2013 ni mwaka wa Mwema kuondoka!

2013 ni mwaka wa Mwema kuondoka!

Kwa kuongea nchi hii tumejaliwa,tuishukuru mitandao ya kijamii imesaidia watu kupunguza stress zao za maisha,maana michango mingine hapa hadi unashangaa.
 
POLE SANA IGP SAID MWEMA-CHADEMA WAKIANDAMana,UNALAUMIWA KWAMBA UNAWALEA SABABU NI WACHAGA WENZIO,UAMSHO WAKIPAMBA MOTO,UNALAUMIWA KUWA WANAPATA KIBURI SABABU NI WAISLAMU WENZAKO,CCM WAKIFANYA JAMBO LAO.

UNALAUMIWA KWAMBA UNAWAOGOPA NA WEWE NI KADA WAO,HATA PENYE JEMA LAKO AU PUNGUFU LAKO KAMA MWANADAMU ,UNAAMBIWA WEWE SHEMEJI WA KIKWETE, LAKINI WANAOKUFAHAMU WAMEKUWA WAKISEMA HUYO DADA WA KIKWETE HAMUISHI KINDOA YAPATA ZAIDI YA MIAKA 15 KIKWETE HAJAWA RAIS.

MAANA WEWE UNAYE MKE MWINGINE AMBAYE SII HUYO ANAYEHUSISHWA NA USHEMEJI WAKO NA JK,-NAWAZA KWA TAFAKARI YA SAUTI,-JE,MH.RAIS KIKWETE ALIKUTEUWA KUWA IGP ILI KUKUPA ZAWADI YA KUMUACHA KINDOA DADA YAKE???AU WANAOKUANDAMA SABABU YA WEWE KUWA IGP KUWA ETI NI SABABU YA USHEMEJI NA KUACHA SIFA ZAKO WANA HOJA GANI!!!!

MAANA ULIPOTEULIWA WASIFU WAKO ULIJIELEZA,wewe ni Mwanasheria kwa Taaluma ,kazi za Polisi ulianzia BENKI kuu kitengo cha frauding,UKAWA afisa wa UPELELEZI katika ngazi mbalimbali ,WILAYA hadi MKOA,kamanda wa Polisi MKOA,na baadae ukaenda Polisi Interpol,Huko Kote USHEMEJI hatukuusikia WALA kuuona.

Magazeti Haya Haya ya Tanzania WADAU watakumbuka,na baadhi ya Waandishi wamo humu Jf,watanisahihisha Kama nakosea,ndio mwanzo yaliyo kupamba na hata kuanzisha tabiri za wewe KUJA kuwa IGP baada ya MAHITA ,hakuna mahala tabiri za magazeti zilihusianisha Bashiri au tabiri za uteuzi wako na USHEMEJI kwa JK,Bali tuliandikiwa mazuri yako,tukaambiwa kazi nzuri uliyoifanya ukiwa RPC MBEYA.

kazi nzuri uliyoifanya ukiwa afisa UPELELEZI maeneneo mbalimbali nchini,uwezo wako,na hata namna ambavyo UMEFANYA kazi nzuri ukiwa Interpol,walichambuliwa WENGI kumrithi MAHITA,NTOBI,TIBAIGANA,MSIKA,CHIKO,TOSI,KOVA,NA WENGINEO WENGI.

LAKINI WEWE RAMLI ZA WAANDISHI ZIKATUAMINISHA KWAMBA KWA UWEZO WAKO UTAPATA NAFASI YA KUTEULIWA KUWA IGP,HAKIKA NAPATA TABU,LEO WATU TUNAPOTAFUTA SPACE YA USHEMEJI KUMJADILI SAID MWEMA,AMA KWA MAZURI,AU KWA MABAYA,TUTENDEANE HAKI KATIKA KUJADILI,KUMUHUSISHA MTU ATI ANAFANYA JAMBO FULANI SABABU YA USHEMEJI,UDINI,UKABILA,AU ITIKADI FULANI SII JAMBO LA FAHARI.

TUMKATAE MWEMA KWA HOJA,NA TUMPENDE KWA HOJA,ITATUSAIDIA KUJENGA TAIFA LENYE AFYA YA WATU WANAOJADILI ISSUES NA SII OPINION.
 
.....[/QUOTE]
Hoja ya ushemeji haina mashiko, kwani kuachia askari wake wapokee rushwa inahusiana na ushemeji? Kuachia askari wake wavute bangi inahusiana na ushemeji?

Kuachia askari wake wawe majambazi inahusiana na ushemeji? Kuachia askari wake kuwabambikizia wananchi kesi inahusiana na ushemeji?

Mwema inawezekana ali-shine sana alipokuwa nafasi za chini na alikuwa mtendaji mzuri, lakini baada ya kupewa cheo kikubwa ndio kime expose udhaifu na uwezo wake mdogo wa kuongoza.

Ameshindwa kudhibiti nidhamu, kashindwa kuimarisha utendaji kazi wa polisi maana hawana ufanisi wowote, kashindwa kuwaongezea mishahara askari na kuwalipa posho na stahili zao kwa wakati, kashindwa kila kitu.

Kidogo ameweza kujenga makazi ya askari kwa baadhi ya mikoa.
 
Amekosa kigezo gani cha KJ huyo Simon?.....

Qualification no 1 ya kuwa IGP unatakiwa uwe kada wa CCM wa viwango vya Wassira, Nape au Lameck Mkumbo aka Mwigulu Nchemba!!!

Je, miongoni mwa polisi wetù nani ni mkereketwa wa CCM wa hao niliowataja hapo juu ili JK amteue kuwa IGP wa kumrithi Mwe.
 
QF Mtakumbuka kuwa mwaka 2006 wakati rais anamteua inspkta jenerali Mwema na WASIFU wake kutolewa mojawapo ya sifa muhimu tunayokumbuka ni kuwa alizaliwa mwaka 1953 Mkoani Kilimanjaro. Kwa msingi huo 2013 anatimiza miaka 60 ambao anatakiwa kustaafu kwa mujibu wa Sheria. Hivyo kwa jinsi JESHI la polisi lilivyovurunda kipindi chake na has a mwaka Jana Hana uhalali Wa kumbembeleza rais amwongezee walau mkataba wamalize nae 2015. Itakuwa ni kipindi kingine cha mauaji ya raia wasio na hatia. Kumbukumbu zinaonyesha hata kova na kamuhanda wanaondoka nae. Tuwatakie KILA la kheri na tuwakaribishe uraiani ingawa wanazongwa na damu za watu wasio na hatia
Waje uraiani tuwalipizie kisasi kama Barlow aliyetangulia kuwaandalia makao
 
Natarajia ndani ya Katiba mpya kutatengenezwa utaratibu bora jinsi ya kupata wakuu wa vyombo vya mashitaka,uchunguzi,upelelezi,ulinzi na usalama.
 
SAIDI MWEMA ANAFUGA UJAMBAZI KAMA ILIVYOKUWA KWA MAHITA,HIVI SASA VIJANA WENGI HAPA MOSHI WAKIWAMO MATAPERI KINA KIPARA,CALVIN NA WENGI WENGINEO AMBAO WANAFAHAMIKA KWA POLISI WANAMILIKI BASTOLA KAMA PIPI,WANAZITUMIA KUFYATUA RISASI MKESHA WA MWAKA MPYA NA KUTISHIA WATU HUKU MJINI NA UKIWAONA HAWANA SHUGHULI ZOZOTE ZAIDI YA KUZUNGUKA NA MAGARI HAPA MJINI KWA SABABU ANAYEWATENGENEZEA UPATIKANAJI WA SILAHA NI KIJANA WA SAIDI MWEMA ALIYEPO HAPA MOSHI.

SAIDI MWEMA NDIYE ALIYEJIPA TENDA YA KULISHA MIKATE MAKURUTA PALE CCP KAMA ILIVYOKUWA KWA MAHITA,KWA HIYO AKITOKA LEO HIYO TENDA YA CCP ATAIKOSA MAANA NI SERA KILA IGP ANAYEINGIA MADARAKANI ANAJIPA TENDA CCP AU CHUO KINGINE PALE DAR,HATUTASHNGAA NA SIRO NAYE AKIINGIA KWENYE HIYO NAFASI ANAFUATA SERA YA CHUKUA CHAKO MAPEMA(ccm),HAKUNA ALIYEMSAFI.
 
Back
Top Bottom