Ukitazama mwenendo wa chaguzi nchini, Lyatonga ali drive uchaguzi 1995 hata kama alipoteza. Mwaka 2000 uchaguzi haukuwa na mvuto kwasababu Mkapa alionesha kutosha na upinzani haukuwa na nyota alyeibuka wala chama kilichokuwa na nguvu yakufanana na NCCR ya Mrema 1995 au kuzidi pamoja na mageuzi yote ya kidemokrasia.
Mwaka 2005 Jakaya Kikwete ali drive uchaguzi ule hasa kutokana na mwamko wa sera ya vijana na siasa za upinzani kuwa kwenye mageuzi ya ndani kimfumo, Utumizi mkubwa wa pesa na rushwa ya kisiasa kushamiri.
Mwaka 2010 Dr Slaa alifanikiwa ku drive uchaguzi katika mazingira magumu kwani alikuwa anashindana na rais anaetetea nafasi yake, tofauti na Lyatonga alivyoshindana 1995 ambapo Mkapa alikuwa mpya na hakujulikana, Slaa alivutia kwasababu alikuwa anatoka chama chenye agenda, cha vijana wengi waliopuuzwa na kudhalilishwa na ccm, Chama chake cha Chadema kilichonekana mbadala na yeye mwenyewe akitokea bungeni ambako alifanikiwa sana ktk agenda ya ufisadi hivyo alikuwa tishio kwa utawala wa kijana kikavu.
Mwaka 2015 naona mashaka ndani na nje ya ccm. Ndani ya ccm simwoni mgombea mwenye mvuto japo nusu ya ule wa JK wa 2005, wale wote wanaojipambanua kutaka kugombea ni wahanga wa uchafuzi ulioasisiwa 2005 wakati wa kumwingiza JK madarakani. Membe, Lowasa, Migiro, Shein, Sitta, Makamba, Tibaijuka, Sumaye, nk hawa wote wamejeruhiana mno, ni wachafu hawafai hata kusimama kwenye kundi la watu mia wakajinadi bila kutumia pesa,
Ukija kwenye upinzani kati ya wagombea wote vinara wa UKAWA bado mgombea mwenye nafuu ni Dr Slaa tu, Pamoja na kuporomoka kwa Slaa kutoka 2010 hadi 2015 bado ndio mtu sahihi ukilinganisha na Mh Mbowe au Mbatia au Lipumba kwasababu mbalimbali ambapo nitazichambua nipatapo wasaa,
Kwa upande wa cdm, Slaa angegombea uenyekiti na John Mnyika akawa katibu mkuu, Mbowe awe mwenyekiti bodi ya wadhamini. Itamsaidia Slaa kupumzika.
Mnyika ana bidii na uwezo wa kusimamia utendaji na anakijua chama vizuri, Pia itaondoa dhana ya uchaga na uchu wa madaraka. Slaa hana compromise na govt. Pia itaondoa dhana ya katiba ilibadilishwa ili mbowe aendelee. Kikubwa Dr Slaa akiwa juu serikali itakuwa na wakati mgumu sana. Mnyika pia atamsaidia management, Mh Mbowe kuwa mwenyekiti wa baraza la wadhamini bado atakuwa ni super threat kwa govt tofauti na watu wanavyofikiri.
Dr slaa alipaswa asiwe anafanya kazi operational za chama. Dr slaa anahitaji team ya watalamu wa siasa na uchumi kutoka vyuo vikuu ama wale ma expart, media na research institution pamoja na watu wenye uzoefu wa nchi kama kina Butiku, Salim, Mtei, Jenerali Ulimwengu nk.
Iwe team ya kama watu 5 ambao wanakutana kila wiki kumshauri na kumpa updates za nchi. Wamtengenezee agenda. Ahutubie kila mwezi kutoa mwelekeo wa nchi. Kazi za utendaji wa chama amwachie mnyika kama katibu mkuu. Wanachama na viongozi wakate rufaa kwake sio yeye akafukuze sasa wakate rufaa kwa nani au wamlilie nan?
Dr Slaa kwenye chama ni zaidi ya kiongozi. Ndio moyo wa chama kwasasa. Hajatengenezwa mwingine bado wakufikia yeye japo jopo la vijana wa kariba yake linaiva wakiongozwa na Lisu, Lema, Mnyika nk.
Chama kimewatengeneza watu kama mnyika na wengine ili wawe viongozi dhabiti wa kisiasa wanaoweza kusimama wenyewe
Chama cha CUF, Maalimu Seif na lipumba wangebaki bodi ya wadhamini. Chama kipate mawazo mapya hasa Bara lakini Seif aendelee kugombea kwakuwa hakuna mbadala wa Seif urais labda Jussa mwaka 2020 ikiwa ataendelea kutembea na kuishi katika mapito sahihi aishiyo leo kwa itikadi ya CUF.
NCCR baada ya uchaguzi mkuu 2010 kiifanya makosa kuto kuunda mkakati sahihi wa kukipeleka mbele, kilipaswa kujikita mikoa mitatu, kigoma, tabora na katavi kwani bado ni chama kidogo kwa rasilimali na maeneo hayo kina angalu wafuasi wengi.
Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA umeonyesha mtazamo chanya wenye turufu ya ukombozi, UKAWA Ikiwa namna hivi ilivyo miezi hii na ikawa na dhamira ya ukombozi wa nchi na kuamua kusimamia MGOMBEA urais mmoja, basi wagawane majimbo ili kudhibiti bunge.
Kati ya majimbo 189 bara, waamue NCCR iachiwe majimbo 20, CUF 20, na CDM 149. Kule zanz yale 50 CUF iachiwe yote.
Nccr ikipewa majimbo 20 haitashinda zaidi ya 10. Na 10 itakuwa kujazia ruzuku. CUF bara hawezi kushinda zaidi ya 5 na 15 itakuwa ruzuku. CDM haiwezi kushinda zaidi ya 70. Mengine itakuwa ruzuku. Na zanz kati ya 50, CUF inaweza kushinda 25. Hivyo jumla UKAWA itakuwa imeshinda( 25+5), 70, na 10. Jumla 110 Kati ya majimbo 239.
Halafu ACT kama ni (chama kweli) ikijipambanua na agenda na ikacha siasa za kutumika kuidhoofisha CDM inaweza kushinda hata majimbo 15 wakiwa sereous kwasababu wanayo nafasi ya kuvizidi nccr na cuf. Na hawa UDP na TLP wakapata jumla 2.
Upinzani kwa ujumla itakuwa na viti 127 kati ya 139. Hii ni zaidi ya nusu, Na hivyo serikali itabidi iwe ya mseto UKAWA, CCM NA ACT.
HUYU ACT ATAAMUA NANI WAUNDE SERIKALI KATI YA CCM AU UKAWA lakini kutokana na pressure ya Umma kutaka mabadiliko, ACT HAITAWEZA KUUNGANA NA CCM. ITAKUWA KAMA ILIVOTOKEA UK LAST ELECTION
Liberaldemocratic ilikuwa 3rd force lakn mwamuzi. Ingawa kiitikadi inafanana na labor lakini ililazimika kuungana na Conservative ambayo kinyume chake kabisa policy wise na Ndivyo Labor ilivotoka.
Hivyo hitimisho ni kwamba 2015 nchi haina mgombea kutoka chama Tawala, Wote ni majeruhi ndani na nje ya upinzani wafanye haya.