36 wajitokeza kuuza figo Hospitali ya Taifa Muhimbili

Super Handsome

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
3,846
6,439
Hospitali ya Taifa Muhimbili imetoa ripoti ya takwimu zinazoonesha kupokea maombi ya wananchi 36 walioomba utaratibu wa kuuza figo zao ili kukabiliana na ugumu wa maisha.

Takwimu hiyo imetolewa jana wakati wa maadhimisho ya siku ya kukabiliana na ugonjwa wa Figo duniani.

Awali, Ofisa Ustawi wa Jamii kutoka kitengo cha figo Muhimbili, Halid Mahenga alinukuliwa hivi karibuni akisema kuwa kati ya Januari hadi Februari, watu sita walikwenda hospitalini hapo wakiulizia utaratibu wa kuuza figo zao.

Aidha, Mahenga katika taarifa yake kwa umma, alisema kati ya mwaka 2019 na 2020 idara yake ilipokea maombi ya watu watatu waliohitaji kupewa utaratibu wa kuuza figo zao, huku mwaka 2021 wakipokea watu wengine 27 ambao baadhi yao wamedai chanzo kuwa ni ugumu wa maisha.

Hata hivyo, ameeleza kuwa wakati serikali ikiendelea kufanyia kazi maandalizi ya sheria ya upandikizaji wa viungo, hospitali hiyo kwa sasa inaendelea kuzingatia misingi yote ya maadili kitaaluma katika upandikizaji wa figo.

“Ni muhimu watu wakatambua kwamba ni makosa kisheria, mgonjwa akihitaji upandikizaji hospitali itazingatia kanuni zinazohitajika kwa mtu anayetakiwa kuchangia figo kwa mgonjwa mwenye uhusiano wa damu” Alisema Mahenga

Hospitali ya Muhimbili tayari imepandikiza figo kwa wagonjwa 68 tangu kuanza kwa huduma hiyo nchini mwaka 2017, huku wagonjwa 110 hadi 120 wakipewa huduma ya usafishaji figo kila siku hospitalini hapo

Chanzo: TanzaniaWeb
 
Katika moja ya vitu alivyofanya Jakaya ni kuandaa mazingira,misingi na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na matibabu ambazo tulikuwa zinapatika nchi za Asia na Ulaya hapo Hospitali ya Muhimbili. Tutakukumbuka Sana Mzee wetu.
 

India: Kifahamu kijiji cha wauza Figo ‘Kidney Village’ kilichopo nchini Nepal​




1647005952954.png






1647005952954.png


Aidha familia hiyo ilitumia fedha hizo kununua kiwanja na kujenga nyumba yao na isivyo bahati nyumba hiyo iliangushwa na tetemeko la ardhi lililotokea kijijini hapo.

Kwa upande mwingine madalali wanaofanya biashara hiyo ya figo wametajwa kuzunguka sana katika kijiji hicho na kuwashawishi Wanakijiji hao kuuza Figo zao
 
Kwani hakuna utaratibu wa kusaini kusaidia wenye shida na viungo pindi unapofariki wanatoa wanachohitaji?

Kwa kweli unakuta mtu anauza kwa mfano halafu baada ya miaka miwili anaishiwa hela
Anachanganyikiwa anaenda tena kuuliza kama wananunua na Kende auze
 
itaongeza mzunguko wa pesa kijana wa ovyo aliropoka 👨‍🦯👨‍🦯👨‍🦯👨‍🦯👨‍🦯
 
Back
Top Bottom