69 Records-Tamthiliya ya kipekee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

69 Records-Tamthiliya ya kipekee

Discussion in 'Entertainment' started by Raia Fulani, Feb 25, 2011.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kusikia kitu kikisifiwa na kulandana na sifa hizo, si kingine bali ni hii tamthiliya changa. Nimeisikia ikitangazwa kwenye clouds media na kupewa sifa. Nilidhani ni majigambo yao ya kila siku ila nilikubali pale nilipoiona japo episode moja. Rangi, maudhui, wahusika, kuuvaa uhusika, etc ni bora kabisa. Baadae nikajiuliza, kwa nini filamu zetu japo hazina vitendo (actions) mbona hazina ubora huu? Nashawishika kusema kuwa Clouds media wapo juu katika tasnia ya burudani. Mpo juu. Ruge Mutahaba-Mkurugrnzi wa utafiti na maendeleo (R& D) pia upo juu kaka. Cheki pia na hapa

  Changamoto iliyo mbele yetu kama watanzania ni kuhakikisha tamthiliya zinakuwa ni mtiririko wa kila siku na wala si mara moja kwa wiki. hii inapunguza mtiririko wa simulizi na utamu wake. Tunaona za wenzetu toka Venezuela, Italia, Brazil, Ufilipino, SA, n.k. Ni ndefu na za kila siku. Isidingo pekee ina umri wa mtu timamu-zaidi ya miaka 10 sasa! Na inaonyeshwa kila siku na wala haipotezi utamu.

  Upande wa kutafuta washiriki wa tamthiliya hilo limewezekana. Bado upande wa kutafuta watunzi wa simulizi nzuri na ndefu. Hii ni changamoto kwa tasnia nzima ya filamu, maigizo na tamthiliya.
   
Loading...