2015 vijana twendeni na january makamba kuwa rais

acer

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
1,595
Reaction score
142
Ndugu wana jamvi wa Jf, leo nami nimeona niwasilishe sehemu ya mawazo na uhalisia wa mambo yalivyo katika maisha yetu kwa sasa. Nikiwa sehemu ya kundi kubwa (VIJANA) lenye maamuzi na hatma ya taifa letu na maisha ya baadae.
Ni hakika tumeshuhudia na kuona matukio makubwa na historia nyingi ndani ya nchi zikitokea, mfano kujiuzuru kwa aliyekuwa waziri mkuu,Richmond, EPA, Dowans, Kikombe cha babu, Umeme wa mgao, Ujio wa rais Obama, Katiba Mpya n.k lakini mimi nimeguswa zaidi na historia zilizowekwa na itakayowekwa hivi punde na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeshuhudia miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika na punde tu tumetoka kushuhudia maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, ndani ya miaka 50 ni mengi mazuri na mema serikali imejitahidi kufanya kwa wananchi wake kutokana viongozi walioshika madaraka. Lakini historia kubwa ninayoiwaza mimi ni ile tunayoenda kuifikia ya kutimiza miaka 50 ya MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzabar, miaka 50 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 26/04/2014 sitaki kuzungumzia Muungano kwa kuwa nimeshatoa maoni yangu kwenye tume ya rasimu ya katiba mpya bali nataka vijana kwa pamoja tukiweka mbali maslahi ya vyama, ukabila,udini, ukanda na maslahi binafsi. Tujadili na tujiandae kisaikolojia hususan kuhusu kiongozi wa nchi, mkuu wan chi, rais mteule ajaye tutakuwa hatuna tofauti na wazee ambao fungu lao ni kuota ndoto (malengo mafupi) kama tukisema tusubiri hadi vyama vitangaze nani atagombea bali tutakuwa tunajidhihirisha kuwa sisi ni vijana wenye maono (malengo na mitazamo yote ya muda mfupi na mrefu) kwa kuanza kujadili mustabali wa maisha yetu ya baadae sasa. Ukweli ni kwamba maisha ni magumu na yanachangamoto nyingi sana hasa kwa sisi vijana, maisha yamekuwa ghali sana, umeme juu, ajira finyu na chache nk lakini kitu kizuri ni kwamba tunaweza kubadili hii hali ingawaje nchi yetu ni changa kwenye viwanda na teknolojia lakini ili limechangawia na kuwa na viongozi wanaoota ndoto ni dhahiri tunahitaji kupata mtu mwenye maono ili aiponye nchi yetu yenye kila aina ya rasilimali, tunahitaji kumpa kijana atakayeweza kutuunganisha na kutumikisha sehemu ambayo tutaweza kunufaika na utajiri tulionao wa maliasili,madini,maji na vijana kama nguvu kazi, tunahitaji kumpata kijana wa jamii ya January Makamba atupeleke kwenye nchi yetu ya maono, Tunamwitaji January Makamba aiponye nchi na ukoma wa umaskini, ajira, na usimamizi uliobora wa rasilimali zetu.
Mimi ni mkristo hivyo usoma sana biblia, Biblia inasema wazi “…na wana wenu waume kwa wakike watatabiri,wazee wenu wataota ndoto, na Vijana wenu wataona maono” Yoeli 2:28, na kama haitoshi Mungu alichagua viongozi vijana na wadogo kama Daudi, Gidion katika Waamuzi 6:15, Sauli katika Samweli 1&2, Pia Mussa alishindwa kufika nchi ya ahadi na Mungu akamchukua na nafasi yake akapewa kijana mdogo Joshua akawapeleka nchi ya ahadi wana Israeli sisemi kuwa wazee hawatufai la hasha bali hawawezi kutupeleka kwenye nchi ya maono, hawezi kutufikisha kwenye mafanikio kwa sababu wazee hawashauriki na hawakotayari kujifunza mambo mapya kwa sababu wanaamini na uzoefu wa kutosha na mbinu walizotumia kumng’oa mkololoni zinaweza kuung’oa umaskini na hali ya nhi ilivyo sasa. Hapa mimi simzungumzii mzee yule aliyehasi imani yake kwa starehe za dunia na kuisaliti nafsi yake kwa sababu ya uroho wa madaraka wala mzee wetu anayepita makanisani na msikitini kutukumbusha vijana tumtumikie Mungu, hakika mzee wangu anafanya kazi iliyo njema kama biblia inavyoelekeza kuwa wazee watawafundisha na kuwashauri vijana wao jinsi ya kuongoza na kuenenda katika njia iliyo safi na bora, naamini kabisa taji hiyo imewekwa kwa ajili yako na ningependa siku uwaambie waziwazi kuwa kuchangisha au kuchangia katika kazi ya Mungu ni wajibu wetu wote hasa vijana na wala haufanyi hivyo kwa sababu unaota kugombea urais bali unatuandaa vijana tuwe na tuone maono bora zaidi.
Pia ningependa kutoa rai kuwa vijana kwa umoja wetu tujaribu kuitumikia jamii yetu kwa nafasi mbalimbali na zaidi tusiache kuwatia moyo vijana mwenzetu ambao wanaona maono ya kuwa viongozi halikadhalika kuwaambia kijana mwenzangu unaweza kuwa kiongozi kwa nafasi hii, kama nami ninavyomshauri kijana mwenzangu, kaka yangu January Makamba boresha maono yako zaidi na zaidi uiponye nchi, uwe rais wetu 2015. January Makamba gombea Urais 2015

JANUARY MAKAMBA NI KIJANA PEKEE KWA SASA ANAYEWEZA KUIPONYA NCHI YETU:

Nawasilisha
 
Naona kuna style imeibuka ,,.,ili uonekane umetoa hoja basi unajaza pages!poor you
 
Naona unawaza kwa kutumia Didas Ma------ kama sio Tumbo,huyo January Makamba amefanya lipi la maana mpaka afikirie kugombea Uraisi?huo unaibu Waziri tuu umemshinda ndio ataweza Uraisi?kama amekutuma uje kupima Upepo mwambie hatupo,aende kwa Vijana wenzake wa UVCCM wakiongozwa na yule mchumia tumbo Mkuu,Makonda. Na napata shida nini litalikumba Taifa letu huko mbeleni kama Vijana tulionao ni type yako wewe mchumia tumbo. Shame on you.
 
ww mleta mada utakuwa ni januari,naona unajaribu kupima upepo wako hapa jamvini,ila ukweli hufai hata kuongoza familia yako sembuse kugombea urais

Tehe,tehe inawezekana na wewe unaota ndoto kama wazee mwenzako otherwise unalipwa tu
 
wazee wamekura maisha yao, wanakura maisha yetu na sasa wanataka kukopa maisha ya watoto wetu.2015 twendeni na kijana mwenzetu mzalendo January Makamba.
 
Naona unawaza kwa kutumia Didas Ma------ kama sio Tumbo,huyo January Makamba amefanya lipi la maana mpaka afikirie kugombea Uraisi?huo unaibu Waziri tuu umemshinda ndio ataweza Uraisi?kama amekutuma uje kupima Upepo mwambie hatupo,aende kwa Vijana wenzake wa UVCCM wakiongozwa na yule mchumia tumbo Mkuu,Makonda. Na napata shida nini litalikumba Taifa letu huko mbeleni kama Vijana tulionao ni type yako wewe mchumia tumbo. Shame on you.
Fahari ya kijana ni nguvu zake na akili zake, hulka ya matusi na kuenenda kwa hisia na miemko ni uzee tu huo,unahoji January kafanyaje mi nadhani ulitakiwa umpongezee kijana mwenzio kwa kazi njema na bora anazofanya,bdway huu si upepo ni ukweli wa mambo naomba umeze hivyohivyo japo ni chungu, wazee wakapumzike tu na wabaki wakitupa ushauri
 
2015 Lowasa Anatosha, January anafaa kuwa Rais, ila asubiri kidogo, zamu yake itafika tu.

Nchi hii inaugonjwa na haiwezi tibiwa na mgonjwa kama Lowasa tunahitaji vijana maana hawa wazee ndio waliotufikisha hapa tulipo.
 
Mi naona vicjy kamata atafaa sana ukizingatia kigezo cha ujana na kua ni mwanamke atapita bila kupingwa
wazee wamekura maisha yao, wanakura maisha yetu na sasa wanataka kukopa maisha ya watoto wetu.2015 twendeni na kijana mwenzetu mzalendo January Makamba.
 
2015 Lowasa Anatosha, January anafaa kuwa Rais, ila asubiri kidogo, zamu yake itafika tu.

Hapana ni zamu ya vijana,wazee wameshatuonesha njia ya kupita tunachohitaji ni busara zao na ushauri tu kwa sasa hata Mungu anasema hivyo
 
Mh! Yaleyale tunaona taasisi ya URAIS ni rahisi sana maana hata kuku aweza kuwa RAIS.Watanzania tuwe serious kwenye jambo hili tusiweke rehani nchi yetu.
 
Kafabya nn tumpongeze au kwa kuvaa suti na kuwakusanya bodaboda
Fahari ya kijana ni nguvu zake na akili zake, hulka ya matusi na kuenenda kwa hisia na miemko ni uzee tu huo,unahoji January kafanyaje mi nadhani ulitakiwa umpongezee kijana mwenzio kwa kazi njema na bora anazofanya,bdway huu si upepo ni ukweli wa mambo naomba umeze hivyohivyo japo ni chungu, wazee wakapumzike tu na wabaki wakitupa ushauri
 
Diamond rais wa wasafi nae tumuunge mkono jamani huyu kijana anaweza sana sana make ni rais wa wawasafi mnaoneje 2015 tukimpa magogoni????

Acha kuota ndoto kama wazee wewe
 
amekuahidi ukuu wa mkoa? hayo mawazo mfu hatuhitaji leo, january asubiri 2025, aonyeshe kwanza anafanya nn, hv ile bilioni alochukua kule barrick kwa kumuweka rehani dada yale alirudisha baada ya kunyimwa uwaziri wa nishati?
 
ww mleta mada utakuwa ni januari,naona unajaribu kupima upepo wako hapa jamvini,ila ukweli hufai hata kuongoza familia yako sembuse kugombea urais

January makamba ana mke wa watoto but slaa ana hawara mpaka leo sasa nani anaweza kuongoza familia!!!
 
amekuahidi ukuu wa mkoa? hayo mawazo mfu hatuhitaji leo, january asubiri 2025, aonyeshe kwanza anafanya nn, hv ile bilioni alochukua kule barrick kwa kumuweka rehani dada yale alirudisha baada ya kunyimwa uwaziri wa nishati?

kafanya mengi tu mbona unajitoa ufahamu lete hoja sio vihoja vya habari za udaku.
 
Back
Top Bottom