2010 - Ni Mwaka wa Uhuru Wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2010 - Ni Mwaka wa Uhuru Wetu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 13, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kijarida chako ukipendacho kimetoka; jipatie nakala yako, wasambazie wengine, na waalike wajiandikishe waweze kupata dozi ya fikra mpya za mabadiliko ambazo hutangulia mabadiliko ya kura!

  [​IMG]
   

  Attached Files:

  Last edited by a moderator: Aug 13, 2009
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Ishakuwa independence day tena?

  Duh!
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Aug 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  What is at stake in 2010 is not their political positions or our own aspirations; what is at stake is our freedoms and liberties; as long as mafisadi still rule over us, we are not free.
   
 4. Companero

  Companero Platinum Member

  #4
  Aug 13, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Naam ndio maana Kuli naye katoa Waraka wake wa Uchaguzi wa 2010!
   
 5. J

  Jews4ever Member

  #5
  Aug 13, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heshima mbele wakuu!
  Nathamini sana kazi mchango wenu katika jamii ya Tanzania.


  Wadugu,uchaguzi unakaribia,imekua ni mazoea kama sio utamaduni,
  kuona jukumu la kupiga kura linachangiwa kwa kiasi kikubwa na
  wenzetu wanaoishi vijijini huku sisi tuliopata nafasi ya kuona mwanga wa elimu na dunia kwa ujumla tukitoa maoni ya nani hafai,anaboa,n.k


  1.Sisi tuliopo ughaibuni, mnaonaje tukianzisha kampeni maalumu ya kitaifa
  na kimataifa kutafuta fedha za msaada kama michango, ili tuwezeshe wasio na fedha za kutosha wajumuike nawe mwenye uwezo mzuri kifedha kurudi nyumbani kwaajili ya kupiga kura ya ushindi?


  2.Kuepuka gharama hizo, ni kupata fursa ya kupiga kura tukiwa nje ya nchi,
  je kwa miezi iliyobaki tunawezafanikisha jambo hili?


  Tazama uzuri wa nchi unaoishi sasa, ni matunda ya mkakati mzuri waliojiwekea waasisi wa mataifa hayo,yamkini hatua zao za mwazo kabisa ktk mapambano zilikuwa katika level inayofanana na pendekezo kama hili.

  Ni lini basi tutatoka katika uongozi huu wa mafisadi,wezi,wenye chuki,usiopenda wala kuthamini nchi na watu wake?

  Chukua hatua, pamoja tunaweza.

  Pole kwa waliokwazika!

  Naomba kutoa hoja.

   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Aug 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,

  Seriously, hivi kweli uchaguzi wa mwaka 2010 utaweza vipi kutusaidia ikiwa CCM wataendelea kuwa madarakani?..

  Maanake nimepiga mahesabu weee sioni ndani kwa sababu hao Mafisadi hawahitaji kuwa serikalini wala kuwa Wabunge..Mambo yote wanayoyafanya yanatokana na wao wenyewe kwani Ukitazama Lowassa as PM alikuwa chaguo la JK, Rostam ni chaguo la marais wote wawili ktk nafasi nyeti ambayo haikumhusisha mwananchi..Manji, Patel na wengine wote hawapo hata ktk ukatibu kata lakini wanatesa..

  Sasa huu uchaguzi wa 2010, utaweza vipi kutuletea Uhuru huo ikiwa sisi wenyewe bado tuna matumaini ndani ya chama ambacho ni mlezi wa Mafisadi!..Viongozi wote tunaowategemea toka JK mwenyewe, Mwandosya, Kigoda, Magufuli, Asha Rose Migiro na sijui kina nani wote hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kufungua mdomo wake kuhusiana na Mafisadi..Tunawaona kina Mengi na Zitto ni wachawi hawatakiwi, wana wivu na chuki, Dr. Slaa tunaambiwa Chadema haifai kuongoza, Mwakyembe na Mama Kilango tayari wameisha pata washindani dhidi yao..

  Hadi sasa hivi hakuna mgombea yeyote aliyejitokeza ktk majimbo waliyokamata Mafisadi toka chama tawala zaidi ya fununu za hapa na pale..

  Sasa kweli hizi nguvu za kutafuta Uhuru zitaanza siku ya kuchukua form au vipi na kina nani wanatakiwa kuondoka maanake tusipowachagua ktk Ubunge, bado JK anazo nafasi 10 safi kibindoni na sii lazima wawe wabunge, nafasi nzuri ya kula ipo ktk Ukuu wa Mkoa maana ndiko una control fedha na matumizi ya mkoa au sio?..Haya kwa kuwaongezea zaidi tamu ya hoja, wengi wetu tunapinga JK kuweka sahihi mfuko wa Majimbo!
   
 7. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  It is true that Tanzania needs a second independence, an independence from CCM. It is clear that CCM cadres lord it over the masses. Most Tanzanians are not CCM members and are not free to contest elections (because they do not toe any party line).

  I would say only about 5% of Tanzanians of majority age belong to political parties and are thus eligible to contest elections. We need a kind of independence that allows anyone, irrespective of which party they belong to or whether they belong to any party at all stand for and even win elections. Why can't we be that free?

  It is true, as Mkandara says that many corrupt people are not elected officials. Yes, but they are CCM stalwarts and have been placed in positions of authority by CCM leaders. If we are freed from CCM, we will automatically be freed from the devils you have listed. Our political and economic woes can all be traced to mismanagement by CCM leaders. To free ourselves from them presupposes freedom from CCM first!

  We have been lied to a great deal. The last time CCM wanted to renew its stronghold over the masses, it lied that it wanted better life for ALL. Yes, there is a better life now, but it is only for ALL the sixty ministers and the top echelons of CCM. The CCM President stated that he wanted a big government because of his program. But his only program so far has been that of creating a big government and making life unbearable for almost everyone esle!

  Frantz Fanon was right on the money. There has been a false start in Africa. There has been a particularly false start in Tanzania. We need to be freed from this false start so that we can embark on a good start. We need a new beginning. That cannot be done before we free ourselves from the shackles of CCM first.

  Tanzanians have a date with destiny next year. They can choose to re-elect CCM and continue to be the economic backwater of East Africa and the country that is ignored by everyone who is anyone that visits the region, or they can choose to free themselves from CCM and create a new future for themselves.
   
 8. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  At least watu wameanza kumjua Mwanakijiji ni nani, wengine wameanza malumbano maji usiyoyajua kina chake usijaribu
  2010 lazima tukate mzizi wa kifisadi mbichi na mbivu
   
 9. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumeonewa kiasi cha kutosha, tumedharauliwa kiasi cha kutosha. Unyonge na ujinga wetu ndio umetufanya tuonewe, tuonyonwe na tudharauliwe.

  Angalizo la MMKJ kuwa 2010 ni nafasi pekee kwa ajilili ya ukombozi wetu ni sahihi kabisa. Lakini suala la msingi ambalo wasomi na wanaharakati wengi tunasahau ni namna ya kuendesha mikakati yetu. Information through internate inawafikia chini ya 5% ya watanzania. Hata survey yangu kwa watu wa mjini ni chini ya 20% wanapata information through internate.

  Kwa hiyo ushauri wangu ni kuwa tuanze from grassroot kuraise awareness ya watu wetu. nini wajibu wao katika ukombozi wao na wa taifa lao. Bado asilimia kubwa ya watanzainia hawaelewi nini sera mbadala ya ile ya ccm. hata vyama vyetu vya upinani vinabakia kuwa mjini zaidi.

  Ndugu MMKJ tunaomba mikakati yako ni kwa vipi tuwaendee wananchi katika grassroot. Vingenevyo tunaishia katika mitandao na watu wetu wanaendelea kuwa kama kondoo asiye na mchungaji
   
 10. Jenerali QoyoJB

  Jenerali QoyoJB JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  harakati za uhuru mpya wa taifa letu lazima zianze mapema, tuambieni nani asimame kuwa rais kwa chama gani kinachokubalika? tumeshaanza kuamini kuwa chdema huenda kinakubalika sasa wengine mnasema hakifai kupewa nchi mbona tunapingana wenyewe? pendekezeni sasa nani asimame na kwa chama gani?

  Au tuunde chama kipya? lazima tuanze sasa afahamike mtu na chama gani. Mtu atakayejitokeza lazima asiwe na kasoro na akubalike siyo siyo mtu hajanawa uso wake afu anakagua nyuso za wenzake wenye macho lazima wataona na kujua kuwa hajanawa uso(Fisadi).

  Wa Tz mlioko nje kama mnaona kuna mwenzenu anafaa huko mrudisheni nyumbani tumfahamu sasa.

  Anayesma chadema haifai atuambie haifai kwasababu gani ni mbadala wake? au tuunde kipya tuchukue kina slaa? minafikiri Chadema ndiyo chama ila watu wapya wasimame siyo kna mbowe, na kama mbowe unanisikia achia ngazi kagombee ubunge tupe mtu mwingine. Siyo kwamba hatukutaki ni kwamba onyesheni mfano ili mkubalike.

  Semeni sasa!
   
 11. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135

  Hii sio kwa Tanzania pekee. Ni kwa kila nchi nyingi barani Africa. Vyama vilivyopewa uhuru vimeishia kuwa na nguvu ya ajabu. Hivyo ni kweli...Nchi nyingi sasa zahitaji ukombozi wa pili. Hii point niliiona kwenye kitabu kinaitwa 'The Shackled Continent'. Mfano mwingine ni ANC South Africa ilivyo na nguvu, nk
   
 12. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hizi falsafa za ugahibuni hizi....kaka huku tumeshakula dozi za democracy, rule of law,good governance, mainstreaming gender, human rights na nyinginezo lukuki lakini wapi.....magonjwa yanazidi tu kutoka njaa, ujinga, malazi hovyo na sasa udini, ufisadi, ukandamizaji na mengine mengi...

  sasa mnapotuletea hayo ya madozi mengine kama "freedoms and liberties" mnazidi kutuchanganya sisi wajinga tuliwao bila ya kula....

  omarilyas
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  2010 kuwa mwaka wa uhuru wetu? Sidhani. Jamaa hawa bado wamekamata sehemu zote muhimu na nyeti za Nchi yetu. CCM yenye wengi wa watu bado ndio yenye SERIKALI. Itashinda tena 2010 kote kuanzia uongozi wa mitaa na vijiji vyetu mwaka huu na MADIWANI, UBUNGE na URAIS mwakani.
  Tunaojua Nchi ilikokuwa, ilipo na inakoelekea bado ni wachache mno na miongoni mwa hao tunaojua, WAOGA tuko wengi, TUNAOFAIDIKA na mfumo wa sasa hatuambiwi kitu tukasikia, NGOs, MAKANISA, MISIKITI ndio vinaamka sasa.
  Kazi bado mbichi kabisa lakini tusikate tamaa kwa kuwa UHURU na MABADILIKO huletwa na WACHACHE.
   
 14. m

  mashuke Member

  #14
  Aug 14, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Nafikiri waraka wa wakatoliki unawaweka wananchi wengi kuanzia walioko vijijini kujua haki na wajibu wao katika kuchagua viongozi safi.Wanaoupinga kama Kingunge naona kama ni mafisadi na wamefulia.Vyombo vingine vya kijamii vichukue hatua kama hizi za kuwaelimisha wananchi hasa wa vijijini ili wasije kurubuniwa na mafisadi hasa wanaotoka CCM wakati wa uchaguzi kwa kupewa pilau,fulana,kofia na vitenge vya sh 3000 ambavyo hivimsaidii mwananchi huyu baada ya uchaguzi.Huu ndiyo utakuwa ukombozi pekee wa nchi hii kutoka mikononi mwa viongozi wasiokuwa na uchungu,uzalendo na ustawi wa jamii yetu kwa uwiano uanokubalika.
   
 15. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  tatizoo sio chama gani kuchukua madaraka ila ni watu wa aina gani wapewe uongoziii..

  hatujajiaminii vya kutosha na kuamua kwa pamoja kuleta mabadilikooo..Mabadilikoo yeyote ya uongozii wa taifa hili kwa sasa yatatusaidiaaaaa..

  hatuna haja ya kuudhofishaa mwelekeoo wa mageuzi ya kiuongozii zaidi ya kuimarishaa ili tufikiee tunakohitajiii..
   
 16. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri sana mwanawane, ila sasa hapa naona kama itakuwa kutafutiana nauli na isitoshe kwa asili ya watanzania anaweza hata kutofika kwenye kituo kutuletea habari mbali na kutopiga kura ingawa wazo lako ni zuri

  Mimi nilikuwa nafikiria wazo la kuchangisha hela ni zuri lakini sasa kwa mfano jarida kama CHECHE nafikiria tunasoma sisi tuu wa mjini ambapo ndio tumepata mwamko mkubwa juu ya SIASA inavyokwenda kwa ujumla nilikuwa nafikiri kwanini tusifanikishe kufikisha vijarida kama hivi vijijini maana ndio ambako kura nyingi zipo huko ili watu wakaelewa nchi inakwendaje na wabunge wao wana msaada gani kwa jimbo husika nafikiri itasaidia sana na uzuri kwamba sasa hivi kura zinaamuliwa jimbo na wananchi hasa hizi za wabunge wa CCM za awali.
   
 17. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Independence day inatakiwa ianze 25 Oktoba 2009, siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa, swali ni: je tunatambua kuwa siku hiyo kuna uchaguzi muhimu? Mnyika John aliandika jamvini kuhusu hilo lilipita bila kusomwa. Je watanzania wote wanajua umuhimu wa tarehe hiyo, je sheria za uchaguzi zimekaa sawasawa, eg kwa nini wagombea wasifanye kampeni? Je kwa nini hakuna wagombea binafsi, mnaona tumeanza kujiuliza chama gani kinafaa kungekewa na indipendent candidates tungeuliza nani anafaa. Je tuendelee na uchaguzi huo muhimu katika hali ambayo refa ni kama mchezaji?

  Je kuna umuhimu wa kuendelea na tume iliyopo ya uchaguzi, je inaweza kuwa huru, anayeiteua naye mgombea haki itatendeka kweli, these things are fundamental if we want our independence.
   
 18. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  CCM hiyo replacement ya CCM mbona haitajwi?
   
 19. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ndipo hapo na mi nashindwaga kupata jibu lenyewe?
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Aug 14, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Uamuzi uliopo mbele yetu ni zaidi ya Chama; anayefikiria kuiondoa CCM na kuingiza Chama kingine madarakani kutaondoa matatizo yetu bado hajapata vizuri uelewa wa mapambano haya. Lengo siyo kubadilisha chama tu au kama alivyosema Mandela kubadili "mkoloni mweupe kwa kumleta mkoloni mweusi".

  Ni kweli hadi hivi sasa kama nilivyoandika kwenye ukosoaji wa wazi wa wanaharakati utaona kuwa hivi ni vita vya kubahatisha; hatuko tayari kumpelekea adui mapambano nyumbani kwake.

  Hata hivyo, ninaamini mbinu mpya ya ushindi ni lazima ipatikane ikiwa na lengo tofautizaidi na lililo wazi zaidi. Binafsi kwa sasa sijali sana chama gani kitakuwa madarakani, kwangu zaidi ni ajenda tunayotaka kuwa nayo.Hivyo, la kwanza naamini ajenda itoke kwa wananchi wenyewe na kutokana na hiyo ndiyo kiwe kipimo cha kuchagua viongozi wajao.
   
Loading...