2015 vijana twendeni na january makamba kuwa rais

Ndugu wana jamvi wa Jf, leo nami nimeona niwasilishe sehemu ya mawazo na uhalisia wa mambo yalivyo katika maisha yetu kwa sasa. Nikiwa sehemu ya kundi kubwa (VIJANA) lenye maamuzi na hatma ya taifa letu na maisha ya baadae.
Ni hakika tumeshuhudia na kuona matukio makubwa na historia nyingi ndani ya nchi zikitokea, mfano kujiuzuru kwa aliyekuwa waziri mkuu,Richmond, EPA, Dowans, Kikombe cha babu, Umeme wa mgao, Ujio wa rais Obama, Katiba Mpya n.k lakini mimi nimeguswa zaidi na historia zilizowekwa na itakayowekwa hivi punde na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeshuhudia miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika na punde tu tumetoka kushuhudia maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, ndani ya miaka 50 ni mengi mazuri na mema serikali imejitahidi kufanya kwa wananchi wake kutokana viongozi walioshika madaraka. Lakini historia kubwa ninayoiwaza mimi ni ile tunayoenda kuifikia ya kutimiza miaka 50 ya MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzabar, miaka 50 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 26/04/2014 sitaki kuzungumzia Muungano kwa kuwa nimeshatoa maoni yangu kwenye tume ya rasimu ya katiba mpya bali nataka vijana kwa pamoja tukiweka mbali maslahi ya vyama, ukabila,udini, ukanda na maslahi binafsi. Tujadili na tujiandae kisaikolojia hususan kuhusu kiongozi wa nchi, mkuu wan chi, rais mteule ajaye tutakuwa hatuna tofauti na wazee ambao fungu lao ni kuota ndoto (malengo mafupi) kama tukisema tusubiri hadi vyama vitangaze nani atagombea bali tutakuwa tunajidhihirisha kuwa sisi ni vijana wenye maono (malengo na mitazamo yote ya muda mfupi na mrefu) kwa kuanza kujadili mustabali wa maisha yetu ya baadae sasa. Ukweli ni kwamba maisha ni magumu na yanachangamoto nyingi sana hasa kwa sisi vijana, maisha yamekuwa ghali sana, umeme juu, ajira finyu na chache nk lakini kitu kizuri ni kwamba tunaweza kubadili hii hali ingawaje nchi yetu ni changa kwenye viwanda na teknolojia lakini ili limechangawia na kuwa na viongozi wanaoota ndoto ni dhahiri tunahitaji kupata mtu mwenye maono ili aiponye nchi yetu yenye kila aina ya rasilimali, tunahitaji kumpa kijana atakayeweza kutuunganisha na kutumikisha sehemu ambayo tutaweza kunufaika na utajiri tulionao wa maliasili,madini,maji na vijana kama nguvu kazi, tunahitaji kumpata kijana wa jamii ya January Makamba atupeleke kwenye nchi yetu ya maono, Tunamwitaji January Makamba aiponye nchi na ukoma wa umaskini, ajira, na usimamizi uliobora wa rasilimali zetu.
Mimi ni mkristo hivyo usoma sana biblia, Biblia inasema wazi “…na wana wenu waume kwa wakike watatabiri,wazee wenu wataota ndoto, na Vijana wenu wataona maono” Yoeli 2:28, na kama haitoshi Mungu alichagua viongozi vijana na wadogo kama Daudi, Gidion katika Waamuzi 6:15, Sauli katika Samweli 1&2, Pia Mussa alishindwa kufika nchi ya ahadi na Mungu akamchukua na nafasi yake akapewa kijana mdogo Joshua akawapeleka nchi ya ahadi wana Israeli sisemi kuwa wazee hawatufai la hasha bali hawawezi kutupeleka kwenye nchi ya maono, hawezi kutufikisha kwenye mafanikio kwa sababu wazee hawashauriki na hawakotayari kujifunza mambo mapya kwa sababu wanaamini na uzoefu wa kutosha na mbinu walizotumia kumng’oa mkololoni zinaweza kuung’oa umaskini na hali ya nhi ilivyo sasa. Hapa mimi simzungumzii mzee yule aliyehasi imani yake kwa starehe za dunia na kuisaliti nafsi yake kwa sababu ya uroho wa madaraka wala mzee wetu anayepita makanisani na msikitini kutukumbusha vijana tumtumikie Mungu, hakika mzee wangu anafanya kazi iliyo njema kama biblia inavyoelekeza kuwa wazee watawafundisha na kuwashauri vijana wao jinsi ya kuongoza na kuenenda katika njia iliyo safi na bora, naamini kabisa taji hiyo imewekwa kwa ajili yako na ningependa siku uwaambie waziwazi kuwa kuchangisha au kuchangia katika kazi ya Mungu ni wajibu wetu wote hasa vijana na wala haufanyi hivyo kwa sababu unaota kugombea urais bali unatuandaa vijana tuwe na tuone maono bora zaidi.
Pia ningependa kutoa rai kuwa vijana kwa umoja wetu tujaribu kuitumikia jamii yetu kwa nafasi mbalimbali na zaidi tusiache kuwatia moyo vijana mwenzetu ambao wanaona maono ya kuwa viongozi halikadhalika kuwaambia kijana mwenzangu unaweza kuwa kiongozi kwa nafasi hii, kama nami ninavyomshauri kijana mwenzangu, kaka yangu January Makamba boresha maono yako zaidi na zaidi uiponye nchi, uwe rais wetu 2015. January Makamba gombea Urais 2015

JANUARY MAKAMBA NI KIJANA PEKEE KWA SASA ANAYEWEZA KUIPONYA NCHI YETU:

Nawasilisha

Mataifa Makubwa kama Marekani na afrika ya kusini wanatambua uwezo wake.vijana tuache kutumika na hawa wazee wa poda.
 
Wana jf wote j makamba ataweza timiza ndoto za walio wengi kwa sasa nchii hii inahitaji rahisi kijana mwenye kuthubutu na makamba ni mmoja wapo
 
Vijana tunahitaji kuwa critical na sio kurush tu kimaamuz. Binafsi naona ukimtoa Makamba January nani mwingine anayeweza kutuokoa vijana? tumetengwa katika nyanja zote kwa sababu uongozi wa vipindi vyote ulikuwa wa wazee na waliwajali wazee wenzao. so tusipochukua hatua mapema na kukubali kwamba 2015 ni mda wetu sasa tutabakia kuwa "TAIFA LA KESHO NA KESHOKUTWA". wazee hawaoni tabu ya ajira na tabu tunazopata mtaani na ndio maana hata kustaafu kwao wanaona ni ndoto. ni mda wa kushtuka na kuchukua hatua 2015 VIJANA KWANZA!!!!
 
January makamba ana mke wa watoto but slaa ana hawara mpaka leo sasa nani anaweza kuongoza familia!!!

Mtoto wa nyoka ni nyoka tu; January ni mtoto wa Yusuf Makamba aliyekuwa kiongozi wa chama cha ccm kwa muda mrefu na sifa yake kubwa ilikuwa ni kula rushwa kwa wahindi na hivyo hivyo mwanae hana tofauti kwani ubunge wake ulifadhiliwa na mafisadi!!! Urais anautamani lakini hauwezi!!!
 
...all i can say is rubish on board...
 
mtoto wa nyoka ni nyoka tu; january ni mtoto wa yusuf makamba aliyekuwa kiongozi wa chama cha ccm kwa muda mrefu na sifa yake kubwa ilikuwa ni kula rushwa kwa wahindi na hivyo hivyo mwanae hana tofauti kwani ubunge wake ulifadhiliwa na mafisadi!!! Urais anautamani lakini hauwezi!!!

hapo mkuu umekalilishwa na misemo ya kidunia rudi kwenye ukweli makamba ni hazina kubwa kwa sector ya uongozi kwa ni ni kijana pekee mwenye kujua maisha halis ya mtanzania na sio fisad
 
Ndugu wana jamvi wa Jf, leo nami nimeona niwasilishe sehemu ya mawazo na uhalisia wa mambo yalivyo katika maisha yetu kwa sasa. Nikiwa sehemu ya kundi kubwa (VIJANA) lenye maamuzi na hatma ya taifa letu na maisha ya baadae.
Ni hakika tumeshuhudia na kuona matukio makubwa na historia nyingi ndani ya nchi zikitokea, mfano kujiuzuru kwa aliyekuwa waziri mkuu,Richmond, EPA, Dowans, Kikombe cha babu, Umeme wa mgao, Ujio wa rais Obama, Katiba Mpya n.k lakini mimi nimeguswa zaidi na historia zilizowekwa na itakayowekwa hivi punde na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeshuhudia miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika na punde tu tumetoka kushuhudia maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, ndani ya miaka 50 ni mengi mazuri na mema serikali imejitahidi kufanya kwa wananchi wake kutokana viongozi walioshika madaraka. Lakini historia kubwa ninayoiwaza mimi ni ile tunayoenda kuifikia ya kutimiza miaka 50 ya MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzabar, miaka 50 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 26/04/2014 sitaki kuzungumzia Muungano kwa kuwa nimeshatoa maoni yangu kwenye tume ya rasimu ya katiba mpya bali nataka vijana kwa pamoja tukiweka mbali maslahi ya vyama, ukabila,udini, ukanda na maslahi binafsi. Tujadili na tujiandae kisaikolojia hususan kuhusu kiongozi wa nchi, mkuu wan chi, rais mteule ajaye tutakuwa hatuna tofauti na wazee ambao fungu lao ni kuota ndoto (malengo mafupi) kama tukisema tusubiri hadi vyama vitangaze nani atagombea bali tutakuwa tunajidhihirisha kuwa sisi ni vijana wenye maono (malengo na mitazamo yote ya muda mfupi na mrefu) kwa kuanza kujadili mustabali wa maisha yetu ya baadae sasa. Ukweli ni kwamba maisha ni magumu na yanachangamoto nyingi sana hasa kwa sisi vijana, maisha yamekuwa ghali sana, umeme juu, ajira finyu na chache nk lakini kitu kizuri ni kwamba tunaweza kubadili hii hali ingawaje nchi yetu ni changa kwenye viwanda na teknolojia lakini ili limechangawia na kuwa na viongozi wanaoota ndoto ni dhahiri tunahitaji kupata mtu mwenye maono ili aiponye nchi yetu yenye kila aina ya rasilimali, tunahitaji kumpa kijana atakayeweza kutuunganisha na kutumikisha sehemu ambayo tutaweza kunufaika na utajiri tulionao wa maliasili,madini,maji na vijana kama nguvu kazi, tunahitaji kumpata kijana wa jamii ya January Makamba atupeleke kwenye nchi yetu ya maono, Tunamwitaji January Makamba aiponye nchi na ukoma wa umaskini, ajira, na usimamizi uliobora wa rasilimali zetu.
Mimi ni mkristo hivyo usoma sana biblia, Biblia inasema wazi “…na wana wenu waume kwa wakike watatabiri,wazee wenu wataota ndoto, na Vijana wenu wataona maono” Yoeli 2:28, na kama haitoshi Mungu alichagua viongozi vijana na wadogo kama Daudi, Gidion katika Waamuzi 6:15, Sauli katika Samweli 1&2, Pia Mussa alishindwa kufika nchi ya ahadi na Mungu akamchukua na nafasi yake akapewa kijana mdogo Joshua akawapeleka nchi ya ahadi wana Israeli sisemi kuwa wazee hawatufai la hasha bali hawawezi kutupeleka kwenye nchi ya maono, hawezi kutufikisha kwenye mafanikio kwa sababu wazee hawashauriki na hawakotayari kujifunza mambo mapya kwa sababu wanaamini na uzoefu wa kutosha na mbinu walizotumia kumng’oa mkololoni zinaweza kuung’oa umaskini na hali ya nhi ilivyo sasa. Hapa mimi simzungumzii mzee yule aliyehasi imani yake kwa starehe za dunia na kuisaliti nafsi yake kwa sababu ya uroho wa madaraka wala mzee wetu anayepita makanisani na msikitini kutukumbusha vijana tumtumikie Mungu, hakika mzee wangu anafanya kazi iliyo njema kama biblia inavyoelekeza kuwa wazee watawafundisha na kuwashauri vijana wao jinsi ya kuongoza na kuenenda katika njia iliyo safi na bora, naamini kabisa taji hiyo imewekwa kwa ajili yako na ningependa siku uwaambie waziwazi kuwa kuchangisha au kuchangia katika kazi ya Mungu ni wajibu wetu wote hasa vijana na wala haufanyi hivyo kwa sababu unaota kugombea urais bali unatuandaa vijana tuwe na tuone maono bora zaidi.
Pia ningependa kutoa rai kuwa vijana kwa umoja wetu tujaribu kuitumikia jamii yetu kwa nafasi mbalimbali na zaidi tusiache kuwatia moyo vijana mwenzetu ambao wanaona maono ya kuwa viongozi halikadhalika kuwaambia kijana mwenzangu unaweza kuwa kiongozi kwa nafasi hii, kama nami ninavyomshauri kijana mwenzangu, kaka yangu January Makamba boresha maono yako zaidi na zaidi uiponye nchi, uwe rais wetu 2015. January Makamba gombea Urais 2015

JANUARY MAKAMBA NI KIJANA PEKEE KWA SASA ANAYEWEZA KUIPONYA NCHI YETU:

Nawasilisha

Hata aje February Makamba hatutaki mazoea.
 
Labda asubiri huyu rais wa wasafi amalize muda wake ndipo awe rais mpya! Ila kwa Taifa tukutu kama Tanzania tunahitaji mtu anayeifahamu Tanzania! Sio hawa vindaki ndaki wasiofahamu hata familia zao kwa undani..
 
ivi watu wanauchukuliaje uraisi jamani.....hadi watu type ya wakina january!!?????
 
Nimetuma post yangu mnipe status ya afya,elimu na miundombinu ya maji tu ya huko Bumbuli na taasisi alizoongoza mafanikio yake ili tumjue vizuri sijapata jibu mpaka sasa.
Wengine hatukuumbwa kumkubali mtu kiushabiki au kuhongwa tunataka facts mkuu.
 
Nenda kamwambie hata akichanjwa mpaka mdomo wa haja kubwa. akamezeshwa .akaifukishwa na akabebeshwa hirizi kibao. Mwisho wake ni hapo alipo.akipanda saana uwazi ha huo wa kishkaji na sio utendaji. Mjinga saana ulieleta mada hii.
 
Akili butu kabisa hizi.Yani kuwa karani wa rais tayari anafaa kuwa rais?akabane pua magogoni?
 
Oya mkuu naomba unijibu basi status ya elimu,afya na miundombinu ya maji Bumbuli na mafanikio kwenye taasisi alizoongoza huyu mtu

Ni muhimu kwanza ukaelewa majukumu ya Mbunge. Mbunge hajengi barabara, hajengi miundombinu ya maji, haajiri walimu wala hajengi maabara. Serikali ndio inapanga bajeti na kutekeleza mambo hayo. Mbunge anapodaiwa barabara kama Serikali haijapanga bajeti barabara hiyo haijengwi hata Mbunge Huyo awe malaika wa namna gani. Ndio maana Mnyika anapiga kelele kuhusu Maji Ubungo kila siku lakini hadi Leo Maji hakuna. Hata hivyo, Huyo jamaa kashinikiza mabadiliko makubwa sana Bumbuli. Na hii ni miaka mitatu tu ya Ubunge. Taasisi aliyoianzisha imeshakopesha Karibu milioni 350. Maandishi ya mitandaoni hayana maana. Ungekuwa umeenda kule kabla ya 2010 na sasa ungeona tofauti kubwa sana. Yule Bwana akiamua anaweza kuwa Mbunge wa maisha.
 
Unajua kaka kuna kitu kinaitwa baraza la madiwani ambalo upanga bajeti na matumizi ya halmashauri na makusanyo naye ni diwani kwahyo bado anajukumu la hivyo vitu nilivyovitaja,angalia mwenzake Kigwangala alichokifanya Nzega kwa kusimamia walichokubaliana kwenye baraza la madiwani ambapo madiwani walitaka kufanya usanii kwenye azimio hilo ila yeye aliungwa mkono na wananchi.
Mbunge ana jukumu kubwa kwenye maendeleo na maendeleo yanahusisha vitu nilivyovitaja nahitaji status yake jimboni mwake na hivyo vyote vipo chini ya baraza la madiwani na yeye mheshimiwa ni mmojawapo aingiaye kwenye hilo baraza.
 
yaani January baada y kupita kugawa wali kwa vijana wa vyuo vikuu ameshajiona ana nafasi ya kupewa urais kwa vile vijana wako wengi? na mshauri asije akategemea wale vijana aliowapa wali vyuoni wengi hawana kadi za kupigia kura na maboresho ya daftari la kudumu ndio hivyo chenga kama pale mbeya alikuwa nao mtenda waliokuja wengi ni first years baada ya kudanganywa kuwa ni part ya welcome first year na organisation haikufanyika vyema kwa kujua ni party hata walioorganize walichaguana kwa upendeleo

Mmmh,we jamaa kama una chuki tu au unalipwa kueneza chuki?
 
Back
Top Bottom