Elections 2010 2010 - Ni Mwaka wa Uhuru Wetu

Hivi unafikiri hadi hivi sasa sijui ndugu zangu ambao ni sehemu ya ufisadi huu? Unafikiri ninaangalia damu yangu ili kujua kama nikemee au la. Sina umoja wa aina yoyote wa kidini, kidamu, kilugha, kirangi au kimahali na anayeshiriki kwenye ufisadi. Wana matatizo wenye kuangalia fisadi kwa minajili ya dini, rangi, kabila au urafiki wao. Kama hii kweli ni vita basi ichukuliwe kama hivyo. Ndugu aliyeungana na adui siyo ndugu yangu tena!

Mwanakijiji:

Don't get me wrong. Ninapojibu posti yako, sina maana ya kukutaja wewe binafsi. Kwa hakika kuna watu wachache sana ambao wanaweza kutenda haki bila kuangalia dini, rangi, kabila au urafiki wao. Na initiatives nyingi zinakwamia hapa.
 
Aisee unaondoka hata bila kuaga? miye nilikuwa bado hapa kwa maana ilielekezwa kwangu moja kwa moja.

Uhuru mnadahi mkiwa majuu.

Kumbe tuko kiujumla sasa. Nakupata vizuri sasa. Unafikiri kiini cha ufisadi tunaousikia ni nini hasa?
 
Tunangoja kwa hamu uhuru wetu wa mwaka 2010

Froida, uhuru huo haungojewi bali unatendewa kazi ili kuuleta. Hautakuja kama hisani bali utachukuliwa kama kwa nguvu; yaani watawala hawawezi kutunyima tukiufanyia kazi kuupata.
 
Aisee unaondoka hata bila kuaga? miye nilikuwa bado hapa kwa maana ilielekezwa kwangu moja kwa moja.

Kumbe tuko kiujumla sasa. Nakupata vizuri sasa. Unafikiri kiini cha ufisadi tunaousikia ni nini hasa?

Mwanakijiji:

Bado nipo, lakini nilikwama kwenye posti yako # 40. Kuna maneno muhimu sana yaliojificha katika posti hile. Uliyosema ni sawa na vitu nivyokuwa nachambua siku mbili zilizopita.

Sasa hivi wanasema CCM imegawanyika. Hivyo nilijaribu kuangalia hayo makundi na kuangalia profile zake.

Ndio kuna mgawanyiko ndani ya CCM. Lakini mgawanyiko huu sio wa kutegemewa katika maslahi ya kitaifa kwa sababu sio wa kiitikadi au kupigania misingi ya chama. Na kama ungekuwa wa kiitikadi basi kundi moja lingejitoa na kuanzisha chama kingine kama vile Mtemvu au Mrema alivyofanya.

Ni mgawanyiko wa makundi ya kutafuta mtu ambaye atakuwa rais katika uchaguzi utakaotekea karibuni ambaye atalinda au ku-advance maslahi ya watu katika kundi lake.
 
Ndio kuna mgawanyiko ndani ya CCM. Lakini mgawanyiko huu sio wa kutegemewa katika maslahi ya kitaifa kwa sababu sio wa kiitikadi au kupigania misingi ya chama. Na kama ungekuwa wa kiitikadi basi kundi moja lingejitoa na kuanzisha chama kingine kama vile Mtemvu au Mrema alivyofanya.

Zakumi yashikilie maneno haya; mgawanyiko uliopo sasa hivi CCM ni lazima utasababisha kundi moja kujitoa kwani makundi yote mawili hayawezi kukaa pamoja kuelekea uchaguzi mkuu. Ni lipi litajitoa na kwa nini inategemea nguvu ya kundi hilo kuelekea uchaguzi mkuu.

Ni kweli vile vile kuwa mgawanyiko uliopo sasa siyo wa kiitikadi ni wa kimaslahi zaidi ya kisiasa ya wahusika. Hata hivyo, kwa kadiri tunavyoendelea lengo langu binafsi ni kuulazimisha kuwa mgawanyiko wa kiitikadi. Si unajua mwanzoni kina GWB walienda kule kutafuta "WMD" baada ya kushindwa kuyapata wakatafuta sababu ya kuhalalisha vita yao?
 
Mwanakijiji,
Narudisha tena swali langu... naona tunayoyoma tu..

Nimeandika hivi:- inanipa shida kubwa sana kutambua vita hii itaelekeza majeshi wapi..Umesema kukiondoa chama CCM madarakani sii hoja haujali ni chama gani kitaingia madarakani..wakati namsoma Mwalimu Augustine Moshi akisisitiza ni wakati wa kukiondoa chama..Hii inanikumbusha uchaguzi wa Iran.. Hivi kweli lengo la wananchi ilikuwa kumwondoa Ahmadinajad au ilikuwa kukiondoa chama tawala. Kenya na Zimbabwe kote tumeona utata uliopo ktk kumwondoa kiongozi madarakani na itakuwa vizuri tukizungumzia zaidi majeshi yetu yaelekeze nguvu zake wapi, kwa maana fupi TATIZO LIKO WAPI?..
1. Je, kumwondoa JK Ikulu itaondoa uongozi mbaya..
2. Je, kukiondoa chama CCM madarakani (Ubunge) kutapunguza nguvu ya rais ktk kuchagua viongozi wabovu?..
3. Je, Kuondoka kwa vyote hivi viwili kutaleta Uhuru wa kweli? na Kivipi yaani..

4. Je Huo Uongozi utakao kuja utakuwa na agenda zipi muhimu ktk kuhakikisha Uhuru wa kweli unapatikana. __________________
 
Tatizo la kufikiria kuwa kuondoa chama kimoja kutatua tatizo/matatizo tuliyonayo kwa kukiingiza chama kingine. CCM kama chama ni umwilisho wa utawala wa kifisadi ni wabebaji wa lawama zote za matatizo ya kifisadi kwani wao ndio waliounda serikali na ajenda yao ndio serikali inatekeleza. Kukiondoa madarakani basi kitamuondoa mtu wa kumlaumu. Wakati huo huo unapoingiza chama kingine na chenyewe kitapata tendencies zile zile za vyama tawala duniani (tumeona yaliyotokea Kenya, Zambia na kwingineko).

Sasa kuna njia ya haraka ya kuondoa tatizo nalo ni kuing'oa CCM madarakani. Lakini hiloo ni sawa na mtu ambaye mguu wake umevunjika na kwa haraka watu wanaamua kukata pale juu kwenye goti na kunyofoa ile seheu yenye madhara. Lakini watashughulikia vipi tatizo la uvujaji damu, uambukizwaji kwenye kigota?

Hapa ndipo linakuja suala zima la kuangalia hii vita kwa upana wake. Majeshi ya Marekani yalipoingia Iraq yaliingia kwa mbwembwe zote za kivita na ninakumbuka siku ile sanamu ya Saddam ilivyoanguka Baghdad na kuashiria "ushindi". Kutokana na hilo GWB akasimama juu ya meli ya kivita nyuma yake bango likitanza "Mission Accomplished". Miaka nane baadaye vita inaendelea na gharama kubwa imelipwa.

Ninachosema ni kuwa CCM ilivyo sasa haipaswi na haifai kuaminiwa utawala wa nchi yetu; lakini katika kufanya hivyo tunataka kiingie nini na nani na kwa nini?

Hapa linakuja suala la Ajenda.

Umesema hapo mwisho:
1. Je, kumwondoa JK Ikulu itaondoa uongozi mbaya.

Siyo lazima ni sawa na kumuondoa Kaunda na kumuingiza Chiluba. It has to be more than removing an individual.

2. Je, kukiondoa chama CCM madarakani (Ubunge) kutapunguza nguvu ya rais ktk kuchagua viongozi wabovu?..

Hapana kwani nguvu ya Rais kuchagua viongozi (wabovu au wazuri) haitegemei chama anachotaka; ni nguvu yake kikatiba.

3. Je, Kuondoka kwa vyote hivi viwili kutaleta Uhuru wa kweli? na Kivipi yaani..

Lengo siyo kuondoa ili visiwepo na badala yake kuingiza vingine vyenye mfanano huo huo. Lengo lazima liwe juu ya haya yote.

4. Je Huo Uongozi utakao kuja utakuwa na agenda zipi muhimu ktk kuhakikisha Uhuru wa kweli unapatikana. __________________

Huo uongozi hauwezi "kuja" na ajenda muhimu; uongozi huo unapaswa kuwa na ajenda hizo sasa. Bahati mbaya hadi hivi hakuna chama cha siasa nje ya CCM ambacho kina ajenda ya kueleweka (sizungumzii "ilani" ya uchaguzi). Mwakani ajenda ya uchaguzi itatoka kwa wananchi wenyewe. Lakini wananchi wawe na ajenda gani? Hapa ndipo ilikuwepo haja ya viongozi wa dini kwa mfano, kukaa pamoja (siyo kama walivyofanya Wakatoliki peke yao) na kutengeneza ajenda mpya ya taifa.

Siyo viongozi wa dini tu hata taasisi binafsi na makundi mbalimbali ya wananchi wanaweza kuwa na ajenda ambayo wanaweza kuipendekeza kuwa ni ajenda ya taifa. Hii JF inaweza ikatengeneza ajenda yake na kuiuza kuwa ni ajenda ya wananchi. Viongozi wanaotaka kutuongoza 2010 itapaswa wakubaliane kwa asilimia 100 na ajenda hiyo.
 
Nafahamu hilo lakini pia wahenga walisema, "Kikulacho ki nguoni mwako."

Kwa hiyo wewe unaniambia kuwa ndugu yako au baba yako akiua kwa makusudi hauta mpeleka police?

Yes, we know who is our common enemy. CCM knows who is our common enemy. They are on the driver seat. Are they taking any action? No.

Do you think if they take action I will support them 100%? You bet.

So, we need to think outside the box.

Binafsi nitampeleka. Lakini ni lazima tuzungumze kiujumla hapa. Kama kweli tungekuwa tunapelekana police, haya mambo ya ufisadi yasingekuwepo.

Kwa mfano: Miaka ya zamani nilikuwa naishi Kigamboni, kule kulikuwa na wizi wa mazao. Kwa bahati kuna wasukuma wanaoishi kule. Kwenye mkutano mmoja wasukuma wakashauri kuanzisha sungusungu hili kulinda mali. Hivyo wasukuma na wazaramo wakaanzisha ulinzi wa sungusungu. Siku ya kwanza, kijana wa kisukuma akakamatwa anaiba mihogo. Akapelekwa kwenye ofisi ya kijiji na baadaye polisi.

Siku ya pili, mtoto wa mwinyi wa kizaramo akakamatwa anaiba nazi. Na yeye akapelekwa ofisi ya kijiji lakini wazazi wakafanya mipango mpaka kijana akaachiwa bila kufikishwa polisi.

Wasukuma wakaona kuwa wanaonewa na watani zao. Na baada ya muda si mrefu jeshi zima la sungusungu likafa na wizi wa mazao ukaendelea kuwakumba wasukuma na wazaramo.

Kwa upande wangu, Lowasa na familia yake ni wezi. Lakini mke wake anaweza kuandaa party ya kidini kumshukuru Mungu na kuandika kuwaalika watu watakaotoa waraka wa jinsi ya kupiga kura 2010. Na kuna watu hapa JF wanaona hakuna makosa. Lakini tunasahau kuwa mama Salma Kikwete naye ana dini yake na anaweza kuandaa watu wa dini yake kufagilia familia yake.

Hivi vitu vinafanyika sasa.
 
Froida, uhuru huo haungojewi bali unatendewa kazi ili kuuleta. Hautakuja kama hisani bali utachukuliwa kama kwa nguvu; yaani watawala hawawezi kutunyima tukiufanyia kazi kuupata.

na hapo ndipo tunapokwama siku zote, kwani wanaojitolea kwa dhati kwenye mapambano haya nguvu yao baaaado ni ndogo saaana....trust me guys.....
 
Aisee unaondoka hata bila kuaga? miye nilikuwa bado hapa kwa maana ilielekezwa kwangu moja kwa moja.

Kumbe tuko kiujumla sasa. Nakupata vizuri sasa. Unafikiri kiini cha ufisadi tunaousikia ni nini hasa?

fikra mbovu na tamaduni mbovu ndizo chanzo,hili ni tatizo wala sio chama ,ukitaka kufahamu hilo mtumie ndugu zako fedha akununulia kitu fulani wape ndugu zako watatu tofautitofauti na hakika kati yao mmoja lazima akufisadi, yani lazima ukupige panga tu ,atakununulia lakini kile cha juu lazima kiwepo.

Tatizo hili ni karibu kwa watanzania tulio wengi, hivyo hao walio ktk vyama ambavyo hawafisadi ni kwasababu hawajapata mwanya huo.Ufisadi kwa tanzania unafanywa karibu na kila mtanzania ila utofauti wao unaonekana kutokana na mazingira na nafasi walizonazo.Tatizo na fikra zetu.

wewe hujawahi kuona mtu smart ana minyumba mjini lakini kwao kweupe? tatizo si yeye tatizo watanzania wa huko kijijini kwake wana mforce akae mjini ama asirudi kwao.Tuna tatizo la kifkra huu ndio uhuru halisi tunaotakiwa kuutafuta uhuru maomboleo wa kudondosha ccm sio uhuru.
 
Zakumi yashikilie maneno haya; mgawanyiko uliopo sasa hivi CCM ni lazima utasababisha kundi moja kujitoa kwani makundi yote mawili hayawezi kukaa pamoja kuelekea uchaguzi mkuu. Ni lipi litajitoa na kwa nini inategemea nguvu ya kundi hilo kuelekea uchaguzi mkuu.

Ni kweli vile vile kuwa mgawanyiko uliopo sasa siyo wa kiitikadi ni wa kimaslahi zaidi ya kisiasa ya wahusika. Hata hivyo, kwa kadiri tunavyoendelea lengo langu binafsi ni kuulazimisha kuwa mgawanyiko wa kiitikadi. Si unajua mwanzoni kina GWB walienda kule kutafuta "WMD" baada ya kushindwa kuyapata wakatafuta sababu ya kuhalalisha vita yao?

Mimi kama mwangaliaji nitasubiri tu mpaka mwakani.
 
Mimi kama mwangaliaji nitasubiri tu mpaka mwakani.

tuna watazamaji wengi na waangaliaji wengi sana; ni vizuri kutoka kuwa waangaliaji na kushiriki kuleta mabadiliko tunayoyataka. Wewe ukiangalia na mimi nikiangalia na yule akiangalia nani atafanya?
 
tuna watazamaji wengi na waangaliaji wengi sana; ni vizuri kutoka kuwa waangaliaji na kushiriki kuleta mabadiliko tunayoyataka. Wewe ukiangalia na mimi nikiangalia na yule akiangalia nani atafanya?

Kisheria kushiriki kwangu ni kuingilia mambo ya ndani ya taifa lingine. Hivyo kilichobakia ni kuangalia tu.
 
Kisheria kushiriki kwangu ni kuingilia mambo ya ndani ya taifa lingine. Hivyo kilichobakia ni kuangalia tu.

Inategemea na nature ya kushiriki kwako. Kwa kuangalia tu tayari unashiriki albeit passively. Lakini bado unaweza kushiriki vile vile pasipo kuvunja sheria.
 
Inategemea na nature ya kushiriki kwako. Kwa kuangalia tu tayari unashiriki albeit passively. Lakini bado unaweza kushiriki vile vile pasipo kuvunja sheria.

Mwakani narudi kuwa mkulima. Nadhani nikiwawezesha watu wa kijijini kwetu kulima na kutengeneza pilau wenyewe, hawatakuwa na njaa za rejareja.
 
Kisheria kushiriki kwangu ni kuingilia mambo ya ndani ya taifa lingine. Hivyo kilichobakia ni kuangalia tu.

Du mkuu ushaukana uraia wa nchi yako ya kuzaliwa. Siamini. Hebu soma makala yangu kuhusu uraia na uzalendo - ipo Pambazuka News.
 
mimi hapa tatizo naona ni kwamba kilamtu anataka kuingia ikulu,ndio maana hata hao mapapa awali tuliwaona vidagaa lastly tumeona outcome zake,"Even satan wears white"they are all pretending sijaona anayefaa Only God can rule his creatures!!!
 
Back
Top Bottom