30 wazimia kwa kukosa hewa!

30 wazimia kwa kukosa hewa!

ChescoMatunda

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2009
Posts
1,232
Reaction score
444
Wafanyakazi zaidi ya 30 wa kiwanda cha kutengeneza nguo morogoro MAZAVA wamepoteza fahamu kwa kukosa hewa. chanzo ni @itvtanzania
 
Daaah viwanda hivi vya nguo vinataka kuwa janga la taifa sielewi ni kwa sababu serikali haifuatilii mazingira ya uzalishaji au tatizo sijui liko wapi!!
 
Tumefika pabaya, niliyasikia kwenye kaselo ka Mbeya hayo mambo. Kumbe na viwandani hakuna SAFETY!.
 
Hatua kali zichukuliwe kwa Management ya kiwanda ili iwe fundisho kwa viwanda vingine visivo angalia usalamu wa wafanyakazi wao, Mpaka wanafikia kupoteza fahamu hujue ilikuwa msalie mtume tena hapo.
 
Thamani ya Binadamu huwezi linganisha na chochote hatua kali kwa Mmiliki huu ni uuwaji.
 
Ni nini kimesababisha wakose hewa mpaka kuzimia?? Ongeza nyama kwenye hii taarifa Mkuu ili uweze kueleweka vizuri!!
 
Thamani ya Binadamu huwezi linganisha na chochote hatua kali kwa Mmiliki huu ni uuwaji.

Utakuta wana HR hao,kazi yake kuhimiza productivity tu healthy and safety haimhusu.
 
Wadau mliopo morogoro tupeni habari za kina juu ya kiwanda cha nguo kinachoungua msavu...
 
moro umekuwa mji wa matukio kila uchao ni zaid ya mbeya nowdayz.
 
Upande wa management hakuna wakulaumiwa kwani kabla ya kuanza kazi wataalamu huwa wanakagua then wanaruhusu au kutoruhusu sasa nani alaumiwe,uwongozi wa kiwanda au serikali?! aka🙁 SIRIKALI).
 
Maafisa afya huwa wanatembelea hivi viwanda wanachukua hela wanatambaa..rushwa kila mahali!
 
Ujumbe mfupi niliotumuwa kupitia simu yangu ya mkononi muda huu, unasema kuwa zaidi ya wafanyakazi 30 wa kiwanda cha Mazava,Msamvu mkoani Morogoro wamepoteza fahamu baada ya kukosa hewa kufuatia shoti ya umeme kutokea kiwandani hapo.

Source:Bomba FM kupitia mtandao wa tigo.
 
Mmiliki wa hicho kiwanda ni nani? WanaJF mnakumbuka kuna kiwanda ki1(cha nguo pia) pale Tabata, mfanyakazi alishawahi kufungiwa kwenye kontena na uongozi wa kiwanda! Icjekuwa ni mambo kama hayo tena wkati wenye nchi tumekaa kimya.
 
Poleni sana ndg, wafanyakazi, kuna watu wanaitwa OSHA kila mwaka wanazungukia viwanda na sehemu za kazi kuangalia usalama sijui kama walishakagua hicho kiwanda.

Any way kwa sasa poleni sana, tunawaombea mpate nafuu haraka ili muendelee na majukumu yenu ya kila siku kwa maslahi yenu binafsi na taifa.
 
Wafanyakazi zaidi ya 30 wa kiwanda cha kutengeneza nguo morogoro MAZAVA wamepoteza fahamu kwa kukosa hewa. chanzo ni @itvtanzania
Halafu utakuta OSHA imekipa kiwanda hati safi ya uendeshaji bora kwa kuzingatia workers safety!! Kwa hali hii naomba kama kuna certificate ya OSHA pale basi aliyeitoa afukuzwe kazi na kufunguliwa mashtaka mara moja.
 
Mmiliki wa hicho kiwanda ni nani? WanaJF mnakumbuka kuna kiwanda ki1(cha nguo pia) pale Tabata, mfanyakazi alishawahi kufungiwa kwenye kontena na uongozi wa kiwanda! Icjekuwa ni mambo kama hayo tena wkati wenye nchi tumekaa kimya.

Aise ni kweli umetukumbusha. Kilikuwa ni NIDA textile cha wakorea au wamalasia sikumbuki vizuri. Kile si ndugu yetu aliyekuwa mbunge wa kawe kutoka chama cha majambazi alikuwa anajichukulia mihela pale kila wiki!! Yaani ukihadhithiwa historia ya lengo la kuanzishwa kiwanda kile with heavy tax exemptio but kunufaisha tumbo za wachache basi utaona ni kwa nini tunahitaji uongozi mpya toka chama kipya kwa nchi hii. Let us do something!! Kama Kibaki aliweza na ameacha Legacy kwa Wakenya why not trying kwa upande wetu?
 
Back
Top Bottom