Jeshi la Kenya dhidi ya M23: Je, Kenya itaweza kufanya kile ilichofanya Tanzania mwaka 2013?

6 Pack

JF-Expert Member
Apr 17, 2022
1,823
4,073
Inakuaje brothers and sisters,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Leo ndio siku ya mwisho waliopewa waasi wa Congo ili kusalimisha silaha zao kwa serikali, kinyume na hapo hatua kali za kijeshi zitachukuliwa kwa kundi lolote la waasi ambalo limekaidi amri hiyo. Na oparation hiyo itahusisha majeshi ya Afrika mashariki kutoka Burundi, Congo, Uganda na Kenya huku Kenya ikionekana kuongoza oparation hiyo ambayo kundi kuu la waasi nchini Congo la M23 likisema kwamba haliitambui oparation hiyo na kwamba yeyote atakaethubutu kwenda kuwachokoza katika maeneo yao wata deal nae.

Tusisahau kwamba mwaka 2013 nchi za Malawi, South Africa zikiongozwa na jeshi la Tanzania ambalo lilisimamia oparation zote za chini ziliweza kulisambaratisha kundi hilo la M23 katika kipindi kifupi cha week kadhaa tu, na kusababisha waasi hao kukimbia ng'ome zao na kuacha silaha zao na kwenda kuomba hifadhi katika nchi jirani za Rwanda na Uganda.

Sasa baada ya miaka 9 ya ile oparation kabambe iliyoongozwa na Tanzania, leo waasi hao wamerudi tena kwa kasi ile ile huku Kenya ikionekana kutaka kuchukua nafasi ya Tanzania ili kurudisha tena amani katika maeneo hayo ya mashariki mwa Congo.

Sasa tukiachana na hizi nchi zingine zilizoshiriki au zinazoshiriki katika oparation hizo kama vile SA, Malawi, Burundi na Uganda.

Swali langu je Kenya itaweza kufanya kile ilichofanya Tanzania?

Au jeshi lake linakwenda kupokea kichapo kile inachopokea serikali ya Congo?

Lets wait to see what's gonna happen. Maana yamebakia masaa matano tu ule muda waliyopewa waasi uishe.

God bless Congo,
God bless Tanzania,
God bless our continent Africa.

Thank you 🙏
 
Vijana wa drc 3000 ndio wanakwenda kupigana nchi zingine kazi yake ni kutoa instructions
Vita itakapoanza ipo haja suala la m23 watakapokimbila, Nchi waliyokimbilia ikishindwa kutoa ushirikiano nayo ichapwe tu.
M23 sio wepesi kama unavyofikiria. Hao vijana 3000 nafikiri wataelekezwa wakapambane na yale makundi ya wahutu waliokimbia Rwanda. Ila kwa M23 hakuna kijana atakaekuwa tayari kuweka pua yake mbele yao.
 
Vijana wa drc 3000 ndio wanakwenda kupigana nchi zingine kazi yake ni kutoa instructions
Vita itakapoanza ipo haja suala la m23 watakapokimbila, Nchi waliyokimbilia ikishindwa kutoa ushirikiano nayo ichapwe tu.
Hao vijana hawana uwezo hata wa kuchinja kuku, wataweza kusimamisha vifua vyao mbele ya M23 kweli? Lets be honestly!
 
Gen. Muhozi ana support M23 so Uganda army watakuwa wanatoa siri kwa M23 na kufanya kazi kuwa ngumu
Serikali ya Congo ilikakaa kushirikiana na Rwanda, lakini imekubali kushirikiana na Uganda. Sasa sijui Tshisekedi hajui kuwa Rwanda na Uganda ni kama vile Tanganyika na Zanzibar kwamba ni nchi moja tofauti kila upande ina mtawala wake.
 
Labda Tz ingepewa hilo jukumu.
Tanzania tumeshafanya kazi kubwa ya kuzikomboa nchi nyingi za kusini.

Pia tulienda Congo tukafanya oparation ya muda mfupi ambayo ilileta matokeo mazuri kwa jeshi letu.

Sasa ni muda wa kuwaachia na wengine nao wafanye yale tuliyoyafanya, ikishindikana dakika za mwisho watatuita tukasafishe pori.
 
Back
Top Bottom