A boy from Tandale: Albamu bora ya muda wote Tanzania

el nino

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
4,712
5,033
Katika historia ya muziki wetu Tanzania kumekuwepo album nyingi mno hasa kipindi cha miaka 15 iliyopita ambapo bado album za wanamuziki zilikuwa na soko kubwa hapa Tanzania.

Nafahamu album nyingi sana za wasanii wa Bongo ambazo zinastahili heshima yake hasa kwa mapinduzi makubwa katika muziki wetu pamoja na ubora wake, kwa haraka niliwahi kuandika uzi kuhusu album hizo ambazo miongoni nilizitaja MACHOZI JASHO NA DAMU ya PROF J, A.K.A MIMI ya NGWAIR , KAMANDA ya DAZ NUNDAZ, SAUTI YA DHAHABU YA T.I.D na nyinginezo nyingi ikiwemo iliyokuwa inaongoza kwa mauzo ya Mb dogg.

Katika soko la album la zamani wasanii wengi walikuwa wanalalamika kuwa hawafaidiki na mauzo ya hizo album, na waliongeza kuwa waliokuwa wanafaidika ni wahindi pamoja na wadau wengine wachache kitu kilichopelea soko la album kudorora ama kupotea kabisa mpaka wasanii walipoibuka miaka hii miwili iliyopita na kuanza kutoa album kama Navy kenzo na Vanessa mdee.

The rise of Dimond platnumz.

Mwaka 2009 wakati anga la muziki wa bongo likisumbuliwa sana na vijana wabichi kutoka T.H.T ,aliibuka kijana kutoka Tandale, wengi walihisi amebahatisha kwa wimbo wake wa kwanza ambao ulipelekea kuzoa Tuzo 3 za kili kitu ambacho hakikuwahi fanyika kabla, baada ya hapo akaendelea kuzikomba tuzo za kitaifa na kimataifa na tokea huo mwaka haina shaka ndiye msanii nambari moja afrika mashariki.

Kwanini "A boy from Tandale " ndiyo album bora zaidi kwenye historia ya bongo fleva.

1.
Imesheheni hits kibao, sio tuu album inabebwa na msanii mkali bali imesheheni ngoma kali sana zikiwemo zilizobamba na kukamata chati mbalimbali afrika mfano, number 1 remix, nana ft Mr flavour, Sikomi,Kidogo,Marry you ft Neyo, Eneka, Hallelujah ft Morgan Heritage, Waka Ft Rick Ross na my favorite Baila.

2. Ina nyimbo zilizoangaliwa zaidi ya mara milioni 100 Youtube, ukienda youtube sasa hivi ukaangalia nyimbo zilizomo kwenye album ya a boy from tandale utaona zimeangaliwa zaidi ya mara milioni 100 (jumla yake),kitu ambacho hakipo na hakijawahi kutokea kwa msanii yeyote tTanzania na afrika mashariki na kati.

3. Ni album yenye tuzo nyingi zaidi afrika, chukua idadi ya Tuzo alizopata na wimbo wa My number 1 remix(zikiwemo 7 za kili na nyingine kibao), chukua idadi ya tuzo alizozoa kupitia Nana(ikiwemo ya Mtv world), hallelujah na nyimbo zingine utapata hitimisho kuwa hakuna album bongo iliyowahi ksheheni nymbo zenye tuzo nyingi kama "A boy from Tandale" na huenda haiongozi tuu afrika mashariki na kati bali afrika nzima.

4. Idadi ya wanamuziki wa kimataifa walioshirikishwa, katika kuchanganya ladha ya muziki wetu na sehemu nyingine album ya a boy from tandale imechanganya ladha ya muziki kutoka pande mbalimbali za dunia, kutoka Jamaica kuna Morgan Heritage, kutoka USA kuna Omarion, Rick ross na Ne-yo, kutoka Nigeria kuna Davido, flavour na Psquare bila kusahau ethiopia kuna miri ben ari.

5.Nyimbo zilizomo kwenye hii album zimempa show nyingi zaidi hasa za kimataifa tofauti na album za msanii yeyote yule hapa bongo.


kwa sababu hizi 5 na nyingine nyingi tuu ambazo nimeacha kuzitaja sababu ya muda, nahitimisha kuwa kwa vigezo vya ubora, mafanikio na impact yake kwenye soko la muziki, album ya Dimond platnumz 'A boy from Tandale" inasimama kama album bora zaidi kwenye historia ya muziki wetu Tanzania.


imgres



areachood@gmail.com
 
Album ni nzuri sana lakini kusema ni bora kuliko zote zilizowahi kutoka napata ukakasi kidogo, ila sio mbaya maana ni mtazamo wako mkuu. Napenda nyimbo mond amefanya na Young killer kwenye hiyo album
Pamela
 
Album ni nzuri sana lakini kusema ni bora kuliko zote zilizowahi kutoka napata ukakasi kidogo, ila sio mbaya maana ni mtazamo wako mkuu. Napenda nyimbo mond amefanya na Young killer kwenye hiyo album
Uzuri mmoja nimetaja na vigezo
 
Unaweza ukakuta msanii ana collection ya nyimbo 200 lakini ana album 10 . Diamond hana album bali anatoa collection ya nyimbo zake zote tangu alipoanza kuimba.
Unaona unavyobugi.. A boy from tandale ni album yake ya pili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom