Sababu ni kua wanaamini kule kuna umakini mkubwa katika suala zima la mahusiano,
Huyo mbaba anakua ameshamaliza mambo yote ya ujana kwa hivyo wao ni kutengeneza maisha tu,
Wanajua kudekeza na kubembeleza,
Wanajua kutunza na kuhudumia,
Wana ushauri wa kimaisha,
Kingine kwenye jamii zetu pia huchangia, mfano binti wa 22 akimpeleka nyumbani wa 22 mwenzie au hata 25,
Watadharau na kusema "aaaghr toeni mapenzi yenu ya kitoto hapa"
Lakini akimpeleka jibaba la 40 hata 30
Utasikia "naam sasa hapo umepata, mtu ameshiba machoni, tuanze tu taratibu za ndoa"
Nadhani umepata mwanga kidogo.