na atakufanyia vipimo na uchunguzi na atajua dawa gani inafaa.

MATIBABU
Matibabu yaliyozoeleka katika hili tatizo la ukavu ukeni ni kwa kutumia Estrogeni za kupaka au kupachika ukeni (topical estrogen),
Pia estrogen inaweza kuwa kaitka miundo mbali mbali kama ifatavyo:

Ring (estring) Hii inakua ni kitu cha duara kama pete ambacho mtu anawekewa ukeni,kinakua kinazalisha hormone ya estrogen,na kinabadilishwa kila baada ya miezi mitatu

Vidonge (Vagifem),Vidonge hivi ni bya kupachika ukeni vinakua na kifaa chake maalumu cha kusaidia kuviingiza ukeni.Unapachika kidonge kimoja kwa siku ndani ya muda wa week mbili.

Dawa za kupaka /cream (Estrace na Prematin)
Dawa hizi unapaka ukeni kila siku kwa muda wa wiki mbili.

MUHIMU: Dawa zenye Estrogen zinakuwa na maudhi madogo madogo (side effects) kama matiti kuvimba na kuuma na dawa za estrogen hazipaswi kutumiwa na watu wenye matatizo yafuatayo:
Saratani ya matiti
saratani ya shingo ya kizazi
Wajawazito na wanonyonyesha


SABABU YA UKAVU WA UKE WAKATI WA KUJAMIIANA (TENDO LA NDOA)

Via vya uzazi vya mwanamke vimeundwa kwa hali ambayo inaweza kukabiliana na aina kama tatu za vitendo ikiwemo kujifungua, tendo la ndoa (kujamiiana) na kutolea uchafu (mkojo na damu ya hedhi). Kila kitendo kina mazingira au hali tofauti kukamilisha kitu husika, maandalizi ya mwili kujifungua ni tofauti na maandalizi ya mwili kwa tendo la ndoa. Wakati wa kushiriki tendo la ndoa ni muhimu kwa mwili wa mwanamke kupitia homoni zake kutengeneza na kutiririsha ute ambao hurahisisha upenyaji wa maumbile ya mume na kuepusha michubuko kutokana na msuguano.

Sababu zinazopelekea ukavu wa uke

Maandalizi hafifu au mabaya. Mwanamke ili aweze kushiriki kikamilifu katika tendo la ndoa inahitaji aandaliwe kwanza kabla ya kuanza tendo lenyewe.Yapo makosa ambayo kwa kusudi au bila kujua wanaume hufanya kwa wenza wao kipindi cha kushiriki tendo la ndoa ikiwemo la kutokumwaandaa vyema mke au mwenza wake.

Bila kujiandaa. Kwa hali ya kawaida tu uwezo wa kusisimka mwili hutofautiana kutoka mtu mmoja na mwingine. Wapo watu ambao wakishaona tu maumbile ya mwanaume wakiwa eneo husika hupata msisimko haraka na kuwa tayari kuingiliwa bila shida yoyote, lakini wengi ni muhimu kutumia muda kidogo kuuandaa mwili wake (zipo homoni zinazalisha maji/uterezi/ubichi ukeni) ili kumweka katika njia ya tendo la ndoa.

Maambukizi. Baadhi ya magonjwa kama vile fangasi na mengineyo huathiri mfumo wa utendaji kazi kwa mwanamke na kupelekea homoni zinazohusika kutengeneza ute kushindwa kufanya kazi.

Msongo wa mawazo. Mawazo yanpo kuwa makali huleta mambo mengi mwilini ikiwemo kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.Kwa wanandoa mara nyingi hubaki kuwa kama kutimiza wajibu tu.

Upungufu wa nguvu za kike. Kwa matatizo mbalimbali ya kiafya hasa magonjwa ya kudumu kama kisukari na TB pia unywaji wa pombe kali au ulevi wa kupindukia huchangia kupotea kwa utendaji kazi mzuri wa homoni hivyo kuleta ukavu wa uke

Kasoro za mfumo wa uzazi. Mabadiliko ya hali ya hewa,vyakula vipya,madawa ya magonjwa na vipodozi hasa vile vinavyokutana na ngozi moja kwa moja huweza kuleta mabadiliko mazuri au mabaya katika mfumo wa uzazi kwa njia ya kuchochea au kupoteza baadhi ya homoni.

Angalizo: Endapo tatizo hili linaonekana, ni vema kuonana na wataalamu wa tiba kwa ushauri wa kitabibu na badala yake kuacha kubashiri ni tatizo dogo au kubwa.

 
mchicha Mbogq,

Hapo palipokolezewa rangi panahusika. Epuka kumpiga mtama mwezio. Tulieni muongee maneno matamu ya mapenzi ili kuondoa/kupunguza msongo wa mawazo, kupumzika muda wa kutosha pamoja na kula vizuri. Ongeza kasi ya ULAJI WA BAMIA.
 
Kama mwanamke hajaandaliwa vizuri au hayupo tayari kusex .pia inachangia mzongamano wa mawazo na ugumu wa maisha ya kila .inatakiwa mwanamke alilax na awe tayari kwa tendo. Pia kuna baadhi ya magonjwa yanachangia hali hiyo .kwa ujumla zipo sababu nyingi sana.inabidii kumhona doctor kwanza.
 
Majibu unayo ndugu kitu ni maandalizi, andaa msosi wako vizuri kisha upalilie ndo upakue, tena hapo unamuumiza sana yani. ivisha msosi wako vizuri utaona raha wakati wa kula.
 
Msongo wa mawazo
Lishe duni
Maandalizi hafifu na wengine hua ni maumbile tu.

Na mi naomba kuelezwa, nguvu za kike ni zipi?
 
Kama huyo mkeo kakeketwa (Kaondolewa Kisimi) basi analo tatizo kubwa la kutopata hisia za tendo la ndoa. Fanya utafiti wa kumgusa sehemu nyingi za mwili wake utagundua ni wapi panamletea hisia kali. Ukisha pagundua basi kabla ya tendo la ndoa pashike, papapase mara nyingi iwezekanavyo hadi umuone amesisimka ndiyo uende huko mahalaelkubra na siyo kabla kwani utamletea maumivu makali na atachukia tendo lenyewe na wewe pia.
 
Msongo wa mawazo
Lishe duni
Maandalizi hafifu, na wengine hua ni maumbile tu..

Na mi naomba kuelezwa..nguvu za kike ni zipi?

Swali zuri sana hilo.

NGUVU ZA KIKE: = Be yourself. Usijifanye kuwa mtu mwengine. Utapata tu mwenzi wako.

Trust me: mimi ni mwamme na nisingependa kujihusisha na mwanamke anaye-ACT.
 
Nguvu za kike ni kutoku act?
:A S-confused1::A S-confused1:..
Swali zuri sana hilo.

NGUVU ZA KIKE: = Be yourself. Usijifanye kuwa mtu mwengine. Utapata tu mwenzi wako.

Trust me: mimi ni mwamme na nisingependa kujihusisha na mwanamke anaye-ACT.
 
Nini kinasababisha mwanamke ambae hakua na uke mkavu kuwa na uke mkavu wakati wa kusex? Tiba yake ni nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom