2026 FIFA World Cup - Special Thread

2026 FIFA World Cup - Special Thread

Orodha ya wachezaji waliocheza mechi nyingi zaidi za mashindano ya Kombe la Dunia
IMG_0240.jpeg
 
Ni Michuano ya 23 ya Kombe la Dunia la FIFA ambapo kwa mwaka huu itakuwa inafanyika kwenye nchi tatu kwa pamoja ambazo ni Marekani, Canada na Mexico.

Michuano hiyo itaanza June 11 mpaka July 19 mwaka huu. Huku idadi ya timu ikiongezeka kutoka timu 32 mpaka 48.

Waandaji Canada itakuwa ni mara yao ya kwanza kuandaa, huku Marekani akiandaa kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo mwaka 1994. Mexico watakuwa wakiweka rekodi ya kuwa Taifa la kwanza kuandaa kwa mara ya tatu baada ya kufanya hivyo mwaka 1970 na mwaka 1986.

Lakini pia, Fainali za mwaka huu zitakuwa za pili kuwa na mwenyeji zaidi ya mmoja baada ya zile za mwaka 2002 zilipoandaliwa kwa pamoja kati ya Korea Kusini na Japan.

Nchi za Cape Verde, Curacao, Jordan na Uzbekistan zitakuwa zikishiriki kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo. Nchi za DRC na Haiti zitarejea katika mashindano hayo baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho mwaka 1974.

Uwepo wa team 48 kwa mara ya kwanza kutakuwa na idadi ya makundi 12 huku kila kundi likiwa na timu 4 kama ilivyoada huku idadi ya mechi ikiwa 104 kutoka 64 iliyokuwa awali.

Afrika tutawakilishwa na jumla ya timu 10 zikiwa ni DRC, Algeria, Cape Verde, Egypt, Ghana, Ivory Coast, Morocco, Senegal, South Africa na Tunisia.

Jumla ya waamuzi wa kati 52, huku washika vibendera wakiwa 88 na 30 wakiwa ni marefarii wa VAR wamechaguliwa kuchezesha michuano hiyo.

Jumla ya majiji 16 yatakuwa tayari kuandaa mitanange ya Kombe la Dunia kutoka katika nchi tatu huku mechi nyingi zikipigwa katika nchi ya Marekani ikiwa na majiji 11, Mexico majiji 3 na Canada majiji 2.

Mechi ya Ufunguzi ni baina ya wenyeji Mexico dhidi ya South Afrika katika dimba la Azteca ambalo lina historia ya kutosha katika soka. Hilo ndio dimba alilofunga Maradona goli la mkono wa Mungu dhidi ya England pale mwaka 1986.

Wakati mchezo wa Fainali utapigwa katika dimba la Met Life jijini New Jersey nchini Marekani.

Mpira rasmi wa mashindano ya mwaka huu unafahamika kama Trionda ukitengenezwa na kampuni ya Adidas ukiwa na maana ya Umoja wa nchi tatu wenyeji ambazo ni Canada, Mexico na Marekani.

Kampuni za Fox, NBC Universal, Bell Media zimepewa kandarasi ya kuzalisha maudhui yote fainali hizo za mwaka huu na kuwauzia wengine katika mataifa mengine duniani.

Wadhamini wakuu wakibakia kuwa ni Adidas, Cocacola, Aramco, Hyundai, Lenovo, Qatar Airways na Visa.

Tiketi za hatua ya makundi zitaanzia Usd 60 sawa na Tshs 155,860. Huku mchezo wa Fainali tiketi ya juu ni USD 6730 sawa na Tshs 17,482, 349. Lazma ujipange. Tiketi zimeanza kuuzwa tangu September mwaka 2025.

Zawadi zimeongezeka kutoka World Cup ile ya Qatar. Mshindi wa kwanza atabeba USD Milioni 50, Mshindi wa pili USD Milioni 33 na Mshindi wa Tatu ni USD Milioni 29.

Team zinazopewa nafasi kubwa ya kubeba taji hilo mwaka hii ni Ufaransa, Ureno, Argentina, Spain na Uingereza.

Changamoto kubwa katika mashindano ya mwaka huu ni muda kwasisi huku ukanda wa Afrika Mashariki. Kuna mechi zitakuwa zikipigwa saa 1 usiku, saa 4 au 5 usiku na nyinginezo hadi saa 9 usiku.

Vikosi vitaanza kuitwa mwishoni mwa mwezi huu May, hivyo kupitia uzi huu utapata dondoo zote kuhusu mashindano hayo.

Karibu tuwe sote…
Kwa maoni yangu michuano ya kombe la dunia2026,

ni mapambano ya mpira wa miguu baina ya mataifa ya France, England, Hispania, Portugal, Germany, Argentina, Brazil and Germany,

mataifa mengine ni wasindikizaji tu kulingana na maandalizi yao yalivyokua yasiyo na matumaini ya kuleta changamoto dhidi ya mataifa makubwa na yenye maandalizi kabambe.

Yeyote miongoni mwa mataifa hayo niliyoyataja anaweza kubeba ndoo ya dunia 2026🐒
 
Kwa maoni yangu michuano ya kombe la dunia2026,

ni mapambano ya mpira wa miguu baina ya mataifa ya France, England, Portugal, Germany, Argentina, Brazil and Germany,

Kombe hili ni la Hispania
 
Sawa mkuu, ngoja tuone
 
Back
Top Bottom