Bado,hatuna vision,kila siku ni visingizio.Inawezekana kufanya kazi masaa 24/7.
Hata uchumi utazunguka mara mbili;chukua mfano kampuni ya basi iwe na basi mbili za mchana na usiku,yaani wauza chakula,nao watauza mchana na usiku.
Mifano ya shughuli zitakazo saidia kukua kwa uchumi:
[1].mfanyakazi anaishi songea ataweza kusafiri,ijumaa usiku na jumamosi asubuhi anakata tiketi ya kuangalia mechi ya jioni ya mpira Dar,national stadium na usiku wa jumamosi anarudi Songea.,na jumapili inamkuta yupo songea.na JUmatatu anaripoti kazini kwake kama kawaida;kwa mfano huu pato linakuwa limeingia kwa kampuni ya usafiri,uwanja wa mpira unapata mapato.!!!
[2].Usafi wa mji unafanyika usiku;mfanyakazi mwenye bidii anaweza kuwa na kibarua cha mchana na usiku,hivyo kuongeza kipato chake maradufu.
[3].kwa wale wafanyakazi,au wafanya biashara wasio kuwa na muda wanaweza kusoma usiku bila kuathiri shughuli zao za mchana.
[4].ajira itaongezeka kwani shift zitakuwepo kwa kila shughuli inayotekelezwa kwa saa 24.!!!(vitu vya mafuta,hoteli na migahawa,kampuni za basi upande wa madereva,
[5]mifano ipo mingi ya kuufanya uchumi wetu ujiendeshe masaa 24,inabidi viongozi wafunguke waache mambo ya kizamani,eti usalama ni mdogo usiku,mbona majirani zetu waweze sisi tushindwe tunanini?!!
[6].Hebu angalia vijijini wanalala mapema,na umasikini na kipato ni kidogo kwa sababu shughuli za kiuchumi zinaishia saa 12 pekee.!!!!!,hebu twende saa 24.
[7].Fikiria simu za mkononi zingezimwa saa 12 jioni ingekuwaje?!!,TUNA KAZI YA KUFANYA KUBADILI MTAZAMO .!!