50 Uhuru - Vikwazo vya uchumi Ludewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

50 Uhuru - Vikwazo vya uchumi Ludewa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Oct 28, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Gari la mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe
  likipita daraja la Ulayasi (Mlangali) barabara kuu iendayo Ludewa toka Njombe


  Historia inaonesha tatizo kubwa la wananchi wa Ludewa ni
  miundombinu, mawasiliano na nishati.

  Licha ya uwepo wa fulsa mbalimbali za kiuchumi haya yamekuwa matatizo sugu katika wilaya ya Ludewa
  kitu kilichopelekea fulsa hizo kutofanyiwa kazi mfano wa fulsa hizo ni kilimo, ufugaji, uvuvi, vivutio vya utalii vya milima ya livingstone na misitu ya asili ya Milo,Madini maeneo ya amani, Mgodi wa chuma cha Liganga na makaa ya mawe ya mchuchuma maporomoko ya mito mfano mnyereri. Mabaki ya vitu vya kale kwakibaba [utilili] na tamaduni za watu wa Ludewa mfano ngoma ya mganda.Tangu kuwepo kwa mbunge Deogratias Filikunjombe baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2010 wananchi wa Ludewa mkoa mpya wa Njombe wana matarajio makubwa sana ambayo yametokana na mbunge huyo kuanza kutimiza ahadi mbalimbali wilayani Ludewa ambapo pia ni Jimbo la uchaguzi.


  Ametekeza ahadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwasomesha watoto mmbalimbali, kutoa michango katika kuendeleza michezo katika kata na shule mbalimbali, kugawa/kutoa magari ya kubebea wagonjwa katika hospitali mbalimbali lakini kubwa ni kuupa msukumo kutia saini mkataba wa ufuaji wa chuma cha liganga na makaa ya mawe ya mchuchuma.

  Tatizo la barabara kutoka Njombe hadi Manda kupitia Mlangali na Ludewa licha ya barabara hiyo kukarabatiwa mara kwa mara kwa kiwango cha changarawe imekuwa haipitiki katika kipindi chote cha mwaka.Wakati wa masika barabara imekuwa haipitiki.

  Tatizo la barabara limekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo kwani licha ya uwepo wa fulsa nyingi uwekezaji umeshindikana kabisa kutokana na kutofikika katika kipindi cha masika lakini hata wakulima wamekuwa wakishindwa kuuza mazao yao pia hata kuyasafirisha ni gharama kubwa kwani kusafirisha kutoka Ludewa hadi Njombe KM 130 ni sawa na kusafirisha kutoka Njombe mpaka Dar es salaam KM 800.

  Lakini pia huko kutofikika kumepelekea fulsa mbalimbali kama utalii kutofanyiwa kazi hivyo kuikosesha serikali mapato. Tatizo la mawasiliano lipo ila ni kiwango kidogo kwani sehemu mbambali makampuni ya simu yameweza kufikisha mawasiliano Barabara ya mkoa kutoka Njombe kuelekea Ludewa wilayani.

  Nishati ya umeme pia ni tatizo kwani hadi mwaka 2005 ni
  Ludewa mjini na Lugalawa tu palikuwa na umeme. Hali hii imebadilika baada ya Mheshimiwa Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005 ambapo waliongezewa majenereta hapo wilayani ambapo mpaka sasa kuna sehemu zenye umeme ni Madunda kwa msaada wa kanisa Katoliki.

  Tatizo lipo katika kata za Mlangali Lupanga Milo Masasi na mwambao mwa ziwa nyasa ambapo hakuna umeme hivyo uvuvi umekuwa hauna tija kwa taifa ambapo wavuvi wamekuwa wakifanya uvuvi kwa ajili ya kitoweo na kujikimu. Pia tatizo hili limepelekea watu washindwe kufungua viwanda vya kusindika matunda kwa sehemu ambazo matunda yanastawi [Ludewa milimani] kama Lusitu matokeo yake matunda yanaagizwa kutoka Afrika Kusini.

  Pia hata kufungua mashine kwa ajili ya kusaga nafaka imekuwa vigumu ambapo wananchi wa ludewa wangeuza unga na sio mahindi kama wafanyavyo sasa.

  Uwepo wa hospitali za madhehebu mbalimbali ya dini kama hospitali ya Lugalawa na hospitali ya milo pia Hospitali ya wilaya ya Ludewa na baadhi ya vituo vya afya kama mlangali na zahanati mbalimbali katika vijiji mbalimbali kwa kiwango Fulani kumewezesha watu wa Ludewa kupata huduma za afya lakini changamoto ni miundo mbinu mfano Kutoka Utilili mpaka hospitali ya Lugarawa zaidi ya 36km ni mbali sana pia barabara ni mbovu sana.

  Licha ya wilaya ya Ludewa kutoa watu waliotikisa nchikatika Nyanja za siasa na taaluma kama Hayati Horace Kolimba, Mchungaji Christopher Mtikila, hayati Dr. Crispin Mponda na Prof Raphael Mwalyosi wilaya ya ludewa haina muamko wa kisiasa pia haina muamko katika suala la elimu nah ii inatokana na kukosa expose na walioendelea kutorudi kwao kutoa msukumo wa mambo hayo. Jimbo la uchaguzi na wilaya la Ludewa ina mbunge wa CCM aliyepita bila kupingwa pia isipokuwa diwani mmoja tu ndio anatoka upinzani [TLP] hivyo hakuna changamoto za kutosha katika kuendesha halmashauri hiyo .

  Hadi mwaka 2004 kabla yakuanzisha kwa shule za kata wilaya ya Ludewa ilikuwa ina shule za sekondari 6 tu yaani Ulayasi, masimbwe,Madunda, Lugalawa, Ludewa na Manda tu.Na mpaka sasa wilaya hii haina chuo chochote cha taifa na ina shule moja tu inayotoa elimu ya kidato cha tano na sita ULAYASI tu.

  Changamoto hizi zimepelekea vijana wengi kukimbilia mjini kutafuta kile wengi wanachokiita kutafuta maisha lakini kwa miundombinu duni hata wananchi wa Ludewa wanaofanya kazi nje ya Ludewa wamekuwa wakikukataa kwamba sio kwao na wengine wamekuwa wakiishi mijini kwa miaka nenda rudi bila kurudi kwao. Lakini pia wafanyakazi ambao wamekuwa wakipangiwa kwenda Ludewa ama walimu ama madaktari na wengineo wamekuwa hawataki kwenda au wamekuwa wakiripoti na kurudi kwao kutokana na kuwepo kwa matatizo haya. Pia imani za kishirikina ambazo huendekezwa baadhi ya maeneo zimepelekea wataalamu hao kutopenda kwenda Ludewa.

  Endapo serikali itatimiza ahadi zake hasa kupitia kwa mbunge Deogratias Filikunjombe kwamba baada ya kusaini mkataba wa Liganga na Mchuchuma itaruhusu ujenzi wa barabara kutoka Ludewa kwenda Njombe kwa kiwango cha lami ni ishara njema kwa mustakabali wa maendeleo ya Ludewai.Pia ni jukumu la wananchi wa Ludewa kushirikiana na mbunge ili kufanikisha masuala haya kwa mustakabali wa Ludewa mkoa wa Njombe na Tanzania kwa ujumla.Mungu Ibariki Ludewa Mungu Ibariki Tanzania.

  Utafiti huu umefanywa na Stewart Frenk Njelekela.
  Mwanafunzi - Chuo kikuu huria Tanzania.Njelekela87@yahoo.com
   
Loading...