2030-2040 CCM itakuwa imekufa kabisa

2030-2040 CCM itakuwa imekufa kabisa

Kinjekitile Jr

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
592
Reaction score
1,698
Kama CCM isipoweza kutafuta mbinu au njia mpya ya kutawala watu,uwenda miaka 10 mbele kusiwepo tena na chama cha Siasa kinacho itwa chama cha mapinduzi

Zaidi ya 50% ya Watanzania ni vijana waliozaliwa Miaka ya 2000’s,yani kwenye sensa ya mwaka 2002 Watanzania walikuwa ni million 30 lakini leo wanaelekea kufika 70 baada ya miaka kumi mbele watakuwa ni zaidi ya millions 90 na ambao million 75 watakuwa ni vijana wa chini ya umri chini ya miaka 30

Hawa wataingia mtaani wakiwa Nchi imeyumba kiuchumi,hali ya kiusalama itakuwa mbovu,utawala utakuwa unaendeshwa na watu walio kosa weledi na mwishoo kabisa kutakuwa hakuna ajira ya kuwaajiri vijana wote hawa

Hawa vijana nusu yao watakuwa na elimu ya darasani na ata wale watakao kosa elimu bado watakuwa na uelewa kutoka kwenye mitandao ya kijamii…….zile nyimbo za kuwa tulinde amani ya Nchi yetu uwenda zitakuwa zimefika Mwisho kabisa

Kizazi cha sasa kinahitaji kuongozwa kwa akili na sio mabavu au propaganda za AMANI NA HOFU YA kunyang’anywa RASILIMALI kama awamu zingine zilivyo fanya kwa kuwalaghai vijana wale

CCM imekosa mbinu na watu makini wa kuweza kung’amua mambo na kuona kuna jambo baya linakuja

Ata hawa vijana waliopo ccm wengi wao hawaipendi ccm ila wapo pale kwa maslahi binafsi

Mtaani sifa ya ccm imechafuka sana na hii ni anguko kwa ccm

Uwenda mbeleni tukapata uongozi wa kijeshi au CHADEMA wakachukua Nchi kama wakileta katiba mpya ndani ya miaka hii mitano
 
KIKUBWA LINDA AMANI YA NCHI YAKO

CCM NI CHAMA ILA NCHI NA AMANI YAKE NDO MUHIMU , KIJANA KATAA KUTUMIKA LINDA UHAI WAKO
 
Hata sasa hakuna ktu kiitwacho ccm mbnu yao ya mwsho ni kutumia polisi na kuwatia uwoga watz nayo ndo imeisha mo29 hawana jpya tn.
 
Kama CCM isipoweza kutafuta mbinu au njia mpya ya kutawala watu,uwenda miaka 10 mbele kusiwepo tena na chama cha Siasa kinacho itwa chama cha mapinduzi

Zaidi ya 50% ya Watanzania ni vijana waliozaliwa Miaka ya 2000’s,yani kwenye sensa ya mwaka 2002 Watanzania walikuwa ni million 30 lakini leo wanaelekea kufika 70 baada ya miaka kumi mbele watakuwa ni zaidi ya millions 90 na ambao million 75 watakuwa ni vijana wa chini ya umri chini ya miaka 30

Hawa wataingia mtaani wakiwa Nchi imeyumba kiuchumi,hali ya kiusalama itakuwa mbovu,utawala utakuwa unaendeshwa na watu walio kosa weledi na mwishoo kabisa kutakuwa hakuna ajira ya kuwaajiri vijana wote hawa

Hawa vijana nusu yao watakuwa na elimu ya darasani na ata wale watakao kosa elimu bado watakuwa na uelewa kutoka kwenye mitandao ya kijamii…….zile nyimbo za kuwa tulinde amani ya Nchi yetu uwenda zitakuwa zimefika Mwisho kabisa

Kizazi cha sasa kinahitaji kuongozwa kwa akili na sio mabavu au propaganda za AMANI NA HOFU YA kunyang’anywa RASILIMALI kama awamu zingine zilivyo fanya kwa kuwalaghai vijana wale

CCM imekosa mbinu na watu makini wa kuweza kung’amua mambo na kuona kuna jambo baya linakuja

Ata hawa vijana waliopo ccm wengi wao hawaipendi ccm ila wapo pale kwa maslahi binafsi

Mtaani sifa ya ccm imechafuka sana na hii ni anguko kwa ccm

Uwenda mbeleni tukapata uongozi wa kijeshi au CHADEMA wakachukua Nchi kama wakileta katiba mpya ndani ya miaka hii mitano
Kwani hata sasa ipo, wale waliotokea kuua watu kuanzia 29 october wale ndio hasa ccm yenyewe. Hawa wafuasi ni koti tu. Vurugu za juzi tu hakuna wanaccm wanathubutu kuvaa sare za ccm, sasa hapo kuna chama ama kikundi cha dola?
 
2030 - 2040 kinakuja chuma kingine cha CCM ❤️
Kudumu chama cha mapinduzi
KAZI na Utu Tunasonga Mbele
Mungu mubariki Rais wetu Dr Samia Suluhu Hassan
 
Back
Top Bottom