A Black Christian is a Traitor to the Memory of his Ancestors | Africa Wake Up

Tuimarishe vilinge vyetu vya kutambikia ili vifanane na 'altare " ya kuabudia. Tumeua vyetu tukafuata vyao! Ni uungwana!!! Usioe au kuolewa ili ufanye kazi ya Mungu! Tuamke sasa! Au tumsubiri Karl Marx afufuke atuamshe!

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Unamsubiri Mzungu? Hongera, ila yule ameshaaga dunia. Subiri tu... (Haraka haraka haina baraka...)
 
BOOK SUMMARY: WHITE POISON

(A Black Christian is a Traitor to the Memory of his Ancestors..Africa Wake Up !)

MWANDISHI: Kayemb “Uriël” Nawej

MCHAMBUZI: Ghost Writer()

Tuanze kwa kumnukuu Rais wa kwanza wa KENYA Bw. Jomo Kenyatta kipindi cha uhai wake aliwahi kusema kwamba;-

"Wazungu walipokuja Barani Africa, walitukuta tuna Ardhi yenye rutuba, na wao walikuja na Biblia, Wakatufundisha kusali tukiwa tumefumba macho, na tulipofumbua macho baada ya kusali walikuwa tayari wanamiliki ardhi yetu na sisi tukapewa Biblia.."

Sasa twende mdogo mdogo tuone alikuwa anamaanisha nini

Tukirudi nyuma mpaka mwaka 1883 huko Ubelgiji Mfalme wa ubelgiji KING LEOPOLD II alitoa hotuba fupi kwenye semina ndogo iliyoandaliwa kwa lengo la kuwanoa Wamishionari kabla ya kuja Barani Africa na kati ya Mbinu waliyoitumia kuliteka Bara la Africa ilikuwa ni ASSIMILATION(Kuwafundisha Waafrica Lugha na utamaduni wa Kizungu)

Assimilation imegawanyika katika tanzu mbalimbali ikiwemo KI-DINI,-UCHUMI, -SIASA na -JAMII Hivyo wakaona ni vyema Kuanza na KIDINI( Religious Assimilation) kwa sababu ndio ingekuwa rahisi kuwarubuni waafrica na pia ingesaidia kuanzisha Mifumo hii mingine kiurahisi.

Baadhi ya mambo aliyowaeleza ni kama yafuatayo;

1. Aliwaambia wamishionari wasiwafundishe waafrica mambo ambayo tayari wanayajua kwa mfano imani kwa wakati huo tayari africa ilikuwa ina imani na walikuwa wanaabudu miungu ambayo sehemu kama Congo MUNGU alikuwa anajulikana kwa majina kadhaa wa kadhaa ikiwemo MUNDI, MUNGU(kama tunavyomuita ata sasa) na DIAKOMBA

Hivyo miongoni mwa majukumu waliyopewa hawa wamishionari ambao walikuja kama viongozi wa dini yaani PRIESTS ni kuhakikisha wanatimiza jukumu la kiutawala walilokabidhiwa toka Nchini kwao Ubelgiji.

2. Wamishionari walipewa jukumu la kuitafsiri injili kwa waafrica kwa minajiri ya kulinda na kufanikisha Malengo yao katika Bara la Africa.

3. Jukumu lingine lilikuwa kuhakikisha Waafrica wanapoteza hamasa juu ya Ardhi yao iliyojaa UTAJIRI mkubwa na yenye rutuba kwa maana bila kufanya hivo Waafrica wasingekubali kuona Wazungu wakichukua Mali zao hivyo wangepigana.

Kwahiyo kwa kuwapumbaza ilibidi wawadanganye waafrica kupitia vifungu kadhaa vya kwenye Biblia vitakavyowapa hofu

Ukisoma Mathayo 5: 3-12 utaona ni kwa namna gani wamishionari walihakikisha wanatumia elimu yao juu ya injili kuwawezesha kuwaambia waafrica kwamba ili kuurithi ufalme wa MUNGU lazima mtu uwe na Unyenyekevu n.k

Soma: (Mathayo 5:3)
"Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.."

Na wakaenda mbali zaidi kwamba ni ngumu sana kwa MATAJIRI kuurithi UFALME wa MUNGU hivyo waafrica wengi wakawa waoga kutumia Rasirimali zao kwa kuogopa kutajirika na kwenda motoni.

4. Wamishionari walikuwa na jukumu la kuhakikisha hawawapi nafasi Waafrica Kuhoji( CRITICAL THINKING) yale yote
wanayoambiwa kupitia mafundisho ya kidini wanayopewa. Hivyo walikuwa wanafundishwa KUAMINI na sio KUHOJI

Soma: (Yohana 20:29)
"Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.."
(AMINI ata kama HUJAONA)

5. Mfalme Leopord II aliwaambia wahakikishe wake zao( wanawake wa kiafrica) wanawaamini na kuwanyenyekea kwa kuwaletea zawadi mbalimbali kama Mbuzi, kuku au Mayai kama ishara ya shukrani( GESTURE OF GRATITUDE) kila wakati wanapotembelea vijijini kwao(..na jambo hili linaendelea hadi leo..loh). Kwa kifupi waliambiwa wahakikishw waafrica hawatajiriki kwa sababu wakiruhusu watajirike hawawezi kuwa WANYENYEKEVU

6. Waliambiwa wahakikishe Waafrica wanalipa KODI kila wiki siku za makusanyiko ya JUMAPILI(..yaani Siku ya kusali ile sadaka ndio kodi..Mmmh hatari!!)

Kisha tumieni Fedha hizo kujenga Hospitali, Mashule na Makanisa kwa ajili yao ili waone tunawapenda na kuwa jali sana waendelee kupumbazika..Sisi Hao..Balaa!!!

Kisha anzisheni mfumo wa Kutubia ( CONFESSION SYSTEM) utakaowawezesha kuchunguza na kujua kama mbinu zenu mlizozitumia zinafanya kazi kwa sababu watakuwa wakikosea wanakuja kutubu(..wakienda kinyume na mafundisho ya kwenye Kitabu cha Mathayo 5: 3-12)

Baada ya wamishionari kufika Africa sana sana Kongo, Aliyekuwa kiongozi wa Makoloni ya Ubelgiji Bw. Jules Renquin mnamo mwaka 1920 aliongezea nyama nyama kwenye kile kilichokwisha semwa na King Leopold II hapo awali na kusema mambo yafuatayo:

Waafrica waambiwe kuabudu sanamu ni kumuabudu shetani hivyo inabidi waache kufanya hivo kisha wamishionari waliambiwa wachukue masanamu hayo wayapeleke kwenye majumba yao ya makumbuko(Museum) lengo kubwa likiwa kuhakikisha waafrica wanawasahau mababu(Ancestors) na utamaduni wao.

Kuwachukulia waafrica wote kama watoto wao wa kufikia..hivyo kuwafundisha wawaite FATHER(Baba)..Mfumo huu nadhani unaendelea mpaka leo Wakatoliki wanamuita kiongozi wao wa kiroho FATHER na wakristo wengine wanamuita kiongozi wao wa kiroho BABA MCHUNGAJI

Wafundisheni Mafundisho lakini nyie msiyafuate hayo mafundisho kwa sababu ni ya uongo na endapo wakiwaliza kwanini nyie hamyatendi na kuyafuata yale yote mnayoyahubiri na kuyanena muwajibu " Mnapaswa kufuata kile ninachokisema na sio kile ninachokitenda"(kauli hii inatumika sana kwa wakatoliki na wakristo wengi mpaka sasa) kwani "Heri ya wale wanaosadiki bila kuona" kama isemavyo biblia.

Maneno ya King Leopold II na Bw. Jules Renquin yamekuwa yakifuatwa kila siku na ikawa ni utamaduni kwa wanawake wa kikongo wakati huo.

Ukisoma kitabu cha ABO UNE FEMME DU CONGO (A woman of Kongo) kilichoandikwa na Ludo Martens kilichochapishwa mwaka 1995 utaona ni kwa kiasi gani mwandishi amejaribu kuzungumzia suala hili kiundani kwa mfano katika ukurasa wa 68 amezungumzia mambo kadhaa yanayoendana na haya tuliyokwisha jadili hapo awali. Alienda mbali na kusema mambo yafuatayo..

Mababu zetu walikuwa wakijitegemea na walikuwa huru kwenye nchi yao lakini wakoloni walipokuja kwa lengo la kuwatawala kijiji baada ya kijiji, waliwaletea babu zetu chumvi na samaki waliokaushwa ili kuwarubuni washirikiane nao ila walikataa. Baada ya kukataa ilibidi watumie silaha za moto(Bunduki) na kwa Muafrica yeyote alieendelea kukataa kwa aliyekutwa na Upinde au Mshale mkononi alipigwa risasi papo hapo kisha wakawalazimisha babu zetu kuwafanyia kazi ngumu na wale walioonekana ni wavivu wakawa wanauawa.

Kisha wakatuletea Wamishionari (Tuwekane sawa kidogo hapa neno Missionary limetokana na Mission-ary ikiwa na maana walikuja na Mission yao) wakiwa na lengo(Mission) la kuwarubuni waafrica ili wawafanyie kazi kwa kujitolea kiroho safi (Ndio maana wakaja na ile mbinu ya Assimilation)

Waliwachukua watoto wadogo kutoka kwa mama zao na kuwafundisha dini kwa kisingizio eti ni Yatima hivyo watoto wamekuwa wakifundishwa dini na kukua wakijua ni Yatima hivyo kuwanyenyekea wao. Hivyo mdogo mdogo wakawa wakiisambaza dini yao baina yetu.. Hii inamanisha nini!?

Wao wamekuwa wakitukataza tusipende Pesa ila tumpende M/MUNGU aliye hai kuliko pesa lakini Wao Je! Hawapendi pesa!? Kampuni zao ikiwemo The Oil Mills of Belgium Congo inaingiza mamilioni ya pesa kupitia jasho letu. Je! Kutopenda pesa ni kuukubali Utumwa kwa kupewa ujira mdogo wakati wao wananufaika zaidi!!?

Walitukataza TUSIUE(Kutoka 20:13), Je! Wao hawaui!!?.. Hapa kilamba Mwaka 1931 waliuwa zaidi ya wanakijiji 1000.

Walitukataza TUSIIBE(Kutoka 20:15), Lakini wao wameiba ardhi yetu yenye rutuba, utajiri wetu na rasilimali zetu nyingi lakini Mtu mweusi alikuwa akiiba lazima aende KUTUBU na kumwambia kila kitu Mchungaji(Priest) kisha baada ya hapo mchungaji anapeleka taarifa kwenye Uongozi wao na yule mtu anakamatwa na kuwekwa Gerezani.

Sasa leo, Unaanzaje kuwa Mkatoliki au Mkristo!?

Unawezaje kuabudu dini ya watu wale waliokutesa!?

Unawezaje kuabudu dini ya watu walio-tesa,-dhurumu,-nyanyasa,-dharirisha,-ua babu zako!?

Wakatoliki na Wakristo wote ambao ni Waafrica wote ni WASALITI kwa mababu zao walioteswa, nyanyaswa,dhurumiwa,na kuuawa na wakoloni hawa.

Ni bora ata waafrica wenzangu waabudu zingine kuliko hii ya hawa waliotunyanyasa zaidi

Unaweza kuwa mkimbagu, mbuddha, muislamu na ata kuwa muumini wa dhehebu lingine lakini sio la hawa Wakristo kwa sababu kufanya hivo ni sawa na kuwatukana Babu zetu..

Hadi leo hii tunaona kuna viongozi wakubwa wa dini hizi ambao ni Waafrica wenzetu..hii inamaanisha nini!?

Waafrica bado tunatawaliwa na tutaendelea kuwa watumwa wa kifikra kutokana na huu Ukoloni mambo leo ulioletwa na watesi wetu.

Je! wakati makanisa ya Catholic, Protestant, Adventist, Baptist na mengineyo yaanzishwa na hawa wazungu kulikuwa ata na muafrica mmoja kati yao!!? Bila shaka jibu ni HAPANA!!

Angalia leo sasa, Sio Ghana, Kongo, Angola, Cameroon na sehemu zingine zote waafrica wanaabudu dini hizi kwa maelfu na maelfu yao huku wakitumia Biblia Takatifu kama kitabu cha marejeo lakini wamesahau hii hii Biblia ndio ilikuwa ikitumika kama kitabu cha marejeo na sheria zilizotumika kuwapumbaza Babu zetu na kusahau imani zao za asili walizowakuta nazo.

Itaendelea!!
(Ghost..)
Mkuu naona kwa asilimia kubwa unajipotosha mwenyewe! Inaonekana hujui historia ya Afrika na mwafirika mwenyewe
Unajiamianisha kuwa Dini zimeletwa na wazungu Afrika
Kwa taarifa karne ya tisa kulikuwa na himaya za Ukirsto Afrika
Nchi kama Sudan,Misri zilikuwa Himaya ya Ukirsto,jamii nyingi zilikuwa zinafanya ibada na walimwita Mungu kwa majina ya kwao
Afrika ilishastarabika kabla ya wakoloni...nenda kasome mji wa Kilwa ulikuwa na wakazi elfu nne na walifanya ibada...Timbuktu etc
 
Weeeee!!!! Rudi darasani.
Hizo himaya ulizosema Misri,Nubia(sudan) ,Algeria ,Libya(Cyrenaica) hizi zilipata ukristo mapema kwa maana zilkuwa part of Roman Empire kwahyo kunawahubiri walohubiri injiri huko ila Mwanzo watu wa maeneo hayo walikuwa na Miungu/Dini yao Asilia.
Ethiopia napo kulkuwa na dini zao za asili mpaka pale Ukristo ulipoletwa na Framentius.
Ikumbukwe kuwa hao watu waliopo leo hii huko Africa Kaskazini ni wahamiaji tuuu. Watu asilia pale walkuwa weusi
 
Duh leo umetoa mpya chief...Utawala wa Roma ilikuwa utawala wa kipagani
 
Umenifanya nifikirie kuhusu hizi Jumuia zilivyofanywa Saccos za mapadre. Yaani zimejaa michango ya kuwanyonya waumini utafikiri huko mbinguni kuna Benki.
 
Weeeee!!!! Rudi darasani.
Hizo himaya ulizosema Misri,Nubia(sudan) ,Algeria ,Libya(Cyrenaica) hizi zilipata ukristo mapema kwa maana zilkuwa part of Roman Empire kwahyo kunawahubiri walohubiri injiri huko ila Mwanzo watu wa maeneo hayo walikuwa na Miungu/Dini yao Asilia.
Ethiopia napo kulkuwa na dini zao za asili mpaka pale Ukristo ulipoletwa na Framentius.
Ikumbukwe kuwa hao watu waliopo leo hii huko Africa Kaskazini ni wahamiaji tuuu. Watu asilia pale walkuwa weusi
Kaka ukipenda lugha kama "rudi darasani" heri utagulie kidogo mwenyewe...
Sudan kamwe haikuwa sehemu ya Dola la Roma. Kuita wakazi wote wa Afrika ya kaskazini "wahamiaji tu" - pia si uthibitisho kwamba ulikuwa macho wakati wa darasa. habari za Waberber umesikia? Bado???
Bila shaka kila sehemu ya Dunia kulikuwa na "dini asilia" - halafu? Inasema nini?? Uingereza, Skandinavia, Ujerumani, Urusi, wote walikuwa na dini zilizotangulia kwa namna fulani.

Menginevyo: ukidai watu wa asili katika Afrika ya Kaskazini walikuwa "weusi" - kumbe kivipi weusi walichelewa kufika Afrika Kusini ambako wenyeji wa kiasili (akina Wasani na Khoikhoi) si weusi kweli?
 
Nikweli Nubia haikuwa sehemu ya Roman Empire lakini kupitia Egypt ukristo ndo ulisambaa katika falme za nubia. Pia hao barbers kulingana na uingiliano wa ndoa na wagen ulipoteza asili yao. Na unaposema mtu mweusi hatumaanishi ngozi tuu! Tunaangalia genetic make up ya mtu, mfano hpa tanzania kuna makabila kama wanyaturu wa singida wengi ni weupe but still tunasema ni weusi kwakuwa ni waafrika. Hivyo hoja ya khoisan kutokuw na ngozi nyeus kama wabantu wengi si hoja.
Tukirudi kwenye hoja ya msingi,sijaona sehemu uliyokana kwamba waafrika wa maeneo hayo tajwa hawakuwa na dini zao za asili. Na hiyo ndo ilkuwa hoja ya msingi japo ulitaka kunikosoa na ukakosa pa kukosoa ukajikita kwenye waberber,khoisani na Sudani lakini hoja ya msingi ni ujio wa dini
 
Duh leo umetoa mpya chief...Utawala wa Roma ilikuwa utawala wa kipagani
Nikweli mwanzo walkuw na miungu yao!! Lakini kuanzia karne ya kwanza 1BK, ukristo ulienea ndani ya Roman Empire lakini wakristo walikuwa wanauwawa sana hasa wakati wa uongozi wa KAISARI NERO. Wakristo waliendelea kuuawa mpaka ilipofika mwaka 313BK ndipo KAISARI COSTANTINE akaurasmisha ukristo kuwa dini rasmi ya Roman Empire. Yeye ndo alkuwa mtawa wa kwanza kuukubali ukristo hapo ndo mauaji ya wakristo yakaisha ,maana sasa ukristo ulikubalika.
 
Duh leo umetoa mpya chief...Utawala wa Roma ilikuwa utawala wa kipagani
Hahaha!! Utachekwa sana historia hujieleza yenyewe tuu bila kutumia nguvu. Et Kwamba nitachekwa? Wewe ndo utachekwa. Roman Empire imetawala kabla ya ujio wa ukristo , hadi ujio wa ukristo pia Roman Empire ilkuwepo. Vp hukupitia Slavery Mode of Production under Roman Empire?
 
Wakoloni walikuja kutafuta resources kwa kuwa walizihitaji wakagundua ziko Africa wakatumia ushawishi wao na viongozi wa waafrica wakakubali kuwaalika na kuwaruhusu wawatawale. Kwanini sasa hao wakoloni watwishwe lawama zote? Tukubali waafrica tulibugi pamoja na hizo imani zetu zilizotupelekea kubugi kwa ridhaa yetu wenyewe kwa kuwa hatukuwa na akili ya kukataa. Sasa la kuwalaumu wakoloni ni kupoteza muda. Kama imani yao imewafanikisha namna hiyo mpaka kuonewa wivu na wazembe wasiojua kulinda mali zao labda ndio imani ya kweli na sisi imani yetu ni ya kutokufahamu kujilinda na kuingizwa kingi king'ombe ng'ombe. Hapa isisingiziwe imani hata kidogo. Tukubali hatukufanya vizuri halafu tuchukue watu wetu peleka kwenye nchi zilizoendelea wajifunze wameendelea vipi wake kuendeleza africa. Hivyo ndivyo walivyofanya wachina mpaka kufikia hapo walipo, superpower. Sio kwa kulialia na imani na dini. Kwanza naona hiyo imani walioileta ndio imetufikisha hata hapa tunaweza kuelewana japo kidogo kuliko utopolo wetu. Acha kulaumu wazungu, amka katafute namna ya kujenga nchi na bara lako. Acha utopolo
 
Hahaha!! Utachekwa sana historia hujieleza yenyewe tuu bila kutumia nguvu. Et Kwamba nitachekwa? Wewe ndo utachekwa. Roman Empire imetawala kabla ya ujio wa ukristo , hadi ujio wa ukristo pia Roman Empire ilkuwepo. Vp hukupitia Slavery Mode of Production under Roman Empire?
Hapo juu ulitoa mfano wa Roman Empire kama kielelezo cha Roma kueneza Ukirsto jambo ambalo halina ukweli wowote
Nimekujibu kuwa himaya hii ilikuwa ya kipagani kuanzia Mwasisi wake Romus na kaka yake
Nilieleza kulikuwa na Himaya za Ukirsto Afrika hata kabla ya wakoloni...
 
Duuh! Ngoja nikuache
 
Nimekwambia kuwa hayo maeneo ya kaskazini mwa afrika yalipata ukristo mapema kwa sababu yalikuw ndani ya Roman Empire. Sio kwamba Roman Empire ilieneza bali iliurasimisha ukristo na ukakuwa zaidi ndani ya mipaka yake ambapo na maeneo ya afrika hayo yalikuwepo. Mbona hapo juu nimeeleza vizur tuu
 
Nikweli Nubia haikuwa sehemu ya Roman Empire lakini kupitia Egypt ukristo ndo ulisambaa katika falme za nubia. Pia hao barbers kulingana na uingiliano wa ndoa na wagen ulipoteza asili yao. Na unaposema mtu mweusi hatumaanishi ngozi tuu! Tunaangalia genetic make up ya mtu, mfano hpa tanzania kuna makabila kama wanyaturu wa singida wengi ni weupe but still tunasema ni weusi kwakuwa ni waafrika. Hivyo hoja ya khoisan kutokuw na ngozi nyeus kama wabantu wengi si hoja.
Tukirudi kwenye hoja ya msingi,sijaona sehemu uliyokana kwamba waafrika wa maeneo hayo tajwa hawakuwa na dini zao za asili. Na hiyo ndo ilkuwa hoja ya msingi japo ulitaka kunikosoa na ukakosa pa kukosoa ukajikita kwenye waberber,khoisani na Sudani lakini hoja ya msingi ni ujio wa dini
Ukitaja habari ya jenetiki kuhusu Wasan na Khoikhoi, basi walikuwa tofauti na watu wengine wa Afrika kabla ya uhamisho wa kutoka Afrika kuelekea kaskazini< kwa hiyo Wazungu ni Waafrika kushinda Khoisan. Au una data tofauti?
 
Back
Top Bottom