25 kila mwezi mishahara uwe tayari

25 kila mwezi mishahara uwe tayari

kamtesh

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Posts
1,395
Reaction score
514
Palitolewa waraka kutoka serekalini kwamba kila 25 ya kila mwezi, watumishi wawe wameshalipwa mishahala yao. Lakini kadri miaka inavyo songa mbele, wahusika wamekua wanazembea mpaka watumishi wana pata mishahara mwisho au mwanzoni mwa mwezi unao fwata. Tatizo liko wapi wahusika? Nchi hii ni kinara wa kupuuza maagizo na sheria sana.

Tunaomba vyombo husika warejee kwenye huu waraka. Tatizo liko wapi la mishahara kucheleweshwa?
 
Tangu mwaka jana sijawahi pokea mshahara zaid ya tar25
Kila ikifika tar 24 usiku kitu huwa tayali kimesoma!
 
Mbona tangu jana mchana kwangu ilishasoma?
 
unataka ulipwe mapema je ukienda kununua bidhaa Dukani unadai risiti ili Serikali ipate kodi itayofanya ulipwe mapema
 
Kwani walimu wameongezewa mshahara?Masikini walimu jaman,kamshahara kao kadogo hadi dhambi,waongezen na wapunguziwe PAYE
 
Kwani walimu wameongezewa mshahara?Masikini walimu jaman,kamshahara kao kadogo hadi dhambi,waongezen na wapunguziwe PAYE

Unaropoka au una uhakika? Mdg wangu mwl na me mhasibu wote tuko serikalin mbona hatutofautiana sana? Sema wao hawana marupurupu! Fanya uchunguz kabla ya kuropoka
 
Kwani walimu wameongezewa mshahara?Masikini walimu jaman,kamshahara kao kadogo hadi dhambi,waongezen na wapunguziwe PAYE

nani kakuambia mshahara wa mwalimu ni mdogo? Mwalimu wa digrii analipwa mshahara wa sh. 716,000 ni hii ndo at appointment. Mbona huo unalingana na mshahara wa watumishi wa serikali ambao shahada zao ni za miaka mitatu. Au labda mniambie TGS D sio around 700 hadi 800 elfu. Labda ukisema mdogo unalinganisha mishahara ya BOT, TANAPA, TRA n.k. ambapo ni mahala pengine. Nawasilisha.
 
Typical slave attitude..

Kwanini usijilipe mshahara mwenyewe kila siku?!
 
Typical slave attitude..

Kwanini usijilipe mshahara mwenyewe kila siku?!

Wewe unajilipa ngapi kwa siku mkuu? Hata mimi natamani kuachana na haya mambo ya kusubiria kila mwezi, kodi tu unakatwa karibia 830,000/=

Nilitaka kuingia kwenye kulima miwa Morogoro nasikia wamechoma mashamba ya watu, bado nafuatilia hizo habari nijue nini cha kufanya mkuu.
 
mwezi Jana mshahara ulitoka trh 21/11/15
Mwezi huu imekuwa ndivyo sivyo mpaka sasa hakuna kitu Sababu nini?
 
Wewe unajilipa ngapi kwa siku mkuu? Hata mimi natamani kuachana na haya mambo ya kusubiria kila mwezi, kodi tu unakatwa karibia 830,000/=

Nilitaka kuingia kwenye kulima miwa Morogoro nasikia wamechoma mashamba ya watu, bado nafuatilia hizo habari nijue nini cha kufanya mkuu.
Nikikwambia ninachojilipa utanipa bonus mkuu.., au lengo unataka kucompare..? hahahahahah...
 
Unaropoka au una uhakika? Mdg wangu mwl na me mhasibu wote tuko serikalin mbona hatutofautiana sana? Sema wao hawana marupurupu! Fanya uchunguz kabla ya kuropoka

Hayo marupurupu ndiyo yanayomfanya mwalimu atofautiane na mfanyakazi wa kada nyingine...!!!

Ikitokea mfanyakazi wa kada nyingine anapata marupurupu wanayofikia robo au nusu ya mshahara wake...huoni kuwa anakuwa amemzidi pakubwa mwl...!!?

Tafakari...!!!
 
Rais atakayeweza kusimamia hilo ndo utakuwa mfano mzuri kidogo BM aliweza
 
Back
Top Bottom