29 Oct na 30 Nov tofauti ni 11.....

29 Oct na 30 Nov tofauti ni 11.....

kanyela mumo

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Posts
2,033
Reaction score
2,124
Kwanza kabisa napenda kupongeza Watu wote ambao wanafanya Taifa ili liwe na Amani, hasa Uongozi thabiti wa Awamu ya tano ikiongozwa na Mh Rais Baba Daktari Mwalimu John Joseph Magufuli.


Kiukweli nimejifunza na ntazidi kujifunza mengi kutoka kwa Rais wangu, pamoja na kujifunza vitu vingi kama njia sahihi ya uwepo wangu hapa Duniani kwasababu najua nina Deni kutoka katika familia yangu na jamii yangu yote ya Kitanzania.

Mwaka 2015 mpaka 2019 nimepata mafanikio makubwa Sana katika Familia yangu na kipato kuongezeka na sikutegea hapa nilipo katika Maisha yangu. Nimekuwa nikibana matumizi na kufanya kazi kwa bidii hakika nimefika hatua kubwa na Watu uniona Kama sio Mtanzania ila sifa ziende kwa Rais wangu maana nilimsoma vizuri uongozi wake nami nikaleta uongozi wake katika familia yangu.

Ndugu zangu naandika haya kwasababu sioni sababu ya kukaa kimya na Kama Rais wangu angekaa kimya nami Maisha yangu yangekuwa kimya na familia yangu ingekuwa kimya na hata jamii forum ningekuwa kimya ila naweza kusema Mh umenipa jeuri haswaa au umetupa jeuri Watanzania haswaa.. Ni kweli binafsi natembea kifua Mbele kwasababu Usawa unao uweka una hakithi Maisha ya wapenda kufanya kazi wengi.


Heshima uliyo tupa kwenye swala la Passport ni kubwa sana Rais wangu, kuna Watu walitoka Nigeria kuja kuchukua Passport ya Watanzania ili wakafanye maovu uko njee ya Nchi.. Ilikuwa ukiwa na milioni 1 mpaka tano unaletewa Passport nyumbani, hakika una stahili pongezi na pongezi za dhati ni hizi kutoka kwangu.

Rais wangu nahaidi ntakuwa moja ya chachu ya Taifa langu.. Nitakufata na kukusikiliza kipindi chote cha Uongozi wako, naapa sitokuwa Negative.. Ntalipa kodi na ntadai risiti ili kuinua Taifa, siwezi kuujumu Taifa langu Mama Tanzania.

Mwisho kabisa nampongeza Mama yangu Jannet Magufuli maana ni mama wa Taifa na pia ni Mama mwenye jina la Marehemu Mama yangu.. Nikimuona namuona Mama jasiri na shupavu Mungu akubariki sana Mama yangu.

Pia nawapongeza viongozi wote Taasisi mbali mbali mbali TRA TPA TCRA na Taasisi binafsi kama Clouds TV Clouds FM mnamchango mkubwa sana katika Maisha yangu. RIP Ruge na Kibondez.

Bila kumsahau Bibi na Babu yangu Katavi mmenilea vyema Sana kiasi kwamba nahisi ni mtu mwenye bahati kuwa mjuu wenu Sina cha kuwalipa zaidi..

Nashukuru wote nilio pita katika mikono yenu nikiwa House boy, Mpika chips, Dobi, Gardener, kontakta, muuza maji, muuza mayai, wateja nilio waoshea Magari, Wazee wakuongeza sifuli mnajijua, na mambo mengi yanaweza kuchukua ukulasa mzima shukrani kwenu.


Nakushukuru ulietaka kunigeuza mwanamke usiku ule kisa sina sehemu ya kulala nakushukuru sana maana ulinifanya nijue watu na kuwa na Hasira na Maisha..


Nashukuru waganga wote wa jadi nilio pitia bila kumsahau mganga wa Mwisho kule Bomani Tanga ulie niambia nina nyota kubwa sistahili kwenda kwa Mganga..

Nashukuru wauza Bange wote maana nilipata utulivu kwa bei ndogo kabisa.


Nawashukuru wote tulio kuwa tunatoa Pombe ya Gongo Mkuyuni kuleta Dar es salaam usiku.


Nashukuru Wananchi wote wapenda Amani na wafanyakazi kwa bidii...

Nashukuru Afande ulie niweka katika buti la Yundai karibu siku nzima nikahisi kukata roho ghafla nikanena na Muumba wangu nimekukosea nini Mungu mbona mimi Bado mdogo kwanini nistahili kifo wakati sijatimiza malengo yangu. Nakushukuru sana maana niliona nguvu za Maombi.

Nashukuru wana Jamii forum.. Hasa kaka Mshana jr umekuwa unanijenga kwa namna nyingi.

Mwisho kabisa nashukuru tena Mh Rais kwa kuanza Ujenzi wa barabara kutoka Katavi mpaka Tabora.. Hakika wewe ni njia ya Watanzania Mungu akujalie Baba.

Nilitaka kusahau, namshukuru mke wangu kwa kunizalia Watoto watatu wazuri wananipa nguvu na hamasa ya kusonga mbele katika kutafuta riziki bila kukata tamaa.. Hakika wewe Mke wangu ni Malkia wa nguvu Mungu akujalie kipenzi changu, nikikukosea sijadhamilia maana nina Mwili na nafsi.

Heshima kwa Mama zetu wote.


Thanks King Crazy GK.. Heshima kwako.


One love kwa wote be Positive










Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unatakiwa kujua kwamba siku zote unapokua unasifia kitu kuna watu wao wataponda hivyo hupaswi kulazimisha watu wote wawe na mtazamo kama wako..hivyo kama wewe unanufaika na hii hali kuna wanaoumia wengi sana..na wao wana sauti zao zinazohitaji kusikika..ila hujaweka mifano dhahiri ya uhusiano wa ulipokua ukifanya kazi kwa bidii na kupunguza matumizi a hali hii ya sasa hivi..ukifanya hivyo itakua jambo jema sana..
 
Unatakiwa kujua kwamba siku zote unapokua unasifia kitu kuna watu wao wataponda hivyo hupaswi kulazimisha watu wote wawe na mtazamo kama wako..hivyo kama wewe unanufaika na hii hali kuna wanaoumia wengi sana..na wao wana sauti zao zinazohitaji kusikika..ila hujaweka mifano dhahiri ya uhusiano wa ulipokua ukifanya kazi kwa bidii na kupunguza matumizi a hali hii ya sasa hivi..ukifanya hivyo itakua jambo jema sana..
Kuchukua Yebo Yebo Pics Mia Mia na kisha kuziuza kila sehemu yenye kituo cha Daladala kwenye watu wengi hapa Dar es salaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu yangu Darasa la sita tafadhali mnisamehe kwa kuwa na mpangilio mbovu ila sasa hivi najifunza YouTube how to grow up with it.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwaio kabla ya Magufuli kuingia madarakani hilo jambo lilikua haliwezekani?
Inawezeka ila nazungumnzia USAWA ulikuwa mdogo sana tofauti na sasa mpaka Wamachinga wana vitamburisho.

Japo kuna wengine wanakandia ila wengi tuna nufaika navyo maana Ruksa kokote Baba kasema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana kwa kufanikiwa,na Mwenyezi Mungu azidi kuonesha njia, pale kwenye changamoto tuzidi pamba,Sina tatizo na taasisi ya Uraisi, shida ipo kwenye wanasiasa uchwara wanaojificha chini ya mwamvuli wa mwenyekiti wa cmm, hao ndio wamelichelewesha taifa hapa tulipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru wauza bange wote

Nashukuru uliyetaka kunigeuza mwanamke

Nashukuru waganga wote

*never give up
 
Nilichogundua ni utajiri wa shukrani ulionao. Kwamba hadi aliyetaka kukuhifadhi kinamna kwa kukosa pa kulala umemshukuru!., kumbuka kuwakaribisha ulipo ili wafurahie mafanikio yako na kuwasaidia wasio na grisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezeka ila nazungumnzia USAWA ulikuwa mdogo sana tofauti na sasa mpaka Wamachinga wana vitamburisho.

Japo kuna wengine wanakandia ila wengi tuna nufaika navyo maana Ruksa kokote Baba kasema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usawa unapatikana kwa machinga wenzio kulazimishwa kuvinunua hivyo vitambulisho au? Na kupewa vitisho wasiponunua vitambulisho hicho? Halafu hujasema usawa wa hao wamachinga ulikua kwenye nini amabapo kipindi cha nyuma haukuwepo..
 
Usawa unapatikana kwa machinga wenzio kulazimishwa kuvinunua hivyo vitambulisho au? Na kupewa vitisho wasiponunua vitambulisho hicho? Halafu hujasema usawa wa hao wamachinga ulikua kwenye nini amabapo kipindi cha nyuma haukuwepo..
Umeshawahi kuuliza Wahusika kwanini wanalazimishwa kuwa navyo?

Najua wana lazimishwa kwa nia nzuri ili kuwa huru na Biashara zao.. Be positive be a gentleman

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenifumbua macho baada ya kuwashukuru wauza bange wote. Nikagundua kuwa hiki cha leo ulipokuwa unaandika; Naamini ni cha kutokea Archugaaa si bure. Ila jambo la maana, ulikuwa umekaa unapovuta.
 
Umenifumbua macho baada ya kuwashukuru wauza bange wote. Nikagundua kuwa hiki cha leo ulipokuwa unaandika; Naamini ni cha kutokea Archugaaa si bure. Ila jambo la maana, ulikuwa umekaa unapovuta.
Nimeshukuru kwasababu lasimi leo nimeacha Bangi, serikali yangu ikiruhusu ntarudi kuivuta maana ni kitu kizuri kwangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom