Cvez
JF-Expert Member
- May 19, 2018
- 4,471
- 13,626
Mwaka 2015 wakati nipo chuo SUA Mazimbu Campus ilikua majira ya jioni around saa moja siku moja kabla ya UE. Maeneo ya Dark City, Mauki kituo cha daladala kuna sehemu tunakaa kunywa kahawa au tangawizi na karanga. Nimeshakunywa kahawa yangu hapo najiandaa kwenda kupiga msuli wa zima moto. Kuna vijana wanauza kuku pale nikchukua kipaja kimoja pale kisha nikaenda kwa Mangi mmoja hivi anakaanga chipsi nikachukua sahani moja.
Enzi hizo ile mifuko ya plastic bado haijapigwa marufuku. Mangi akanifungia chipsi then nikachukua kile kipande cha kuku nikatumbukiza ndani ya mfuko wa chips. Nikachukua barabara ya kuelekea ghetto kwangu eneo la Makaburini hukohuko Dark City. Mara ghafla naona bodaboda inakuja upande wangu kwa kasi, nikajaribu kuikwepa lakini bahati mbaya ikanigonga kwenye mguu eneo la paja. Bodaboda akaanguka nami nikaanguka. Nashukuru Mungu sikuumia sana zaidi ya maumivu kiasi kwenye mguu na uvimbe baadae, yule dereva nae aliumia kiasi kulikua na wanachuo wengi pale wakataka kumpiga ila akaomba msamaha yakaisha.
Kumbuka mwanzoni nilisema nilikua nimebeba mfuko wa chips ndani yake kuna mfuko wenye kipande cha kuku. Kitu ambacho mpaka leo sielewi ilikuaje wakati naamka kutoka chini nilipoanguka mkononi nilikua nimeshika mfuko wenye kipande cha kuku ule wa chips ulianguka chini. Mpaka leo natafakari ilikuaje nikaweza kudaka mfuko uliokua ndani hali ya kua mfuko ulio nje nilishindwa kuuzuia?