Ndugu Wana JF,
Kwa hali ya upepo wa kisiasa unavyokwenda ndani ya CCM kuanzia Januari Mwaka huu wa 2013 ni wazi kuwa CCM sasa inaelekea kuanza kwa makundi mbali mbali yatakayofanya chama sikivu kirudi tena Dodoma na Kuvunja makundi kama wataweza kutokana na matamko yafuatayo.
GESI YA MTWARA NA MATAMKO:
Mbunge wa Mtwara Mjini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara na nk.:
wao wako tayari kupoteza nyazifa zao kwa kutokubali gesi kwenda Dar/Bagamoyo
Mwenyekiti CCM taifa, Makamu Mwenyekiti na Naibu waziri Mawasiliano, Waziri wa Nishati na Madini na nk.:
hawa wako tayari kutumia nafasi zao kushinikiza gesi kusafirishwa mapaka Dar/Bagamoyo
Kwa kuwa wanaobishana wote ni wanachama wa CCM ni wazi kuwa wapo wanaofuata matakwa ya wananchi na wengine wanaofuata matakwa ya Mkuu wa nchi hivyo basi hali hii italeta pande mbili la wafia wananchi na wafia mkuu wa nchi.
URAISI KWA TIKETI YA CCM 2015 NA MATAMKO
Salaamu za EL mwaka mpya kwa Watanzania:
salamu za maamuzi magumu zilizotolewa baada ya kikao cha EL na Shelukindo, Chenge, Mgeja na Serukamba, na baadae kufuatiwa na kauli ya uamuzi mgumu wa shelukindo wa kumpigania EL kumrithi JK ni kirusi kingine ambacho kinawaambia wanamtandao wa EL wachukue maamuzi magumu ya kuweka bayana ni nani wako nao wa kupeperusha bendera ya CCM 2015. kwa hali hii 2013 ni mwanzo wa mapande yatakayozaliwa CCM kwa wawania uraisi tena kwa vijembe vya hali ya juu.
yaliyoandikwa hapo juu ni mtazamo wangu kisiasa na mwenye kupinga au kusapoti kwa hoja au kukashifu, kutukana, kukejeli wote mnakaribishwa maana ndio demokrasia yenyewe.