70% ya Watanzania wanafata Upepo - JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

70% ya Watanzania wanafata Upepo - JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GAMBLER, Dec 9, 2009.

 1. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Juzi Bwana mkubwa aliporudi ziarani, aliongea uwanjani na waandishi akasema kuwa,haiwezekani kwake kupendwa na watu wote, kwa sababu watu wanatofaotiana kimtazamo, asilimia 15 ya watu wanaweza kumpenda, asilimia 15 watamchukia hata afanye mema, na asilimia 70 wanafata upepo!! Wadau kuhusu hii asilimia 70 ya wa tz kufata upepo haijanikalia sawa, kwa kweli inatoa picha mbaya, inaonyesha kuwa asilimia 70 ya Wa tz ni mambumbumbu??? Great thinkers nakuombeni mtoe mchango wenu kuhusu hii asilimia 70 !!
   
 2. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 8,907
  Likes Received: 3,576
  Trophy Points: 280
  akiwemo yeye mwenyewe
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,460
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Gambler,
  Umenikuna kichwa. Sijui yeye yuko kundi gani.
   
 4. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,688
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mkifuata Bell Curve, JK yupo karibu na ukweli ki takwimu.
   
 5. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,712
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Sasa mnataka tutoe maoni kutoka mtu aliyekubali kuwa ametoka kupimwa akili? Anyway, labda atueleze takwimu hizo alitoa wapi REDET?
   
 6. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,688
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145

  Kupimwa akili sio kuonyesha kuwa mtu ana matatizo ya akili. Hizi stigma ndizo zinazofanya watu wasime afya zao.

  Kama zipo points dondokeni ama sivyo mtaonekana kuwa mna matatizo ya akili na hamtaki kwenda kupimwa.
   
 7. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,242
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  He was too polite:
  Wanaomchukia 1%
  Wanaompenda/na kufuata upepo 99%

  Unahitaji Vigezo?
   
 8. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 7,596
  Likes Received: 3,894
  Trophy Points: 280
  tatizo kubwa la Africa (Tanzania), viongozi wetu wanaonekana kama ni miungu, ni watu ambao hawezi kuumwa na ndio maana hata raisi JK akianguka tunaambiwa ni uchovu tu, sasa hiyo picha tunayopewa na watu wa usalama ndio inatufanya tuwe na maswali pale raisi wetu anapokwenda hospitalini kupimwa chochote, kwa hiyo hiyo sio stigma ni wao wenyewe ndio waliotujenga hivyo

  kuhusu hilo la 70% mambumbumbu mimi naona ni kweli kabisa kwa maana mbili mbili

  1 mpaka sasa sisi hatujajua ripoti ya raisi kuhusu akili zake, kwa hiyo inawezekana anaamuaga mambo kwa akili yake ya ugonjwa na asilimia kubwa inamfuata hivyo anatugroup sisi kama yeye

  2 anashangaa haya mambo yote ya RICHMOND, IPTL, DOWANS, BUZWAGI, ZOMBE na mengineyo, serikali yake haijachukua hatua yoyote na WATANZANIA tupo happy tu wala hatuwezi kuitingisha serikali kwa lolote basi ni lazima tutakuwa mambumbumbu tu
   
 9. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,688
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Niambie alipimwa akili au alipimwa viungo vya kibaiolojia vya fahamu? Maana naona wengi mnaviweka pamoja wakati ni vitu viwili tofauti.

  Matokeo ya vipimo vya mgonjwa wowote ni private matter. Lakini kwa nyinyi mliozoea kupanga foleni kuangalia matokeo ya kidato cha pili, nne na sita yakitolewa hadharani sishangahi kuona mkidai matokeo ya uchunguzi wa afya ya rais.

  Kuhusu Richmond, ........ Mmehamua kuendesha nchi kikatiba na kisheria. Kazi za bunge, vyombo vya usalama na sheria viko wapi? Jengeni taasisi na msitegemee rais afanye kila kitu.
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,125
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  To me, hili si la kujiuliza! Ni ukweli usiopingika kwamba watanzania tena hata zaidi ya asilimia sabini wanafuata upepo tu. Mara ngapi tumepiga kelele oooh CCM hii CCM hii, at the end of the day tunaipa kura asilimia 1000? huoni kama ni umbumbu huo? JK yupo sahihi zaidi ya kuwa sahihi. Na ukitaka kujua ukweli kwamba yupo sahihi kiasi gani, subiri 2010. Wananchi kule kijijini sasa hivi ukiwaona wanapiga kelele kupita maelezo, serikali hii imetutelekeza, lakini wakati wa uchaguzi hata wale wa Loliondo waliochomewa nyumba, watampa JK kura asilimia 100. Sasa huo sio umbumbu? Nampa heko JK kwa kujaribu kuwa mkweli. Ni juu yetu kujiangalia tupo upande gani.
   
 11. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 680
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni kweli watanzania ni mambumbu hajakosea kitu JK, wewe hushangai watanzania wanavyo mfagilia Nyerere wakati ndio kiongozi aliliua taifa hili.Kafariki hadi leo tunaendelea kuzongwa na mizimu yake ikiwemo miungano, ujamaa uliobaki baki kwenye serekali n.k....na watz hawasikii hawaoni kwa mwalimuuu.....

  Sasa kakosea nini hapo JK, huo ndio ukweli kabisa:)
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Dec 9, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 9,806
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Yuko sahihi, cha muhimu ni kujiuliza binafsi uko kundi gani? kama uko kwenye kundi la upepo , je mwakani utampa kura wakati ameshakufumbua macho????
   
 13. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli kabisa inasikitisha na kuhuzunisha, mtu unaacha kazi yako inayokupa rizki, unaamka alfajiri, unapanga foleni ndefu, kwenda kumpigia kura bwana mkubwa, what next??? kumbe ni mfata upepo!!! ...sijui watu watazinduka lini...kazi kweli kweli
   
 14. G

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 8,736
  Likes Received: 1,767
  Trophy Points: 280
  ndo maana yake anajua hata uwike vp! urais anao we unadhani kwann anawakingia kifua wakina EL na RA? huwezi mfanya kitu!
   
 15. G

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #15
  Dec 9, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 8,736
  Likes Received: 1,767
  Trophy Points: 280
  ukiacha majimbo yaliyo chini ya Upinzani mengineyo yote wapigaji kura wake wanafuata upepo! Mwana wa Kikwere anakuambia utake usitake!
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Dec 9, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,809
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kwamba wabongo wengi ni mrengo wa kati!!! sasa kama ndio kufuata upepo basi sawa

  tatizo letu waswahili, unweza kusema kitu cha kawaida lakini mtu akabadili maneno ilimradi tu kuleta drama!!!

  Kuwa neutral haina maana kufuata upepo, i would rather say ni kwamba tunasubiri upepo hatuufuati
   
 17. tovuti

  tovuti Senior Member

  #17
  Dec 9, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani hii kauli hata mimi imenisikitisha sana, hivi lini sisi tutazinduka????
  please say noooooooooooooooooooooo to ccm 2010
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Dec 9, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,809
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Mkuu, kuna mengi ya kuiangali CCM kwa jicho la tatu... hata la kumi!!! Ila kwa hii kauli nadhani tunatafuta cha kusema tu, si dhani kama alikuwa na lengo la ku-insult

  Tuwe makini na waandishi uchwara
   
 19. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #19
  Dec 9, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Labda ni katika hiyo asilimia 70 aliyoisema ....
   
 20. tovuti

  tovuti Senior Member

  #20
  Dec 9, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahahaha... Ilongo hapo umeniacha hoi
   
Loading...