3d modelling and animation | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

3d modelling and animation

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by 3D., Sep 10, 2010.

 1. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuna mtu anaweza akaniambia Tanzania tumepiga hatua kiasi gani katika mambo ya 3D animation ikihusisha matangazo ya TV na Filamu?
   
 2. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Kuna kozi hapo chuo zamani kilikua kinaitwa Dar tech (nadhani kinaitwa D.I.T) wana fundisha somo la animation in 3D.
   
 3. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Thanks mtoto wa kishua kwa reply. Kitu kinachonishangaza ni kuwa sioni matumizi ya kutosha ya animation katika sinema zetu. Najua wasanii kama Kanumba huenda wangependa kuweka effects katika sinema zao, lakini inaonesha hakuna watu wa kufanya animation au wako wachache, kama wapo.
   
 4. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nataka kukukosoa rich.nzemya kwa kuchafua mada iliyotangulizwa hapa. Naona umeamua tu kubambikia swali lako katika topic hii bila kujali kuwa hii itaiua hii topic kwa wale ambao wangeweza kuichangia ipasavyo. Hii na maanisha kuwa, contributions mbili zilizofuata yako ni utumbo mtupu. Na hii namaanisha majimoto na Amoeba, jamani nini sasa mnafanya kuweka "comments" zisizo na maana hata kidogo. Sasa 3D aende wapi jamani kupata jibu ambalo limeenda shule kiasi?
  Jukwaa hili linasemekana kuwa ni forum ambayo angalau unaweza kupata discussions zenye kusaidia watu ki'mawazo, ki'elimu nk, jamani, tudumishe hili lengo na isiwe another forum ambayo mtu unakosa hamu kuitembelea kwani utapata topics being hijacked au watu ku'submit comments ambazo hazina msingi wowote. Kama kweli ulichukua muda wako ku-register hapa, tafadhali jumuisha jamii kwa mambo ya maana, sio tu kujaza article counts.

  Sasa narudisha topic kwa 3D

  Angalia software zifuatazo katika CG na 3D Animations na jinsi gani ya ku-combine na standard footage.

  Maxon Cinema 4D (commercial)
  blender 3D (free)
  NUKE (commercial)
  voodoo (free /ple)
  Autodesk Softimage (commercial)

  Na nyingine nyingi.

  Mimi hapa napenda kuifuatilia development ya blender 3D ambayo inaweza kutumika in animation pamoja na kutengeneza 3D assets for film. Katika kuifahamu, bado nipo beginner sana na ningependa kuwasiliana na watu wengine wenye nia ya kujifunza 3D hapa bongo. Ukipata muda, google blender 3D uone some developments ambazo watu wanatengeneza.
  Katika filamu za tanzania, kweli hata mimi ningependa angalau waanze kujaribu kutumia hii na kama ufahamu wake bado mdogo, wawape vijana nafasi za kujifunza na hapo labda miaka ya baadae, film industry inaweza kuwa na ufundi huu katika filamu zao.

  KK
   
 5. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hakuna kuaminiwa - tz ila kuna kujiamini na kubebwa!!! Wenye vipaji wapo vijiweni wana vuta bangi... Na hata hawajui mnayo ongea...na hata mkijua ..mnawaonea wivu au manataka wawe wana siasa...
   
 6. g.n.n

  g.n.n JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tuwe wapole jama tutoe comments za maana wakujifunza tupo wengi.
   
 7. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  true mkuu.
   
 8. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe kuwa miongoni mwa mambo yanayorudisha nyuma maendeleo ya waTz wengi nis uala hili la kubebana. Ukweli huu upo hata katika medani ya sanaa. Ila hata hivyo suala la wenye vipaji kuwa vijiweni na kuvuta bangi inategemeana sana na ufahamu wa mhusika mwenyewe. Kazi za sanaa kwa kiasi kikubwa hujionesha zenyewe na haihitajiki nguvu katika kuuleza uwezo wa msanii.. ni suala la kuonesha kazi zako.

  Tatizo lililopo ni baadhi yetu kusubiri serikali iweke mazingira mazuri ili tufaidike. Haiwezekani. Serikali iko bize na mambo mengine (ya maana na yasiyo ya maana). Serikali ikishindwa kutengeneza njia basi tengeneza mwenyewe. Kwa mfano kwa mazingira ya nchi yetu sijaona vyuo rasmi vinavyofundisha serious 3D (hata ambayo si serious sana)... sasa katika mazingira kama haya kwa sisi ambao hatuna uwezo wa kwenda kusoma nje ya nchi tufe masikini au tusomee uhasibu kwa kuwa hakuna vyuo? Ingekuwa udaktari sawa ni lazima usome sehemu lakini sanaa unaweza kujifunza mwenyewe na mambo yakaenda japo kwa kuhangaika.

  Ulimwengu wa 3D na Motion graphics hapa nchini kwetu kwa kiasi kikubwa unamilikiwa na Wahindi (sina tatizo nao katika hili) pamoja na Wakenya kwa wana opportunities kubwa ya vyuo etc kuliko sisi. Je, ukweli huu utufanye wanyonge katika nchi yetu wenyewe? Hapana. Nikumbushie usemi katika tangazo la redio la zamani (miaka ya tisini) la magari ya Mitsubishi Pajero:

  "Penye nia pana njia, pasipo na njia pana Pajero."
   
 9. HT

  HT JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  tuingie tuacheni uoga! Kama serikali haitaki kuweka mazingira sisi tuyatweke kwa nguvu!
   
 10. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 11. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  It's awesome what that piece of software can achieve. I believe in the future developers are going to make it more user-friendly.
   
 12. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2014
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mambo?
   
 13. snipa

  snipa JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2014
  Joined: Dec 10, 2013
  Messages: 4,159
  Likes Received: 191
  Trophy Points: 160
  poa....................................
   
 14. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2014
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hatua kwa hatua jiwe kwa jiwe tuna weza.... Limbe - Music - HulkShare
   
 15. Good Guy

  Good Guy JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2014
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 4,511
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  2D is more of my thing!!
   
Loading...