2015 hatuhitaji Rais Malaika lakini tuwe makini na watu aina hii.

T

TAI MWEKUNDU

Member
Joined
Jun 17, 2013
Messages
5
Likes
0
Points
0
Age
43
T

TAI MWEKUNDU

Member
Joined Jun 17, 2013
5 0 0
Mjadala wa Urais 2015 unazidi kushika kasi, japo baadhi ya wanasiasa na wapambe wao hawapendi hili lisemwe kwa sababu wanazozijua wao. Ni wazi kwamba wagombea wote watakaojitokeza kuomba nafasi hiyo ya juu zaidi watakuwa na mapungufu yao kama binadamu lakini kama Taifa linalohitaji kujikomboa kiuchumi, kijamii na kisiasa; ni vema tuwaepuke wote wenye sifa hizi ambazo kwa maoni yangu zinazidi kiwango cha mapungufu ya kibinadamu;

1. Wala rushwa: Hawa watahalalisha rushwa ili waweze kufaidi keki ya nchi yetu wao, marafiki zao, wapambe wao na familia zao. Nchi itazidi kudidimia katika lindi la umaskini. Kama wao watafanya madudu huko juu, walio chini pia wataiga. Wanyonge na maskini watazidi kutokomea kwenye tope hilo.

2. Mafisadi/ watuhumiwa wa ufisadi: Hawa wataifisadi nchi na wote waliomo. Namaanisha nchi itazidi kuuzwa na vyote vilivyomo ikiwa ni pamoja na wananchi. Wataingia kwenye mikataba ya kifisadi ili mradi wao wananufaika binafsi. Hapa tutashuhudia maandamano kila kona ya nchi. si wanachuo, Madaktari, walimu, bodaboda nk.

3. Wanaotumia udini na ukabila: Hawa wanaweza kusababisha machafuko nchini.

4. wenye visasi: Watapanda mbegu ya chuki na visasi miongoni mwa watanzania.

5. Wanafiki/ Wasanii: wazuri wa kuongea na kupanga mikakati mitamu na mizuri kusikia lakini ndani yake usanii mtupuu.

Wakuu, naomba mwenye mchango zaidi aongezee
 
mansakankanmusa

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Messages
4,193
Likes
662
Points
280
mansakankanmusa

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2010
4,193 662 280
umenena mkuu, mH Rais ajae

sifa yake kubwa akisimama hata kabla hajaongea watu wampe 100%

Raisi ajae hatakiwi aseme sana watu wenyewe watasema
1. si mwizi
2. mdini
3.ukanda
4.ukabila
5. atajali maskini
6. atakuwa na mtazamo uliompa nafasi mh kikwete namna ya kuvuna madini yetu na yatupe matunda ya wazi wazi
watanzania wote
7. Raisi mtoto wa mkulima asiejitamkia ukulima kama huyu wa sasa, na maneno yake hayanaga maana tena
8. rais anaeweza kujali watu wakulima, matumishi na watu wote
9. asiwe mwanamke
10.
 
mansakankanmusa

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Messages
4,193
Likes
662
Points
280
mansakankanmusa

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2010
4,193 662 280
asiwe mwanamke inamaana nyingi sana
 
segwanga

segwanga

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Messages
2,789
Likes
38
Points
145
Age
42
segwanga

segwanga

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2011
2,789 38 145
1. Asiwe mwanachama wa magamba
2. Asiwe na akili kama fastjet,kila kukicha safari
 
K

kingukitano

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Messages
1,971
Likes
2
Points
0
Age
39
K

kingukitano

JF-Expert Member
Joined Jul 18, 2011
1,971 2 0
Mjadala wa Urais 2015 unazidi kushika kasi, japo baadhi ya wanasiasa na wapambe wao hawapendi hili lisemwe kwa sababu wanazozijua wao. Ni wazi kwamba wagombea wote watakaojitokeza kuomba nafasi hiyo ya juu zaidi watakuwa na mapungufu yao kama binadamu lakini kama Taifa linalohitaji kujikomboa kiuchumi, kijamii na kisiasa; ni vema tuwaepuke wote wenye sifa hizi ambazo kwa maoni yangu zinazidi kiwango cha mapungufu ya kibinadamu;

1. Wala rushwa: Hawa watahalalisha rushwa ili waweze kufaidi keki ya nchi yetu wao, marafiki zao, wapambe wao na familia zao. Nchi itazidi kudidimia katika lindi la umaskini. Kama wao watafanya madudu huko juu, walio chini pia wataiga. Wanyonge na maskini watazidi kutokomea kwenye tope hilo.

2. Mafisadi/ watuhumiwa wa ufisadi: Hawa wataifisadi nchi na wote waliomo. Namaanisha nchi itazidi kuuzwa na vyote vilivyomo ikiwa ni pamoja na wananchi. Wataingia kwenye mikataba ya kifisadi ili mradi wao wananufaika binafsi. Hapa tutashuhudia maandamano kila kona ya nchi. si wanachuo, Madaktari, walimu, bodaboda nk.

3. Wanaotumia udini na ukabila: Hawa wanaweza kusababisha machafuko nchini.

4. wenye visasi: Watapanda mbegu ya chuki na visasi miongoni mwa watanzania.

5. Wanafiki/ Wasanii: wazuri wa kuongea na kupanga mikakati mitamu na mizuri kusikia lakini ndani yake usanii mtupuu.

Wakuu, naomba mwenye mchango zaidi aongezee
Asiyependa wake za watu
Anayeheshimu kazi za vyombo vya dola
Mzalendo mwenye kuthubutu
Asiyepanga njama kuua wanahabari
Chama chair kisiwe na mrengo wa kigaidi
 
Forum statistics

Threads 1,275,062
Members 490,894
Posts 30,531,839