Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,954
- 142,084
Sasa kwanini watu wauhusishe uteuzi wa Bashiru na uongezwaji wa mihula?Katiba ipo wazi. Mwisho ni mihula miwili.
Mzee waacheni tu mtateseka bure kujibizana nao. Rejea mwaka 2015.....ilifikia hatua akisa Sugu walimuita Kikwete kuwa ni Nkurunzinza wa Tanzania...kila siku walikuwa na press za kuitaka tume ya Taifa ya Uchaguzi itangaze tarehe ya uchaguzi.Sasa kwa nini watu wauhusishe uteuzi wa Bashiru na uongezwaji wa mihula?
Na siyo CUF tu....hata CHADEMA.Mkuu usiwe mchoyo wa ukweli kufanya siasa za upinzani nchini ni vigumu mno na ilikuwa rahisi kwa ANC kufanya siasa ndani ya SA kipindi cha utawala wa kibaguzi wa makaburu kuliko kwa CUF kufanya siasa ndani ya Tanzania ya President Magufuri.
Ahaaa!Kauli ya Bashiru Ali kuwa watashinda uchaguzi kwa kutumia Dola na hata wengine(wapinzani ) wakishika dola wataitumia kubaki madarakani kwa nguvu.....
Sasa kwa nini watu wauhusishe uteuzi wa Bashiru na uongezwaji wa mihula?
Usiwe na hofu....CCM inawatu wazuri sana wakukemea jambo kama hilo. Na tunavija ambao wanauwezo mkubwa sana wa kukemea hata wazee pale watakapopotoka.Wasi wasi unakuja kwa vile tayari kuna watu walishaanza kutest mitambo, kuanzia bungeni mpaka kwa wasataafu wenye kuheshimika katika hii Nchi, mashaka zaidi yanakuja kwamba hakuna kiongozi yoyote wa CCM ambaye ameshawahi kukemea hili kwa KUMAANISHA, narudia kwa KUMAANISHA ukiacha Mzee Mkapa ambaye hatunaye kwa sasa.
Hilo ni moja, lingine linalonitia shaka ni nani atajaribu kuinua mdomo kusema, kuandika au hata kuonyesha dalili ya kupingana na hilo suala siku litakapoamuliwa, angali vyombo vya habari vilivyojikunyata, hakuna atakayepinga ikitokea siku imeamuliwa hivyo.
Dr. Bashiru amekuwa sehemu kubwa ya ushindi haramu na wa kishindo kwa CCM 2020, pengine akawa tena sehemu ya mageuzi ya Katiba yetu kufanikisha kile wengi wanachokihofia.
Niseme tu kwamba Mh. Rais amekuwa msema kweli na mpenzi wa Mungu wakati wote, hope hili linalosemwa hatalikubali hata alazimishwe vipi.
Ni hayo tu.
Kwani mtu hawezi kubadili mawazo?Kuna clip ipo humu mitandaoni ikimuonyesha Bashiru akiapa kuwa hatukubali akipewa nafasi nyingine zaidi ya huo ukatibu mkuu. Kama Magufuli hana nia kujiongezea muda, ni kwanini amchague mtu aliyekiri mbele yake, na hadharani kuwa hayuko tayari kupatiwa nafasi nyingine tena?
Ile ilikuwa na kauli ya ndani ya chama......ameteuliwa kuingia serikalini.Kuna clip ipo humu mitandaoni ikimuonyesha Bashiru akiapa kuwa hatukubali akipewa nafasi nyingine zaidi ya huo ukatibu mkuu. Kama Magufuli hana nia kujiongezea muda, ni kwanini amchague mtu aliyekiri mbele yake, na hadharani kuwa hayuko tayari kupatiwa nafasi nyingine tena?
Na siyo CUF tu....hata CHADEMA.....
Miaka ya 2010 mwishoni hadi na 14....hakuna mwana CCM alikuwa anathubutu kuvaa sare ya chama mtaani.....yaani tulikuwa tunazomewa kila kona.
Mambo yamebadilika.......CCM sasa tunatamba. Na itaendelea kuwa ngumu kufanya siasa mpaka pale wapinzani watakapotambua kuwa CCM ndicho chama tawala Tanzani....ili wakati watakapokuwa wanakosoa wakosoe wakijuwa wanaongea na chama kikubwa na wawe na adabu.
Kwani mtu hawezi kubadili mawazo?
Ile ilikuwa na kauli ya ndani ya chama......ameteuliwa kuingia serikalini.
Na pia hata kwa ustaarabu tu wa kawaida.....asingeweza kumkatalia Rais wa nchi na kwa nafasi nyeti kama ile.
Kingine,mwanasiasa akisema kitu,angalia nyakati na mazingira.
Mwaka 2010 Kiwete alibana na Slaa akajikuta anaahidi kila kitu. Yaani hata angekuta dimbwi mahali angeweza kuahidi meli. Zilikuwa nyakati ngumu na mazingira magumu ya siasa za wakati huo.
Kwa wakati Bashiru anatoa kauli ile....tulikuwa tunaelekea uchaguzi mkuu.....analikuwa anasisitiza jambo.