Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Wazo la Leo (kutoka lililopita). Sifa za huyu mtu ambaye tunataka aje na kuwa Rais wetu na nyuma yake safu nzima ya viongozi wenye uwezi nilisema ni lazima ajitofautishe kwenye mambo kadhaa. Lakini kabla hatujaangalia haya naomba niangalia sifa moja ambayo niliidokeza mara ya mwisho - MTU WA WATU.
Kwa bahati mbaya maana ya "mtu wa watu" kwa baadhi ya watu wanafikiria ni mtu "maarufu kwa watu" au "anayependwa na watu". Maana ya kuwa "mtu wa watu" ni zaidi ya hivyol. Ninapuzungumzia ni "mtu wa watu" nina mambo matatu kichwani.
a. Anayetokana na Watu: Kiongozi huyo siyo anayejipachika au kupachikwa kwa watu. Bali watu (wananchi) wanamtambua uwezo wake, vipaji vyake na ni wao ndio wanamsukuma kuwatumikia. Na yeye akitambua uzito wa utumishi huo anasita. Anasita si kwa sababu hana uwezo au nia ya kuwatumikia la hasha! Anasita kwa sababu anatambua uzito (the gravity) ya wito wa kuwatumikia watu. Kwa hiyo anakuwa ni 'the reluctant hero'. Lakini anaposhawishiwa na wananchi wake na baadaye anakubali kuwatumikia basi huyo anakuwa ni kiongozi wa 'watu'.
b. Anayeongozwa na utu wa watu wake: Mojawapo ya mambo ambayo yanatusumbua sana kwa viongozi wetu ni suala la kuangalia vitu na si utu wa watu. Tunaangalia nani ni 'mwenzetu' kwa misingi ya urafiki, udugu, udini, ukabila na hata uchama. Kiongozi wetu ajaye ni lazima awe juu ya hivi vinavyotutofautisha bali aongozwe na kitu kimoja kinachotuunganisha wote - utu wetu. Hatutaki wala kustahili kiongozi anayeongozwa na "uenzetu huu" unaoangalia dini, kabila, rangi, hali ya maisha, elimu au ujiko wa kisiasa. Mtu wa watu ni yule anayejali UTU WA WATU wote.
c. Anayewejabika kwa watu: Sasa kiongozi ajaye si yule ambaye anatoka kwa watu au anaongozwa na utu wa watu wote bali zaidi ni yule anayewajibikwa kwa wananchi wake. Hatutaki kiongozi au Rais ambaye anajiona au kujifikiria kuwa ni "juu" ya wananchi. Mojawapo ya matatizo makubwa ambayo tunayaona (angalau kwa watu wenye msimamo wangu) ni kuwa viongozi wengi wanajiona ni "juu" ya wananchi kiasi kwamba wamekuwa na mawazo ya kikoloni. Yaani, wako pale kuwafanyia watu vitu - wasiulizwe, wasipingwe, wasihojiwe na wala wasiwajibishwe na wananchi wao. Wakati wakoloni walikuwa wanajali zaidi kuwajibishwa na "Ofisi ya Makoloni" kule Uingereza watawala wetu wa sasa wanajali sana kuwajibishwa na "vyama vya siasa". Wanaogopa zaidi vyama vyao kuliko wananchi wanaowatumikia! Isipokuwa wakati wa uchaguzi tu!
Tunataka kiongozi ambaye anatambua na kukubali kuwa yeye ni mtumishi wa wananchi. Na kutokana na utumishi huo basi wananchi kwake ni watu wa juu kuwaheshimu, kuwatii na kukubali mamlaka yao. Leo hii wale waliowekwa kutawala juu yetu wanawachukulia wananchi kwa dharau iliyoki(utter contempt). Hawanyenyekei mbele ya wananchi, wanajiaminisha kuwa wao 'ni bora' na wanastahili kuwepo pale. Matokeo yake wamekuwa wakifanya lolote, vyovyote, na kwa lolote. Hatutaki viongozi kama hao.
Tunaposema "mtu wa watu" hatumaanishi mwenye sura nzuri au tabasam zuri; hatumaanishi mwenye kujichekelesha, kucheka, kucheka cheka na kuchekewa au kuchekelewa na watu. Na kwa hakika tunaposema "mtu wa watu" hatumaanishi yule mwenye kugongewa, kupongezwa au kushangiliwa na watu. Bali yule ambaye anatoka kwa watu, anajali utu wa watu wote na anatambua kuwa anawajibika kwa watu huku akiheshimu mahitaji, matamanio na mamlaka yao.
Huyu ndiye MTU WA WATU!
Lakini uwezo wa mtu tunayemtaka kuwa kiongozi unaweza kuoneshwa vipi?
Wazo hili litaendelea inshallah.