MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 849
Binafsi sina mapenzi na chama chochote cha upinzani. Na sifichi ukweli kwamba nime kuwa mpenzi wa CCM tokea udogo haswa kutokana na kumu idolize Nyerere. Ila pia naweka mapenzi ya nchi mbele ya mapenzi ya chama. Najua Tanzania ita nufaika sana na upinzani wenye nguvi na vyama vinavyo pokezana mara kwa mara. Najua fika kwamba mwaka huu uraisi unge takiwa uende kwa Slaa. Lakini sidhani kama hayo yata tokea mwaka huu.
Ndo maana ule ushauri wako feki uliokuwa unautoa hapa kwa wapinzani ulikuwa unapuuziwa.
Na hata huu tunaupuuzia pia,huyu Mwana FA ndo wale wanaotumiwa kutupotosha tusijadili namna ya kupata viongozi bora (kwa kuiondoa CCM Madarakani),anataka atuaminishe hivyo,anasubiri 2015 ikifika aseme "Tujipange 2020",Tumpuuzie na hii post yake na tu focus ni jins gani Dr.Slaa anaweza akaingia Madarakan na kutuletea Tanzania yenye Neema,Yenye kujali utwala wa sheria na kuwa na nia ya dhati ya kupambana na rushwa.
Angalau leo umekubali mwenyewe kuwa wewe ni mpenzi wa chama cha mafisadi ... last time uliambiwa hili ukaruka kimanga ... ohh .... msiniionee...ohh....mimi sina chama..
Come on, watu walishasoma maandishi yako muda mrefu tu wakayajua mapenzi yako kwa chama la kijani. Ndo maana ule ushauri wako feki uliokuwa unautoa hapa kwa wapinzani ulikuwa unapuuziwa.
Ama kweli siku ina masaa 24 ... umevumilia weeee kwenye closet (kibanda ndani ya chumba) lakini uzalendo umekushinda
You got it twisted. Kamwe sija wahi kuficha kwamba mimi siyo supporter wa chama chochote cha upinzani au kuficha kwamba CCM kimekua chama changu tokea utotoni. Ulicho niaccuse wewe safari uliyo pita ni kudai mimi ni mtetezi wa mafisadi na nakumbuka sana post zote za siku hizo.
mimi napiga mluzi tu hapa ..... hizi propaganda zako zinafaa sana kule redio uhuru.
Kumbukeni kuwa wakati mnajiandaa kujipanga kwa 2015 Rostum na vikaragosi wake tayari wamefanya maandalizi na wameanza kumulika 2020.
Na hata huu tunaupuuzia pia,huyu Mwana FA ndo wale wanaotumiwa kutupotosha tusijadili namna ya kupata viongozi bora (kwa kuiondoa CCM Madarakani),anataka atuaminishe hivyo,anasubiri 2015 ikifika aseme "Tujipange 2020",Tumpuuzie na hii post yake na tu focus ni jins gani Dr.Slaa anaweza akaingia Madarakan na kutuletea Tanzania yenye Neema,Yenye kujali utwala wa sheria na kuwa na nia ya dhati ya kupambana na rushwa.
You really do not know politics do you? Nadhani hii miaka yote umeishi chini ya pango. Dr. Slaa hata shinda kwa mawazo ya kiutopia. Kitu pekee kitakacho mletea ushindi ni watu kujua kwamba kazi si rahisi. Kujua kwamba tunabidi tujipange siyo tu kwa ajili ya leo bali pia kwa ajili ya kesho na kesho kutwa. Hivi umesahau Mrema 1995 pamoja na star power aliyo kuwa nayo nini kili tokea? Mkuu kila kitu katika maisha ni mipango. Kama hautaki kuniamini endelea na mawazo hayo na uchaguzi huu ukiisha nita kupm directly na kukuuliza wewe ulifanya nini kuhakikisha Dr. Slaa anashinda. Na kasoro zote ninazo jaribu kuzionyesha ili zirekebishwe kama zita mcost Dr. Slaa nita kuja kwako tena na kukuuliza tena mipango yako wewe ilienda vipi. I think you are taking this too lightly.
Nadhani wengi mnasahau kwamba kazi si mwaka huu tu. Slaa akifanikia na akashinda bado itabidi yeye na chama chake kiongoze serikali kwa miaka mitano. hamna anaye ongelea nini kifanyike baada ya ushindi kana kwamba kutoka kwa CCM tu ndiyo mwisho wa kazi. Wengi wenu mtasema tukazanie kuona kwanza ushindi wa upinzani lakini mimi ni mtu ninaye penda kuangalia mbele. Ni sawa sawa na kuomba visa ya kwenda kusoma ne bila kufikiria ada utailipaje. Mimi ni wale ambao siyo tu naangalia visa nitaipataje bali ada na mahitaji mengine nita yafanikishaje....kuangalia mbele.
Wengine kinachotupa taabu ni hii dhana ya kufikiri wengine wana lengo moja tu la kuing'oa CCM halafu labda ndio wakae kufikiria la kufanya. Hii dhana inatoka wapi mathalan tuseme Chadema wanakamata madaraka. Unataka kuniambia hawana sera, hawana ilani ya uchaguzi na huyo Dr. Slaa anayataka hayo madaraka bila kujua atayatumiaje. Kwa nini tusisubiri hata hiyo siku atakapozindua kampeni yake atakapotoa vision yake ya anapotaka aifikishe Tanzania.
Wote tunakubaliana kuwa Dr. Slaa ni mtu makini halafu hapo hapo tunamkejeli kuwa anakimbilia kuing'oa CCM bila kupanga atalipeleka wapi taifa. Bila shaka unasahau kuwa tatizo kubwa linalolikabili utawala wetu wa siku zote ni utendaji. Sera na mipango ya CCM zilizo kitabuni kwa mfano sidhani kama ni mbaya kiasi hicho ila tatizo ni uaminifu, utendaji, na uwajibikaji. Mwana CCM anaapa kuwa hatatoa wala kupokea rushwa lakini shuhudia hii vurugu mechi inyoendeshwa kwenye kura za maoni.
Hapana Mwanafalsafa hatuwezi kuvumilia miaka mitano mingine ya Kikwete, hatuwezi kuvumilia miaka mingine mitano ya CCM na hatuwezi kuendelea kuwakumbatia viongozi wabovu na utawala wa kisanii usioheshimu sheria.
Wakti ukiwa unasoma primary au sekondary uliwai kufikiria kurudi nyuma darasa moja ili uwe best student kama si wa shule wa wilaya au mkoa au taifa.?
Je unaweza kufikiria kuchukua uamuzi huu wa kumrudisha nyuma mwanao anayekuwa wa kumi darasani ili awe wa kwanza? Wht if ukimrudisha akaendelea kuwa wa kumi au akawa wa nane na si wa kwanza.?