2015: Uchaguzi utakao ingia kwenye historia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2015: Uchaguzi utakao ingia kwenye historia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, May 25, 2012.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Habari zenu ndugu zangu. Ni muda mrefu sana sija post kitu wala kuanzisha thread humu ndani bali nimekua nikipitia tu maneno ya wengine. Wahenga walisema ni bora zaidi kusikiliza kuliko kuongea. Kwa leo nimeona nitupie senti mbili zangu kwenye hali ya kisiasa nchini hasa kuelekea 2015.

  Kwanza kabisa niseme nina amini kwa asilimia 100 kwamba 2015 ndiyo utakua uchaguzi muhimu kuliko yote katika historia ya Tanzania, hata kushinda ule wa 1995 ambao ndiyo ulikua uchaguzi wa kwanza kushirikisha vyama vingi. Pia niseme kwamba huu siyo utabiri wa kishehe Yahya bali ni jinsi tu ninavyo ona mambo yanavyo kwenda. 2015 bado ni mbali na tunayo yaona leo yanaweza yakawa tofauti ndani ya miaka mitatu. Sasa nitaje sababu za mimi kuhifikia hivi.

  1. Umaarufu ya upinzani na wapinzani:
  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Upinzani (haswa Chadema) umepiga hatua kubwa sana hii miaka saba. Ni nani ambae 2005 ange dhani kura za Kikwete zingine pungua toka asilimia themanini na kitu mpaka asilimia sitini na kitu? Ni nani 2005 angeamini leo hii Chadema ingekua na wabunge zaidi ya arobaini? Upinzani umekomaa Tanzania, vyama vya upinzani vimeanza kukua wakati CCM imekua ikizeeka.

  Zama za CCM kumsimamisha mgombea yoyote yule na kutegemea atashinda kwa sababu tu ni mwanaCCM zimepita. 2015 CCM lazima iwe makini ya watu watakao wapa dhamani ya kupeperusha bendera ya chama kuanzia ubunge mpaka uraisi. Wakidhani wanaweza mpachika yoyote na kumpromote kwa vile tu ni mwana CCM wataumia. Mfano vizuri ni uchaguzi uliopita ambao ulimpa kijana mdogo tena asiye na uzoefu wa kisiasa Nassari ushindi. Mbombea wa CCM kwenye uchaguzi huo alikua bwana Sioi na aliwekwa kwa vile tu ni mtoto wa marehemu mbunge mteule wa jimbo hilo na mkwe wa Lowasa.

  2. Viongozi wa CCM sasa wanaweza kosoana wenyewe kwa wenyewe:
  Japo bado kuna nidhamu ya woga, tumeona baadhi ya viongozi wa CCM ambao wapo tayari kutofautiana na chama chao kwenye maswla fulani. Mfano mzuri ni Bunge lililo pita na zile sign 75 alizo kusanya zito. Kipole pole nidhamu hii ya woga inapungua na tutarajie mengi zaidi huko mbeleni.

  3. CCM haitaki kukubali hali halisi:
  CCM bado haijakubali kuwa upepo unabadilika. Hakuna kitu kibaya kama mgonjwa kuogopa kwenda hospitali kwa kuhofia majibu. Matokeo yake ni kufuga ugonjwa mpaka unakuua. CCM is in DENIAL. Kama CCM inataka kujiokoa ikubali kuwa ina dalili ya maradhi, ikubali kujipima na kuanza kutafuta tiba mapema. Ikisubiri 2015 ugonjwa unaweza ukawa mbaya kiasi cha kuto kutibika.

  4. Wananchi wamebadilika:
  Sasa hivi Watanzania wameinuka. Japo mbali kuna safari ndefu ya Watanzania kuanza kujitambua na kutambua haki yao bado tunaona ongezeko la watu ambao sasa wanajua viongozi ni watumishi wao na si mabosi wao. Jinsi watanzania watakavyo endelea kutambua hili ndiyo itakapo zidi kuwawia vigumu CCM kutumia ubabe.

  5. Vyombo vya dola vinaundwa na walalahoi:
  Tumeona serikali mara kadhaa ikitumia nguvu ya dola kulinda utawala wake. Ila serikali inasahau kuwa asilimia kubwa ya vyombo hivi vinaundwa na wananchi walalahoi. Leo hii polisi wa kawaida anaetumwa kwenda kupiga wananchi wenzake hana tofauti ya kimaslahi wala kimaisha ya hao watu anaoenda kupiga. Itafika kipindi nacho hawa walalahoi wanaounda dola watachoka kuburuzwa na serikali. Je wakuu wa vyombo hivi wataingia wenyewe barabarani?


  Hali ya kisiasa Tanzania sasa hivi ni onyo kwa CCM na changamoto kwa upinzani. Tutaona mengi kuelekea 2015. Mwenyezi Mungu atujalie tu uzima na afya.
   
 2. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,103
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  safi sanaa kwa kuyaona haya... tuombe uzima tufike 2015 salamaaaaaaaaaa
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Nadhani itoshe kusema kwamba Alichotabiri DR SLAA kwamba akikaa nje ya Bunge na kupata fursa ya kukitumikia chama kwa kipindi chote 2010-2015 basi, kwenye uchaguzi wa 2015 ndio siasa itakuwa tamu.KIMEANZA KUTIMIA
   
 4. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu you have said it all, 2015 ni mwaka wa ushangao kwa wasiasa wa mazoea hasa wanaccm. Ni mwaka ambao watoto wa secondary za kata watapiga kura zilizojaa hasira ya maisha magumu yasiyo na matumaini na kuzilinda kwa nguvu zote. Ni mwaka wa uchaguzi ambao si polisi wala jeshi letu litakubali ghiriba za ccm badala yake litasimama imara kuwalinda wanyonge wa nchi yao.
   
 5. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Alikuambia nani?
  Au unaota tu!
   
 6. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Mkuu umesahau kusema kwamba 2015 rais wa kwanza kutoka upinzani atakuwa ni Dr. Slaa.
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Kuna mhindi mmoja karopoka kweli kule dodoma, eti ndani ya chadema hakuko salama. Watasoma namba awamu hii
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Pia kwa kukaa pembeni kwa Slaa kumeonyesha kuwa chama kina rasili mali ya vipaji vya kisiasa na si kwamba walikuwa wanategemea vichwa vichache tu. Slaa katoka nje ya bunge na nafasi yake imechukuliwa na watu kama Mnyika, Lissu, Mdee nk.
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mpenda demokrasia yoyote wa chama chochote kile lazima akubali upinzani wenye nguvu ni muhimu katika maendeleo ya siasa ya nchi yoyote ile. Pia mtu yoyote ambe anapenda ushindani (competitive) anataka ushindani mkubwa ili akishinda aweze kweli kutamba kwamba I was challenged and I beat the best possible competition.
   
 10. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante kwa thread ndefu. Ukiondoa makosa kibao ya kiuandishi, imejaa ujumbe murua. Nilikuwa kusema huko nyuma kwamba ccm ni sikio la kufa na sasa wengi mnaanza kuona bayana. Mungu tuwezeshe tuung'oe huu mbuyu unaoitwa ccm.
   
 11. S

  Soki JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu umechambua vizuri sana. Naomba tusaidiane kuhariri kidogo kazi yako!

  Hatusemi mtu 'yoyote' bali mtu 'yeyote'
   
 12. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Nilifikiri utasema, sio onyo ni hukumu imeishapitishwa tayari.
   
 13. S

  Soki JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu mbona sijakuelewa?
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  May 26, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mwanafalsa1 yaani kwa mara ya kwanza nimekupa like.....umefanya uchambuzi mwanana na mujarabu haswa....wewe unajua nini unaandika na kweli unaishi ukichambua historia ya mienendo ya siasa za nchi hii kwa umakini sana...mungu atupe uhai mrefu na 2015 tukutane kujadili haya tena...asante sana msalimie shemeji..
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  May 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hatuwapi uongozi wahuni - Nape.
   
 16. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #16
  May 26, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi ambao, ama kwa hakika wa ushindani mkubwa kutokana na wimbi la vijana kujiingiza kwenye siasa hasa kutokana na ukosefu mkubwa wa ajira ama ajira zenye ujira usiokidhi mahitaji, uchaguzi ambao ili uweze kuwa wa amani itahitajika busara ndogo tu ya IGP kutoa maneno mafupi yakurudisha imani ya raia kwa polisi.
   
 17. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #17
  May 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Asante sana mkuu kwa kunisahihisha. I appreciate.
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  May 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Polisi wenyewe wana njaa mkuu. Useme IGP atahitajika kuwa ambia vijana wake (polisi) wasiigeuke dola maana wao wenyewe wana njaa. Hata hao polisi ni raia na sehemu ya jamii.
   
 19. S

  Soki JF-Expert Member

  #19
  May 26, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sasa nimekupata Mkuu Sangarara! Kumbe ingawa umeninuku mimi lakini umejibu hoja ya Mwanafalsafa kutoka na maneno yake mwishoni.

  Tanzania yenye neema inawezekana. Inakuja kwa kasi. 2015 tunarajia Tunatazamia Nchi Mpya. Tumeonewa vya kutosha! tumefisidiwa vya kutosha!

  No one can hinder this!

  Jambo la muhimu tu ni wale walioko front line kuongoza jahazi hizi wawe makini kuliko wakati mwingine wowote, kudumisha umoja na mshikamano; na kutokumvumilia yeyote ambaye atakuwa ni pandizi la kuharibu na kuvuruga hii move.

  Kama mambo yakiendelea hivi na kuzidi kuboreka, 2015 CCM kwaheri ya kutokuonana!
   
Loading...