Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakuu napingana na nyie mlio wengi - kiwango cha Ujerumani, Mexico, Urugway, Ghana, Brazil, Spain na Agentina ni kizuri sana. Mfano game ya jana kati ya Argentina na Mexico ilikuwa ya kiwango cha juu mno ni kati ya game nzuri so far.
Tutaona viwango safi hasa kwa hizi timu za America ya kusini wanacheza mpira wa kasi sana. angalia magoli ya jana lile moja na mexico na lile la mbali la Tevez - angalia movements wanapokuwa na mpira utapenda.
Still to come jamani - timu zilozotoka ndiyo zilikuwa zinadororesha mashindano haya zimeshatoka - timu kama uingereza jamani? hata kama wangepewa goli la Lampard lakini sijaona kitu wamefanya, kweli soka ya uingereza ina tatizo kubwa, something has to be done faster. kuna mdau amesema anamkosa Gaucho - mi nafikiri gaucho alikuwepo kwenye timu ya Mexico yule kijana machachari sana jina limenitoka ila wadau mtamkumbuka tu ana kasi mjanja sana. tutamkosa sababu timu yake bora imetolewa na timu bora zaidi.
Kwa wafuatiliaji wa WC ya mwaka huu watakubaliana na wachambuzi mbalimbali wa soka duniani kuwa haya ndiyo mashindano yaliyotia fora kwa kiwango duni kati ya mashindano matano (au zaidi), ya miaka ya karibuni. Ndiyo mashindano ambayo waamuzi ama kwa makusudi au kwa ufinyu wa ujuzi wameboronga zaiai, na ndiyo mashindano yaliyoongoza kwa kuwa na warusha maonyesho ya TV wenye viwango duni zaidi hata ikilinganishwa na ligi za mataifa kadhaa... It is so sad!!!!!!!!!!
hii ni the best worldcup, wanaosema ni mbaya ni kwamba timu zao zimetolewa baaasi, mexico super, ghana wako juu ukiondoa matatizo ya umaliziaji, ureno kamwonyesha brazil kuwa ukikaa vibaya na kombe huchukui, argentina safi zaidi ya mexico, uingereza pumba za mwaka ndo maana wakachezea kichapo cha mbwa mwizi toka kwa wajeru,tatizo watu wanapenda kuendeshwa na historia, kwamba uingereza hajafungwa na ujerumani since 1966, mara oohh france ndo sijui nn, those things are outter control these days, matatizo yaliyopo ukiondoa maamuzi mabovu ambalo ni tatizo la fifa the rest ni matatizo ya kawaida ambayo hutokea kila mara kutegemea na mahali world cup ilipofanyika...SA wamejitahidi sana na naamini some of the wazungu walokuwa siku zote wanaona Afrika kwa ujumla wake ni nothing watakuwa mpaka sasa wanashangazwa na everything they see down in mzansi!!lets be realistic guys..