2013 CCM itakuwa na mgawanyiko

2013 CCM itakuwa na mgawanyiko

JUST

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2010
Posts
552
Reaction score
236
Ndugu Wana JF,

Kwa hali ya upepo wa kisiasa unavyokwenda ndani ya CCM kuanzia Januari Mwaka huu wa 2013 ni wazi kuwa CCM sasa inaelekea kuanza kwa makundi mbali mbali yatakayofanya chama sikivu kirudi tena Dodoma na Kuvunja makundi kama wataweza kutokana na matamko yafuatayo.

GESI YA MTWARA NA MATAMKO:

Mbunge wa Mtwara Mjini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara na nk.:

wao wako tayari kupoteza nyazifa zao kwa kutokubali gesi kwenda Dar/Bagamoyo

Mwenyekiti CCM taifa, Makamu Mwenyekiti na Naibu waziri Mawasiliano, Waziri wa Nishati na Madini na nk.:

hawa wako tayari kutumia nafasi zao kushinikiza gesi kusafirishwa mapaka Dar/Bagamoyo

Kwa kuwa wanaobishana wote ni wanachama wa CCM ni wazi kuwa wapo wanaofuata matakwa ya wananchi na wengine wanaofuata matakwa ya Mkuu wa nchi hivyo basi hali hii italeta pande mbili la wafia wananchi na wafia mkuu wa nchi.

URAISI KWA TIKETI YA CCM 2015 NA MATAMKO

Salaamu za EL mwaka mpya kwa Watanzania:

salamu za maamuzi magumu zilizotolewa baada ya kikao cha EL na Shelukindo, Chenge, Mgeja na Serukamba, na baadae kufuatiwa na kauli ya uamuzi mgumu wa shelukindo wa kumpigania EL kumrithi JK ni kirusi kingine ambacho kinawaambia wanamtandao wa EL wachukue maamuzi magumu ya kuweka bayana ni nani wako nao wa kupeperusha bendera ya CCM 2015. kwa hali hii 2013 ni mwanzo wa mapande yatakayozaliwa CCM kwa wawania uraisi tena kwa vijembe vya hali ya juu.

yaliyoandikwa hapo juu ni mtazamo wangu kisiasa na mwenye kupinga au kusapoti kwa hoja au kukashifu, kutukana, kukejeli wote mnakaribishwa maana ndio demokrasia yenyewe.
 
Itakuwa imejitahidi sana kubaki mapande mawili kutoka kwenye mapande zaidi ya saba yaliyopo sasa!...........
 
hiyo ya mapende saba sikuwa na uthibitisho nayo ila haya mawili yamejidhihiri mwaka mpya wa 2013 mwezi januari
 
hivi gesi ina enda dar au bagamoyo?kwa sababu naona kadalili ka upotoshaji hapa.kuhusu kuhitilafiana; ukiona watu wanahitilafiana ujue wanafikiri na ukiona wanaendeana pamoja kwa kila kitu ujue mmoja au wote ni poyoyo
 
Kutakuwa na mgogoro kweli, lakini WATAUNGANISHWA na FEDHA za UFISADI wa mradi wa ujenzi wa bomba la gesi. Gharama za mradi pale wamepiga karibu mara mbili ya gharama halisi ili hela inayobaki wagawane. Kitu pekee kinachowaweka wa CCM pamoja ni FEDHA na RUSHWA na kwa kuwa kwenye gesi kuna vyote hivyo hakuna mwana CCM atakayegombana na wenzie. Labda wapishane kwenye mgao. Nape na kelele zake zote hataki miradi ya gesi iwe Mtwara na watanzania wapelekewe PRODUCTS za gesi kwa kuwa bila kujengwa bomba la gesi CCM haitapata mabilioni ya shilingi za KUWAUNGANISHA.

Anayebisha anitajie mwana CCM hata mmoja ambaye sio fisadi, kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa....
 
uko sahihi mtoa mada
katika kuongezea
kaburi la ccm kwa kanda ya kusini ni gesi
 
Betlhem, unayosema ni sahihi ila wanamtwara wao kwenye mabango yao walikataa gesi kwenda dar/bagamoyo sijui kwanini na mbunge wao wa CCM anawasapoti. inawezekana kuna jambo limefichika nyuma ya pazia labda gesi ikifika dar itapelekwa na bagamoyo
 
hivi gesi ina enda dar au bagamoyo?

Kote kote.
Dar ni kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme, majumbani na viwandani (tayari kuna viwanda kama Twiga Cement vinatumia gesi kama nishati). Kwa Bagamoyo, kuna Wachina wameshajenga viwanda tayari, wanahitaji gesi kama nishati ya kuendeshea mitambo yao, mbali na umeme. Viwanda hivi viko upande wa kushoto, kama unakwenda Bagamoyo ukitokea Dar, nadhani ni nyuma kidogo ya eneo linaloitwa Kiromo
 
asante kwa ujumbe mimi nilihisi kumbe data zipo
 
hili nalo neno.

CCM wanatamani sana makundi waliyonayo yatokezee pia kule Chadema ili iwe ngoma draw...ukijiuliza msingi wa makundi ni nini, jibu wala haliridhishi
 
Kote kote.
Dar ni kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme, majumbani na viwandani (tayari kuna viwanda kama Twiga Cement vinatumia gesi kama nishati). Kwa Bagamoyo, kuna Wachina wameshajenga viwanda tayari, wanahitaji gesi kama nishati ya kuendeshea mitambo yao, mbali na umeme. Viwanda hivi viko upande wa kushoto, kama unakwenda Bagamoyo ukitokea Dar, nadhani ni nyuma kidogo ya eneo linaloitwa Kiromo
ok! nimekupata.navifahamu hivyo viwanda.sasa mbona watu wanaongea kama inaenda bagamoyo nyumbani kwa kikwete?
 
Neno 'Nyumbani' nadhani lilmekaa 'kiuzawa' zaidi, kwa maana ya anakotoka Kikwete, na sio nyumbani kwake. Malalamiko ya wana wa Mtwara yana mantiki fulani, sio ya kupuuzwa kama Muhongo anavyotaka kutuaminisha! Kwa nini gas plant isijengwe Mtwara na umeme ukasafrishwa kuja Dar na maeneo mengine?
 
mtoa mada umenena vyema ila nahauri tusitegemee migogoro ndani ya ccm ndio iwatoe madarakani kama alivyosema mchangiaji mmoja nikweli watakorogana lkn shekeli zikiwekwa mezani wanasahau shida zao kwa muda na kuanza kuimba ccm oyee! Kuwe na mgogoro kusiwe na mgogoro tuhakikisheni ccm 2015 inakuwa chama pinzani.
 
Ndio maana watu wakiwa wazee sana sababu ya upweke hugeuka wachawi RIP to:

  1. KANU
  2. UNIP

You died gracely! CCM will die shamely!
 
Ndugu Wana JF,

Kwa hali ya upepo wa kisiasa unavyokwenda ndani ya CCM kuanzia Januari Mwaka huu wa 2013 ni wazi kuwa CCM sasa inaelekea kuanza kwa makundi mbali mbali yatakayofanya chama sikivu kirudi tena Dodoma na Kuvunja makundi kama wataweza kutokana na matamko yafuatayo.

GESI YA MTWARA NA MATAMKO:

Mbunge wa Mtwara Mjini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara na nk.:

wao wako tayari kupoteza nyazifa zao kwa kutokubali gesi kwenda Dar/Bagamoyo

Mwenyekiti CCM taifa, Makamu Mwenyekiti na Naibu waziri Mawasiliano, Waziri wa Nishati na Madini na nk.:

hawa wako tayari kutumia nafasi zao kushinikiza gesi kusafirishwa mapaka Dar/Bagamoyo

Kwa kuwa wanaobishana wote ni wanachama wa CCM ni wazi kuwa wapo wanaofuata matakwa ya wananchi na wengine wanaofuata matakwa ya Mkuu wa nchi hivyo basi hali hii italeta pande mbili la wafia wananchi na wafia mkuu wa nchi.

URAISI KWA TIKETI YA CCM 2015 NA MATAMKO

Salaamu za EL mwaka mpya kwa Watanzania:

salamu za maamuzi magumu zilizotolewa baada ya kikao cha EL na Shelukindo, Chenge, Mgeja na Serukamba, na baadae kufuatiwa na kauli ya uamuzi mgumu wa shelukindo wa kumpigania EL kumrithi JK ni kirusi kingine ambacho kinawaambia wanamtandao wa EL wachukue maamuzi magumu ya kuweka bayana ni nani wako nao wa kupeperusha bendera ya CCM 2015. kwa hali hii 2013 ni mwanzo wa mapande yatakayozaliwa CCM kwa wawania uraisi tena kwa vijembe vya hali ya juu.

yaliyoandikwa hapo juu ni mtazamo wangu kisiasa na mwenye kupinga au kusapoti kwa hoja au kukashifu, kutukana, kukejeli wote mnakaribishwa maana ndio demokrasia yenyewe.
Umerithi mikoba ya sheikh Yahya?!
 
Umeona; walitaka kukiua CHADEMA sasa yamewageuka. Sawa tumeona mara nyingi migogoro ya CCM huwa inaisha kwa kutulizana na fedha wanazotuibia kwa kuwa wao ni chama tawala na hivyo kutumia nafasi hiyo vile wanavyotaka. Mimi napingana na anayesema wataendelea kutawala kwa mtindo huo. Mbona haya ya watu kutaka rasilimali wazifaidi pia wakazi wa maeneo husika na mambo mengine mengi ya watu kudai haki zao za msingi yanajitokeza sasa, kuliko wakati mwingine wowote? Hii inaonyesha wazi watu kuelimika na kuwa na uelewa wa kutosha juu ya yanayoendelea katika nchi yao. Kwa maana hiyo CCM wasitegemee mteremko 2015 kama walivyozoea kushinda kwa kura za mizengwe. Hii si nchi ya EL au Shelukindo nk.
 
ungeanza kumwambia wasira ambaye alitamka bila kudadavua. mtabiri hadadavui
 
Umeona; walitaka kukiua CHADEMA sasa yamewageuka. Sawa tumeona mara nyingi migogoro ya CCM huwa inaisha kwa kutulizana na fedha wanazotuibia kwa kuwa wao ni chama tawala na hivyo kutumia nafasi hiyo vile wanavyotaka. Mimi napingana na anayesema wataendelea kutawala kwa mtindo huo. Mbona haya ya watu kutaka rasilimali wazifaidi pia wakazi wa maeneo husika na mambo mengine mengi ya watu kudai haki zao za msingi yanajitokeza sasa, kuliko wakati mwingine wowote? Hii inaonyesha wazi watu kuelimika na kuwa na uelewa wa kutosha juu ya yanayoendelea katika nchi yao. Kwa maana hiyo CCM wasitegemee mteremko 2015 kama walivyozoea kushinda kwa kura za mizengwe. Hii si nchi ya EL au Shelukindo nk.

yaliyotokea mtwara ni kielelezo tosha
 
hili nalo neno.

CCM wanatamani sana makundi waliyonayo yatokezee pia kule Chadema ili iwe ngoma draw...ukijiuliza msingi wa makundi ni nini, jibu wala haliridhishi

huu ni wakati wa mpasuko CCM kuliko kipindi kingine chochote
 
mtoa mada umenena vyema ila nahauri tusitegemee migogoro ndani ya ccm ndio iwatoe madarakani kama alivyosema mchangiaji mmoja nikweli watakorogana lkn shekeli zikiwekwa mezani wanasahau shida zao kwa muda na kuanza kuimba ccm oyee! Kuwe na mgogoro kusiwe na mgogoro tuhakikisheni ccm 2015 inakuwa chama pinzani.

migogoro ikitumiwa vizuri hudhoofisha chama na hata kukiua. unakumbuka migogoro ya NCCR? na wapi NCCR ya 1995 ilipo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom