Uhuru mnadahi mkiwa majuu.
Lugha rahisi na nyepesi ni kuchukua KITI CHA IKULU..binafsi naamini kabisa utawala wowote hasa nci zetu maskini huanzia IKULU. Nikitazama sehemu zote za Ufisadi zimetokana na Teuzi za rais kuwapa nyadhifa hao Mafisadi toka mawaziri, wakuu wa mashirika ya Umma, wakuu wa mikoa na nafasi zote nyeti za kuvuta mtaji hutokana na uchaguzi wa rais.Tatu.. muungano huo ni lazima uwe muungano wenye misingi yake; muungano wenye lengo la kuingusha CCM tu ni muungano unaojiandaa kushindwa. Lengo la kuunganisha nguvu liwe ni zaidi ya kuiangusha CCM; yaani, kuanguka kwa CCM kuwe ni matokeo tu ya lengo hilo kuu.
Zakumi Kuli yupo nchini, anaudai uhuru hapa hapa kwa ajili yetu na ninyi mlioikimbia nchi yenu wenyewe na kuwaachia mafisadi na wawekezaji waipepete kama ngano!
Uhuru mnadahi mkiwa majuu.
Uhuru unatakiwa kudaiwa mtu akiwa wapi? na kwanini ni mahali pekee hapo panapotakiwa kudaiwa uhuru?
Tatu.. muungano huo ni lazima uwe muungano wenye misingi yake; muungano wenye lengo la kuingusha CCM tu ni muungano unaojiandaa kushindwa. Lengo la kuunganisha nguvu liwe ni zaidi ya kuiangusha CCM; yaani, kuanguka kwa CCM kuwe ni matokeo tu ya lengo hilo kuu.
Mwanakijiji:
Don't get me wrong. Sehemu yoyote unaweza kupambana. Kwa kipaji chako na kwa matukio yaliotokea Tanzania katika kipindi cha sasa, kama ungekuwa ndani ya CCM na kuanzisha vuguvugu humo, huo uhuru ungepatikana.
Lugha rahisi na nyepesi ni kuchukua KITI CHA IKULU..binafsi naamini kabisa utawala wowote hasa nci zetu maskini huanzia IKULU. Nikitazama sehemu zote za Ufisadi zimetokana na Teuzi za rais kuwapa nyadhifa hao Mafisadi toka mawaziri, wakuu wa mashirika ya Umma, wakuu wa mikoa na nafasi zote nyeti za kuvuta mtaji hutokana na uchaguzi wa rais.
Kushinda Ubunge sii tiketi ya kupewa wadhifa wa juu, wapo wabunge wengi sana walichaguliwa nje ya uongozi wa serikali na ndivyo inavyotakiwa lakini kwa kutumia mfumo wa zamani unaosisitiza hatua ya kwanza kwa uteuzi wa kiongozi wa serikali unatokana na kushinda chaguzi za Ubunge sasa hivi umepotea na wala hauna maana tena zaidi ya jina la mwakilishi kwa sababu RAIS ndiye mchaguzi wa viongozi wetu.
Hivyo inanipa shida kubwa sana kutambua vita hii itaelekeza majeshi wapi..Umesema kukiondoa chama CCM madarakani sii hoja haujali ni chama gani kitaingia madarakani..wakati namsoma Mwalimu Augustine Moshi akisisitiza ni wakati wa kukiondoa chama..Hii inanikumbusha uchaguzi wa Iran.. Hivi kweli lengo la wananchi ilikuwa kumwondoa Ahmadinajad au ilikuwa kukiondoa chama tawala. Kenya na Zimbabwe kote tumeona utata uliopo ktk kumwondoa kiongozi madarakani na itakuwa vizuri tukizungumzia zaidi majeshi yetu yaelekeze nguvu zake wapi, kwa maana fupi TATIZO LIKO WAPI?..
1. Je, kumwondoa JK Ikulu itaondoa uongozi mbaya..
2. Je, kukiondoa chama CCM madarakani (Ubunge) kutapunguza nguvu ya rais ktk kuchagua viongozi wabovu?..
3. Je, Kuonndoka kwa vyote hivi viwili kutaleta Uhuru wa kweli? na Kivipi yaani..
Huo Uongozi utakao kuja utakuwa na agenda zipi muhimu ktk kuhakikisha Uhuru wa kweli unapatikana.
Wewe bado unaamini penye daraja lazima kuna mto unapita chini. Hizo zama zimepitwa siku nyingi sana.
Kwa taarifa yako, jikumbushe South Africa walipataje uhuru wao kutoka kwa makaburu. Sina haja ya kusema mengi.
There's are so many avenue to advance this fight as long as everyone play their part.
2010 kuwa mwaka wa uhuru wetu? Sidhani. Jamaa hawa bado wamekamata sehemu zote muhimu na nyeti za Nchi yetu. CCM yenye wengi wa watu bado ndio yenye SERIKALI. Itashinda tena 2010 kote kuanzia uongozi wa mitaa na vijiji vyetu mwaka huu na MADIWANI, UBUNGE na URAIS mwakani.
Tunaojua Nchi ilikokuwa, ilipo na inakoelekea bado ni wachache mno na miongoni mwa hao tunaojua, WAOGA tuko wengi, TUNAOFAIDIKA na mfumo wa sasa hatuambiwi kitu tukasikia, NGOs, MAKANISA, MISIKITI ndio vinaamka sasa.
Kazi bado mbichi kabisa lakini tusikate tamaa kwa kuwa UHURU na MABADILIKO huletwa na WACHACHE.
Zakumi mashamba wameshagawana, yale ya NAFCO wamepewa wawekezaji - ni 2 tu yamerudishwa kwa wananchi ila na hayo bado hali ya ugawaji wake ni tete. Kule Kilosa ndio usiseme, wakuu wana ekari na mahekta. Na hapo Mvomero nako mmh. Ibwagwamoyo wameuza kwa bei chee mashamba ambayo wajamaa tuliyataifisha kwa maslahi ya umma. Hivyo kama unarudi basi huwezi kuikimbia siasa ya ukombozi, lazima kwanza ujiunge kupigania uhuru wa pili - na tutakapoupata huo uhuru wetu mwaka 2010 kamwe hatutakubali uwe kabaila humu, labda uwe mkulima mwenza wa kijamaa!
Kuna kitu kinaitwa common enemy. South Africa waliweza kufanya vile kwa sababu walikuwa na common enemy, (mzungu na siasa zake za ubaguzi).
Leo hii Mwanakijiji anapigania haki sahihi, lakini maadui ndugu zake tena wengine wa damu. Akirudi kwao kijijini anamkuta mjomba wake ana shati la CCM. Binadamu yake kajenga nyumba nzuri aliyofikia kwa kutumia pesa za akaunti ya EPA.
Mambo yanayofanywa na watawala wetu yangekuwa yanafanywa na wageni, tayari tungekuwa na sirikali mpya.
Kuna kitu kinaitwa common enemy. South Africa waliweza kufanya vile kwa sababu walikuwa na common enemy, (mzungu na siasa zake za ubaguzi).
Leo hii Mwanakijiji anapigania haki sahihi, lakini maadui ndugu zake tena wengine wa damu. Akirudi kwao kijijini anamkuta mjomba wake ana shati la CCM. Binadamu yake kajenga nyumba nzuri aliyofikia kwa kutumia pesa za akaunti ya EPA.
Mambo yanayofanywa na watawala wetu yangekuwa yanafanywa na wageni, tayari tungekuwa na sirikali mpya.
kila kitu ni mikakati na kwenye siasa hakuna kitu muhimu kama mikakati yenye timing. Believe me, ningekuwa nyumbani labda sasa hivi nisingekuwa na muda wa kufanya ninayofanya.
ulivyosema hapo juu ni kama kuashiria kwamba ambaye hayuko Tanzania hapaswi kupigania uhuru wa taifa lake na ni wale walioko nyumbani tu ndio wenye haki na sababu ya kufanya hivyo.
Mwanakijiji:
You are absolutely right, mikakati yenye timing ni kitu muhimu. Lakini watanzania wengi hatujuhi tunapigania nini?
Kama unashindwa ku-define unachopigania, mikakati yako yenye timing itakuwa ni kitu cha bure.
Kwa mfano katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, vita vilikuwa dhidi ya ufisadi. Now, uchaguzi unakaribia vita vipo kwenye uhuru, na baadhi ya mafisadi wamekuwa viongozi wa kupambana na ufisadi na wengine wanaogopa usalama wa maisha yao.