3G Network Yaingia Tarime. Oyeeeee!!!

3G Network Yaingia Tarime. Oyeeeee!!!

SuperImpressor

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
1,505
Reaction score
649
Nawapongeza sana Tritel (T) Ltd kwa kuwajali watu wa Tarime kwa kuwaletea mtandao wa kasi. Sikuamini macho yangu kwa sababu nilijua
Voda ndio wangelianzisha na sasa hivi naEnjoy Speed yake.
 
Nawapongeza sana Tritel (T) Ltd kwa kuwajali watu wa Tarime kwa kuwaletea mtandao wa kasi. Sikuamini macho yangu kwa sababu nilijua
Voda ndio wangelianzisha na sasa hivi naEnjoy Speed yake.

hongereni, inamaana muda wote ilikuwa ni edge? na hii tritel bado ipo kumbe mi nikajua ilikufaga miaka ileee
 
Nawapongeza sana Tritel (T) Ltd kwa kuwajali watu wa Tarime kwa kuwaletea mtandao wa kasi. Sikuamini macho yangu kwa sababu nilijua
Voda ndio wangelianzisha na sasa hivi naEnjoy Speed yake.
tRITEL si ilishakufa enzi ya mzee ruksa au mzimu wake bado unatembea?
 
hongereni, inamaana muda wote ilikuwa ni edge? na hii tritel bado ipo kumbe mi nikajua ilikufaga miaka ileee

Mkuu mda wote tulikuwa na Edge tu na kwa Zantel bado tuna Gprs labda tu iwe roamed kwa mitandandao mingine
 
Kweli wakurya watata.. Hadi leo Tritel bado ina exist huko... Kazi kweli kweli
 
hata mi hapa nipo Nzega nina android nikisearch networks naiona zote na TRITEL TZ
nikiichagua hyo inarun kwny chip ya Voda. na inakasi ya ajabu inapanda inakua H
nikichagua Voda inakua Edge
 
Hii kitu vocha zake bado sijaziona hata modem ila unachotakiwa kufanya kama una laini ya vodacom nenda kwenye network setting kisha angalia available networks au manual selection na hapo mitandao iliyopo hewani itakuja na hapo utaona mmojawapo ya hiyo umeandikwa Tritel(T) Ltd, select huo utaona kwenye home screen panasomeka hivi 3G 64001 Vodacom. Hapo kazi kwisha. NB. hakikisha simu ina UMTS/3G/HSDPA na kama haina hutaona kabisa kitu kama hicho.
 
hata mi hapa nipo Nzega nina android nikisearch networks naiona zote na TRITEL TZ
nikiichagua hyo inarun kwny chip ya Voda. na inakasi ya ajabu inapanda inakua H
nikichagua Voda inakua Edge

Yaani ni hivyo hivyo ulivyoeleza mkuu
 
Hiyo ni voda naona wanafunga mitambo ya 3g makao makuu ya wilaya karibu zote nimepita Ushirombo, Katoro, Geita, Sengerema,Magu, Bunda pote panasoma 3g ila inakuwa ni roaming sijui kwa nini.
 
Tritel imefufuka?

Mimi nipo Tanga na uki search kwenye simu ni kweli TRITEL inakuwepo kwenye available networks. Nashindwa kuelewa wenye taarifa na hili watujuze zaidi...
 
kweli huu mtandao upo? mbona sijawai kuona hata vocha zake huku dsm!
 
Back
Top Bottom