Mapinduzi rahisi ya mfumo wa nchi yatatokea ndani ya CCM

Mapinduzi rahisi ya mfumo wa nchi yatatokea ndani ya CCM

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
1,199
Reaction score
2,869
Sio kwamba wana CCM wote wanaipenda CCM, sio kwamba vijana walioko CCM wanajivunia chama chao, na wala usidhani hawaumii kuona kila aina ya uovu wa nchi hii unahusishwa na CCM. Ni binadamu, wanayaona makosa, wanaumia lakini watafanyaje sasa na ndo wako mateka! Hawana uhuru, fikra zao zimeshikiliwa mateka

Wanaokusanya taarifa za kumfanya Nyerere kuwa mtakatifu sio wajinga. Huyu mzee ni kiumbe cha pekee kilichozaliwa Tanzania

Aliyoyasema kwenye hotuba zake za miaka ya 1960's, 1970's, 1980's na early 1990's ukiyasikiliza na kulinganisha na yanayoendelea ni kama ameyaongea leo wakati hata jeneza limekwisha oza lote

Nyerere aliwahi kusema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM! Hili bado naliamini na ukipenda unaweza kusema "waasi wa uasi wa CCM" ndio watakaoikomboa nchi kwa mara ya pili

Hawa machawa wanaojengwa sasa hivi, hawa UVCCM wanaojitoa ufahamu na kugeuka mazezeta siku hizi ipo siku watapata akili na siku hiyo ndio itakuwa ukombozi wa nchi hii

Sasa hivi wanagugumia tu ndani kwa ndani huko, wanasifia hata mtu wao akijamba hadharani lakini hawatavumilia siku zote kwasababu mwanadamu ameumbwa na haya

Ukitaka kulielewa hili vizuri kaa nao, jifanye marafiki kwao, anzisha story, sikiliza maoni yao, kaa upande wao utayajua mengi

Haya yanayoendelea wametulia kama sio wao. Magroup yao wamepoa hakuna chochote wanachoongea, wamezibwa midomo, wanahofu hata ya kusalimia wanahisi watakosea

ÇCM imewaweka mateka watu wao, vijana wao wako mahabusu wasipoweza ku exercise uhuru wao! Hili ni bomu la baadae

Hakuna wanaokaa mateka siku zote ni ama watatoroka, watakufa au watakombolewa. Tuwaombee wakombolewe au watoroke wasifie mikononi mwa watekaji wa fikra
 
Back
Top Bottom