50 Cent, Ghetto Economics na Muziki wa Rap - 1

Gego Master

Member
Jul 19, 2021
5
45
50 CENT, GHETTO ECONOMICS NA MUZIKI WA RAP - 1

UTANGULIZI

Peace Family

Kwenye Kitabu nilichoandika cha “Uelewe Utamaduni wa Hip Hop” kuna sura inajulikana kama “Vita vya Kimashahiri mjini New York” na kati kati ya vita hiyo muhusika muhimu kabisa anajulikana kama Curtis Jackson au maarufu kama 50 Cent.

Akiwa na miaka 45 sasa, 50 Cent ni mtu mzima ambaye kila akiufikiria ujana wake anakumbuka kwamba anayo sababu maalumu ya kuendelea kuwepo duniani kwani Mungu alimleta afanye jambo fulani. 50 Cent ni mmoja wa Rappers maarufu duniani LAKINI kwangu mimi ananivutia sana na harakati zake zilizopelekea yeye kuwa maarufu kiasi hicho.

Andishi hili 50 Cent, Ghetto Economics na Muziki wa Rap ni maalumu kwako wewe mpenzi wa muziki wa Rap na ambaye unafuatilia utamaduni wa Hip Hop kuweza kumuelewa 50 Cent sio tu kupitia muziki wake bali kupitia harakati zake mbali mbali chanya anazozifanya.

Katika utamaduni mzima wa Hip Hop 50 Cent ni miongoni mwa Ma-Emcee/Rappers aliyeandika vitabu vingi kuliko wakongwe kadhaa. Kwangu mimi Emcee/Rapper ambaye anao uthubutu wa kuandika vitabu ni mtu muhimu sana kuliko Emcee/Rapper ambaye hana uthubutu huo. Kwangu mimi 50 Cent ni scholar muhimu katika utamaduni wa Hip Hop kuliko wakongwe wengi.

Mpaka sasa 50 cent ni mfano bora sana kwa yeyote anayetaka kujifunza juu ya Economics, Business Management, Leadership, Muziki wa Rap, Marketing na mengine mengi. Ni kweli unaweza kwenda shule na kufundishwa yote hayo LAKINI ukijifunza hayo yote kupitia maandishi ya 50 Cent na Muziki wake unayo nafasi kubwa sana ya kufanikiwa katika harakati zako. Hivyo andishi hili ni maalumu kukufungua juu ya hayo yote hapo juu.

FAMILIA

Sehemu kubwa ya malezi ya awali ya 50 Cent yalisimamiwa na Bibi yake Beulah Jackson ambaye alifariki 2014. Bibi huyo alikuwa na mapenzi mazito kwa mjukuu wake Curtis Jackson kuliko watoto wake na wajukuu wengine alioishi nao hapo South Jamaica mjini Queens.

Kilichopelekea 50 Cent aishi sana na Bibi yake ni kifo cha Mama yake mzazi aliyejulikana kama Sabrina. Mama huyu alifariki kwenye kifo ambacho kilikuwa ni cha kupangwa kwani Sabrina alikuwa ni muuzaji maarufu sana wa madawa ya kulevya.

Sabrina akiwa na miaka 15 alimzaa 50 Cent. It’s crazy. tunasema mtoto kazaa mtoto. Na miaka 8 baadae Sabrina akaaga dunia Hivyo 50 Cent alikuwa kampoteza mama akiwa na miaka 8 na huku akiwa hamjui baba yake ni nani na mwisho wa siku ndio maisha yote yakaishia kwa Bibi, Ingawa hata kabla ya kifo cha mama yake tayari 50 Cent alikuwa akiishi na Bibi kwani hustle za mama mtu zilikuwa na kashi kashi nyingi haikuwa salama kwake kukaa na mtoto.

Kipindi Mama yake 50 Cent akiwa hai, ilikuwa ni rahisi kwa 50 Cent kupata vitu vingi vizuri, nguo, viatu na chochote ambacho mtoto atakihitaji, mama mtu alimnunulia hata bike ya kutesa nayo kitaa. Baada ya mama kufariki kidogo mambo ikaanza kuwa ngumu na Bibi yake alikuwa na familia kubwa ambayo inamtegemea hivyo kuna vitu alikuwa anahitaji na Bibi hawezi kumnunulia.

50 Cent anakumbuka juu ya mahitaji yake ya sneaker za zaidi ya $100 kitu ambacho asingeweza kumwambia bibi yake amnunulie. Kuna kipindi washirika kadhaa wa kibiashara na marehemu mama yake walikuwa wakimcheki 50 Cent na kumpatia hizo sneaker anataka LAKINI baadae nao mambo yakawa magumu.

Kuna wajomba zake 50 Cent walikuwa ni watumiaji wa madawa ya kulevya, Hii familia ilikuwa na changamoto sana mama yake 50 Cent alikuwa muuzaji, hao wajomba walikuwa watumiaji, Bibi yake 50 Cent akisisitiza kumfanya mjukuu wake awe mtu wa kanisa kwani bibi kanisani alikuwa habanduki wakati huo huo babu yake 50 Cent hataki hata kulisikia kanisa baada ya kuchangisha hela huko kanisani na mchungaji mmoja akapita nazo hivi.

Kati kati ya hayo yote ndipo 50 Cent alilelewa, unaweza ukapata picha ya namna ambavyo ilibidi akuwe haraka sana na kuzipita stage kadhaa za kuwa mtoto ili aweze kupata mafanikio aliyonayo leo kwani mazingira ya hood hayakuwa nafuu hata kidogo.


GHETTO ECONOMICS

Ukisoma kitabu cha 50 Cent “from Pieces to weight” kunalo somo zuri juu ya concept ijulikanayo kama Ghetto Economics picha linaanza hivi;

“Motherfuckers would go to jail and come back talking pro- black and breaking down racism. Or they’d come back religious, quoting chapters and verses of the Koran or the Bible. One guy I knew even came back a Buddhist. Red came back an economics major.”

Kama hujapata nafasi ya kusoma katika mitaala maalumu ya shule na vyuo basi elimu ya mtaani inapatikana kwa kiasi kikubwa jela, kwenye mitaa tunayoishi, kupitia muziki wa Rap, na pia njia zitumikazo kuuza dawa za kulevya. 50 Cent baada ya mambo kuwa ngumu alijikuta akiingia katika biashara hiyo ya uuzaji dawa za kulevya.

Na hapo juu anamtaja mtu ajulikanaye kama Red ambaye alifungwa kwa issue za uuzaji wa dawa za kulevya na kisha kutoka akiwa ana uelewa mkubwa juu ya Economics ya mtaani na alikuwa akimpa somo 50 Cent. Ndio hapo juu anaeleza kwamba kutokana na somo alilokuwa anapewa na Red alimuona kama kasoma Economics major.

LAKINI sio Red aliyemuingiza 50 Cent kwenye biashara hiyo. Wale wajomba zake 50 Cent kuna kipindi walikuwa wakimtuma kwenda kuwanunulia dawa hizo mtaani, Lakini pia mmoja wa mjomba wake ajulikanaye kama Trevor alikuwa muuzaji wa madawa hayo. Trevor alikuwa akifanya vikao vyake na washirika wake wa madawa hayo nyumbani kwao ambapo 50 Cent anaishi yaani kwa bibi yake 50 Cent.

Baadae Trevor alikuja kufungwa lakini kabla hajafungwa kuna mdau anaitwa Sincere ambaye Trevor alimuunganisha na wauzaji wakubwa wa madawa 50 Cent anamtaja mtu ajulikanaye kama Carlos kama mshirika huyo. Pia 50 cent anamzungumzia Uncle wake mwingine ajulikanaye kama Harlord. Hao wote aliowataja 50 Cent kwenye kitabu chake cha ‘From Pieces to Weight” ndio alikuwa watu anaowaona mtaani, wakiwa na fedha nyingi zilizotokana na uuzaji wa madawa hayo. Ni family member, ni majirani. Kwa namna moja au nyingine hiyo ilipelekea kwake kuona hamna namna nyingine rahisi ya kupata hela kama sio kuuza dawa za kulevya.

Akimuelezea Sincere 50 Cent anasema;

“Sincere was one of the new breed. His aunt lived next door to my grandmother’s house and his grandfather lived two blocks away. He was practically family. Sometimes he’d see me in the street doing nothing. My sneakers would be torn; my clothes dirty; and my skin ashy. He’d pop open the door to his BMW and, just like that, he’d take me shopping. And not just around the corner but down to Jamaica Avenue to the mall, to Pop’s, where he’d get me Fila sweatsuits and all sorts of sneakers: Ellesses, Lottos, Adidas, Nikes. When it was cooler outside, he got me a Starter jacket”

50 Cent anamtaja Cousin yake mmoja ambaye kwa kipindi kile alikuwa kwenye umri wa kuwa shule LAKINI wapi, alikuwa mtaani ana-hussle, Cousin huyo anaitwa Brian. Anaendesha gari kali na anauza unga tu. 50 Cent alipomuomba amsaidie kupata sneaker mpya Brian aliishia kumcheka tu na hapo ndipo akawa kila akitaka kitu msaada ni kwa Sincere tu.

LAKINI 50 Cent anasema;

”But the time came when Sincere wouldn’t buy clothes or sneakers for me, either. Sincere began to change. Mel and Jack, some of the older guys from the neighborhood, had kidnapped his grandfather for ransom money.”

Yes kitu kama hicho kilitokea pia kwa Brian kwani hao wadau Mel na Jack walimvamia pia Brian ili wamuibie fedha zake na katika purukushani hiyo walimpiga risasi mama yake Brian. Sababu ya matukio yote hayo ni kwamba vijana waliokuwa wanasaidiwa kama alivyo 50 Cent walikuwa na mdomo mrefu wa kuonge aongea mtaa na matokeo yake chuki ikaanza na washikaji wakaanza kukaba na kuwadai pesa wauzaji wa madawa kama Brian na Sincere. Hivyo 50 Cent hapa alipewa somo la kwanza juu ya Ghetto Economics na Sincere ya kwamba;

” it was better to stay quiet about what you were getting and how much of it you were keeping around the house.”

Baada ya somo hilo la kwanza juu ya Ghetto Economics 50 Cent anaendelea kusema ya kwamba Sincere alimwambia;

“Listen, if I give you a pair of sneakers, they’re just gonna get dirty and I’ma have to buy you a new pair all over again, man,” Sincere said. Then he pulled out a small wrapped bag of cocaine and told me that it contained a little bit over a gram of powder. He measured out the bag into five equal parts and wrapped them in foil. “There’s five Alberts, man,” he said. “Sell those to your uncles and bring me back a hundred dollars.”

Na kama hivyo basi 50 cent akaingia rasmi kwenye biashara ya uuzaji wa madawa ya kulevya, kila uncle zake wakimtuma akawaletee unga yeye anazuga kama anaenda kuzurua huko nje kununua unga kumbe anao ndani kauficha anakuja na kuwapa. Mpunga wote anasave home na huku akikaa kimya bila kumwambia mtu kitu.


Itaendelea


Gego Master,

Hip Hop Philosopher, Scientist Emcee

G.E.G.O Master
 

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
2,866
2,000
Jamaica Queens, South East Queens na maeneo ya jirani ambayo 50 alikulia yalikua maeneo ya hatari sana.

Miaka ya ukuaji wa 50 hayo maeneo ndio biashara ya crack cocaine ilikua imeshika kasi, wazungu wanasema ilitoka bad to worst, mauaji, utekai ilikua ni nje nje mchana kweupe kwa magenge ya mauza madawa ya kulevya.

Angalia hii documentary utaelewa.
 

ze-dudu

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
14,761
2,000
50 cent aliibuka kwenye zamu zangu za ukuaji aiseee mpaka leo mwamba yupo moyoni......album ya kwanza niliinunua kwenye casette kwa shilingi 1200....pale kariakoo enzi ya mkapa hii pesa niliisotea mwezi mzima maana nilikua nasoma
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom