24K together for Kagera

24K together for Kagera

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
Kwa pamoja tunaweza nunua tshirt. Hizi ili kwa pamoja tuweze kuchangaia wahanga wa tetemeko la ardhi kagera
1473939414514.jpg
1473939424378.jpg
 
Wanaohitaji tshirt hizi ni pm tafadhari.
 
Hapana sio fursa ya kupiga hela kuna campain tuaniandaa kwa changizo maalumu litahusu chakula cha asili,ya kagera, muziki wa asili, ya kagera. Na mengineyo katika tukio hili tunaamini tutapata kiasi kifaacho japo kidogo kama mchango wetu, hivyo hizi tshirt ni utangulizi tu wa tukio lifuatalo..kama ukipenda npm# nikutumie wimbo maalumu wa changizo hilo.. Na video yake soon
 
Nawe pia waweza shiriki sbbu enzi za kusubiri wafadhiri katika maafa zimepita kumbuka inaanza na wewe wengine wanafuatia. Pia unakaribishwa katika kampeni hiyo.
 
Hapana sio fursa ya kupiga hela kuna campain tuaniandaa kwa changizo maalumu litahusu chakula cha asili,ya kagera, muziki wa asili, ya kagera. Na mengineyo katika tukio hili tunaamini tutapata kiasi kifaacho japo kidogo kama mchango wetu, hivyo hizi tshirt ni utangulizi tu wa tukio lifuatalo..kama ukipenda npm# nikutumie wimbo maalumu wa changizo hilo.. Na video yake soon
Si ungeweka maelezo yote yanayojitosheleza hapo mtu anasoma anaelewa. Sema wazi hizo hela za tisheti zinakwenda wapi na zitatumikaje. Mbona huwa ni vigumu sana kwa sisi Wabongo kuweka tangazo linalojitosheleza? Ujanja ujanja tu kila kona.

Mimi siwezi kushiriki kwenye hilo tamasha bila kujua kama mchango wangu kweli utawafikia wahanga au utaishia mikononi mwa wajanja akina Getrusa. Kuna njia nyingi nyingine za kufikisha mchango wangu huko na hii yako SIYO!
 
Toa maelekezo ya kutosha kiongozi. Wapi tshirts zinapatikana na kwa shilingi ngapi. Ikiwezekana na mawasiliano.
 
Kuna numbers ambazo mfuko wa Serikali wa maafa umezitoa.
Sasa ingekuwa busara mngeungana nao ili mtu akinunua fulana pesa inaenda moja kwa moja kwenye mfuko kisha nyie mnarejeshewa gharama mlizotumia.

Hapa ni kujua gharama gani mmetengeneza fulana na faida yake ndio iende kwenye maafa.
Maana nisawa na fulana za kwenye misiba au Majeneza yanapouzwa,pale huwa ni faida.

Hili tukuo ni kwa vile tu limekuwa la kidunia na la kiajabu kwa ukanda wetu,ila maafa zaidi ya hayo kama Bus kuuwa watu telee,lakini hakuna mchango hata mmoja uliotoka na familia zinateseka.
Sema hili linaboost issues,na hapa ndio umuhim wa Bima unakuja hapa.
Ningeshauri Serikali ihamasishe kuhusu Bima,maana Wa TZEE ni wabishi ile mbaya,ila wenye bima hapo wanapeta tu na maumivu yanakuwa sio sana kwa mali na majeruhi
 
Ila Mungu atusamehe kama Mleta Post unania nzuri.
Tatizo ni kwamba wale wasio waaminifu ndio wanatia Doa wale wenye nia njema.
Kama ni kwa nia njema basi Mungu atakupa wepesi
 
Duuh, basi sawa nikuibie ili iweje? Nimeona jamii forum ni sehemu ya kulielezea kwa upana kiasi.. Nadhani ukiwa na mashaka usinunue! Ila ukiwa na nafasi njoo kwenye hilo tamasha na wanao ili angalau wajue chakula cha asili,ngoma za asili na mengineyo.. Lakini pia ukiweza zile nguo ambazo wewe huzitumii tena zaweza wafaa sana wenye uhitaji huo.tuletee.na ukiona bado hutuamini.basi tunakushukuru hata kwa maoni yako.
 
Kumbuka sisi tunafanya yaliyo ktk uwezo wetu. Ni vema ukatushauri namna ya kuboresha tunapokosea sababu ni letu sote na linaanza na wewe!!!!
 
napenda kujua mchango wa clouds media kwenye haya maafa maana naona wamegoma kabisa kusitisha fiesta yao
 
Back
Top Bottom