hii kuna mdosi alijitoa itv akasema anapiga mall ya nguvu na blue print akazionyesha, kitu matata sana ! Zaidi ya miaka miwili hivi, muhindi mwenyewe ni kama africarrier hivi, mdosi wa hapa hapa !Hivi nayo hii ilikuwaje?
Aiseee acha kabisa kunikumbusha bakulutu la pale . Roho inauma saana
Wakuu kuna mtu ana news yoyote kuhusu nini kinaendelea kuhusu hii hoteli ?
Miaka ile 1995 mpaka hata 1999 inanikumbusha matukio fulani humo ndani miaka ile. bucho nakwambia mafisadi wameiweka hotel 77 mifukoni mwao.
Wanajamii ni muda sasa karibu miaka 5 hotel hii imebinafsishwa lakini hakuna ujenzi unaendelea ni kitu gani kinazuia ujenzi kuendelea ? Kama mwekezaji ameshindwa kuiendeleza si anyang'anywe apewe mwekezaji mwinine , hii hotel ni muhimu sana kwa uchumi wa mkoa wa Arusha . Kama kuna mtu anajua kinachoendelea atujuze.