hebu nenda pale muhimbili kawaulize wagonjwa haya maswali halafu uone watakufanya nini. Mnakaa kushabikia upuuzi na kuleta maswali ya kizembe tu, kwanza wagonjwa watibiwe huku majadiliano yanaendelea au elitaka wagonjwa wasubiri mpaka hao madaktari watimiziwe shida zao?
Kwanza hii ni porojo tu ya mkuu ambaye amekubuhu na kutukuka kwa uongo. Wote mnakumbuka muda kiasi gani ulipita kabla madakatari kutoka jeshini kufika Muhimbili awamu ya kwanza ya mgomo. Hivyo unaposema kuwa wagonjwa watibiwe, swali ni lini? Vilevile, tusidanganyane duniani hakuna nchi yenye ziada ya madaktari.
Tatu hii inaonyesha kuwa serikali haitaki tu kuwapa madaktari wetu malipo ya kukidhi mahitaji lakini uwezo inao kama inavyoainishwa hapa chini:
Kama serikali ingetumia busara kidogo tu na kuwaajiri hawa sawa na wanataaluma kutokana na unyeti wa kazi zao kwa uhai wa Watanzania wangeweza kabisa kuwapa mshahara wa TZS 3,500,000/=. Hata kama ingekuwa pungufu ya hapo lakini sio laki tisa.
Ina maana kuwa class mate wako aliyebaki MUHAS akaajiriwa kama mhadhiri msaidizi na wewe unayeajiriwa kuwa Daktari kule Ikwiriri tayari mnapishana kwa zaidi ya laki tano. Ikiwa tuna madaktari (MD) wasiozidi 2,500 malipo yao yanawezekana kabisa. Kwani unadhani zinahitajika fedha kiasi gani?
Mbona serikali haisemi? Kwa taarifa yako kama kwa wastani kila daktari angelipwa 7,000,000/= (mara mbili ya madai yao maana kuna masinia) basi kwa mwezi serikali ingetumia TZS bilioni 17.5 sawa bilioni 210 (inalingana na pesa ambayo serikali imeamua kukodi madaktari toka nje) kwa mwaka ambayo ni sehemu ndogo sana ya posho za vikao (sitting allowance) serikalini, kwenye mashirika ya umma na serikali za mitaa.
Nina uhakika kuwa malipo halisi yatakuwa pungufu ya haya na yanawezekana. Hii ingeonyesha jinsi serikali ilivyo makini na inavyojali uhai wa Watanzania lakini sasa imeonyesha kinyume chake ndio maana haijali kuona mtu ameuwawa, uhai kwa serikali hii si kitu cha thamani hata kidogo.
Je, ni mambo mangapi ya kipuuzi yanayofanywa kwa kutumia fedha nyingi za taifa zaidi ya hizi? Yana umuhimu gani kwetu kama Watanzania?
Ukweli ni kuwa tu serikali haitaki na kunapokuwa na watu kama wewe ambaye unaiunga mkono wanafarijika sana maana wajinga ndio waliwao. Hivi kweli ukiwa mgonjwa ukatibiwa na daktari ambaye hajaridhika unadhani utapata huduma inayotakiwa? Walazimisheni, wafukuzeni na muwajengee chuki madaktari; matunda yake sote tutafaidi.
"Mungu hadhihakiwi, kwa maana apandacho mtu ndicho atakachovuna"; na kwa nchi au utawala ni hivyo hivyo.