singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
SEKTRETARIATI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imetangaza kuwachukulia hatua za kisheria za kuwafikisha mbele ya Baraza la Maadili, Viongozi wa Umma 3,709 ambao hawajarejesha fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni kama ambavyo sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inavyotaka.
Uamuzi wa kuwafikisha mbele ya baraza hilo, umetolewa jana Dar es Salaam na Kamishna wa Maadili wa Sekretariati hiyo, Jaji Mstaafu Salome Kaganda, katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
Jaji Kaganda alisema hadi kufika Desemba 31, mwaka jana iliyokuwa tarehe ya mwisho wa kurejesha fomu, jumla ya viongozi wa umma 11,428 ndio waliorejesha matamko yao kwa Kamishna wa Maadili.
“Hadi kufikia Desemba 31, 2015 jumla ya viongozi 11,428 ndio waliorejesha matamko yao kwa Kamishna wa maadili 3,709 hawajatimiza wajibu huo wa kisheria na hatua zitachukuliwa dhidi yao,” alisema Jaji Kaganda.
Alisema viongozi hao watafikishwa mbele ya Baraza la Maadili na hatua nyingine za kisheria pia zitachukuliwa, iwapo hawatakuwa na sababu za kuridhisha za kutowasilisha kwa wakati fomu hizo.
Katika hatua nyingine, serikali imeanzisha utaratibu wa viongozi na watumishi wote wa umma ambao wako katika mihimili mitatu inayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yaani Serikali, Bunge na Mahakama kutia saini Fomu ya Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wote na Watumishi wote wa Umma.
Jaji Kaganda alisema viongozi hao wanawajibika na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya Mwaka 1995, kutia saini Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma na kurejesha kwa Kamishna wa Maadili kabla ya Februari 28, mwaka huu.
Akizungumzia hilo, Jaji Kaganda alitoa mwito kwa Wakuu wa Wizara, Taasisi na Idara wa sehemu husika kuhakikisha viongozi waliopo kwenye maeneo yao wanatia saini katika tamko hilo.
Alisema kwa kuzingatia Misingi ya Maadili iliyoainishwa katika Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995, viongozi wa umma wanapaswa kuzingatia viwango vya juu vya Maadili.
“Kwa kuzingatia matakwa ya sheria hiyo viongozi wa umma wanapaswa kuzingatia viwango vya juu vya maadili ili kukuza utu, uwazi, uadilifu, uwajibikaji, maendeleo ya nchi na kuimarisha imani ya wananchi kuhusu dhana ya Utawala Bora kwa ujumla,” alisisitiza Jaji Kaganda.