200billion kukodi madaktri ni sahihi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

200billion kukodi madaktri ni sahihi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MASIKITIKO, Jun 30, 2012.

 1. M

  MASIKITIKO JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 841
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
  Katika gazeti la Tanzania Daima la leo kuna habari hiyo.
  Hapa napata maswali mengi kiliko majibu.
  1.kwa nini kiasi hicho kisitumike kutekeleza madai ya madaktari na kutanzua mgogoro huo?
  2.Fedha hizi kwa nini zisitumike kuboresha hospital kwa kununua vifaa vya hospital?
  3.Kwa nini kwa Serikali hii kukija swala la kukodi kitu fedha hupatikana mara moja?
  Na maswali mengine mengi,hebu tuisaidie serikali katika kufanya mipango yake.Tujadili
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Sijui wanakuwa wamerogwa na zile posho?yaani washauri kila kada lakini vitu haviendi!!washauri wa JK na mawaziri wote na usalama ,wakuu vyombo vya usalama hawayaoni haya?utakodi ma DR hadi lini?hiyo pesa umepata wapi haraka hivi?mishahara je italipwa kweli kwa wakati??
   
 3. King2

  King2 JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwanini zisitupe pia fursa vijana kupata ajira.
   
 4. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chama changu
   
 5. paty

  paty JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,253
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  wakifanya ivyo wataweka rekodi duniani , sisi kama tumerogwa vile, yaani iyo pesa imekuwa azi kusaidia kuboresha mazingira ya kazi kwa madaktari , then iyo itumike kuwaleta madaktari toka nje , kweli hii itaingia kwenye vitabu vya Guinness world book of record
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,307
  Likes Received: 22,111
  Trophy Points: 280
  Tanzania ni zaidi ya uijuavyo
   
 7. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Cccm ccm ccm ccm ccm ccm


  HABARI KAMIKI TOKA TANZANIA DAIMA

  SERIKALI imeamua kuagiza madaktari kutoka nchi za nje watakaochukua nafasi ya wale wa hapa nchini ambao wamegoma kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.

  Habari kutoka katika moja ya vyanzo vya kuaminika zimesema kuwa uamuzi huo wa serikali ulipitishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana mjini Dodoma juzi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.

  Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa Rais Kikwete alikerwa na tabia ya madaktari kupingana na serikali licha ya juhudi zote zilizofanywa kuboresha maslahi yao.

  Kwa mujibu wa habari hizo, kiasi cha sh bilioni 200 kimetengwa kwa ajili ya kuwaleta na kuwagharimia madaktari hao wa nje na pia baraza limepitisha azimio la kuzungumza na hospitali za jeshi kama Lugalo na zingine ndogo kubeba jukumu hilo kwa sasa pamoja kuagiza madaktari wastaafu wote warejee kazini katika kipindi hiki cha mgomo.

  Habari zimedai kuwa madaktari hao wanasadikiwa watatoka katika nchi rafiki, zikiwemo India, China, Cuba na Afrika Kusini, na kwamba wataziba kikamilifu pengo la wale wa hapa nchini ambao wamegoma.

  Inaelezwa kuwa mara baada aya kukamilika na kuanza rasmi kwa huduma za matibabu, madaktari wa hapa nchini waliomo katika mgomo na wale zaidi ya 200 waliodaiwa kufukuzwa na serikali kimyakimya, watalazimika kurejeshwa kazini kwa masharti makali.

  Hata hivyo, uamuzi wa serikali kuwatimua madaktari wakati suala lao liko mahakamani, umewagawa wabunge.

  Baadhi ya wabunge walijaribu kuhoji suala hilo Bungeni, lakini walikwama baada ya Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwa madai kuwa suala hilo liko mahakamani.

  Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala, alisema kuwa kilichofanywa na serikali ni kiini macho kwani juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema serikali haiwezi kutoa kauli dhidi ya madaktari kwa madai kuwa kuna kesi mahakamani.

  “Juzi serikali imesema kuwa haiwezi kutoa kauli kwa vile jambo hilo lipo mahakamani, sasa imewezaje kuwafukuza madaktari wakati jambo lipo mahakamani?” alihoji Dk. Kigwang’ala.

  Aliitaka serikali kuondoa kesi hiyo ili kurejesha majadiliano kwani ndio njia pekee ya kukabiliana na mgogoro huo.

  Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alimshangaa Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwani ungeweza kujadiliwa bila kuingilia uhuru wa mahakama.

  Juzi uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, uliwafukuza kazi madaktari 229 walioko katika mafunzo kwa njia ya vitendo kutokana na mgomo unaoendelea wa kushinikiza kulipwa posho zao za mwezi mmoja.

  Hospitali zingine ambako madaktari wamefukuzwa kutokana na mgomo huo ni pamoja na Mbeya na Dodoma.

  Jeshi lachukua nafasi za madaktari

  Wakati huo huo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali la kutoa huduma za kitabibu kwa wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari nchini.

  Juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa bungeni alisema serikali imeamua kuwatumia madaktari waliopo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wastaafu na hospitali zote za jeshi kuendelea kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa.

  Msemaji wa JWTZ Kanali Kapambala Mgawe katika mahojiano maalum na gazeti hili, alisema juzi baada ya Waziri Mkuu Pinda kutoa agizo hilo, walianza utekelezaji wake ambapo kwa jiji la Dar es Salaam, hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Kikosi ya 521, Mgulani na ile ya Kikosi cha Navy-Kigamboni na hospitali zake zote kote nchini zilianza kutoa huduma hiyo bila vikwazo.

  “Kwanza naomba umma uelewe hivi hospitali za JWTZ hapa nchini kwa asilimia 70 zimekuwa zikiwatibu raia bila vikwazo vyovyote hivyo agizo hilo la serikali huenda likaongeza idadi ya wagonjwa kutibiwa katika hospitali zetu labda kwa asilimia 90.

  Mgawe alisema madaktari wanajeshi wapo kwa ajili ya kulinda taifa na watu wake, hivyo akawahakikishia wananchi wanaougua kutosita kwenda katika hospitali za jeshi hilo kutibiwa akidai kuwa hawaoni mantiki ya daktari kugoma.
   
 8. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chama changu lazima kinapepo mbaya sana, hakika tumelogwa na tumewapa uongozi mataahila!
   
 9. j

  jigoku JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Liwale na liwe
   
 10. mbalu

  mbalu JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hii laana ni nani aliyetulaani watz?
   
 11. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wana akili ya Ndezi, wanaficha kichwa wakati mwili wote wameuacha nje. Ndio serikali ya Dhaifu hiyo. Tatizo la Dhaifu, wenzie wameshamjulia, huwa wanamwambia tu anachokipenda kusikia na si lazima kiwe cha kweli.
   
 12. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  wakodi vitanda, dawa, vifaa tiba
   
 13. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wana akili ya Ndezi, wanaficha kichwa wakati mwili wote wameuacha nje. Ndio serikali ya Dhaifu hiyo. Tatizo la Dhaifu, wenzie wameshamjulia, huwa wanamwambia tu anachokipenda kusikia na si lazima kiwe cha kweli au chenye manufaa kwa nchi. Anapenda kusifiwa sifa za kijinga.
   
 14. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Hii inaonesha uwezo wa serikali kuwatumikia Watanzania umefikia mwisho! Haiwezekani serikali isiwe na hela za kuwalipa madaktari wake na kuwaboreshea mazingira yao ya kazi na halafu serikali ileile ipate hela za kuwakodisha/ajiri madaktari kutoka nje. Serikali baada ya kuua elimu yetu, imeamua kuua sekta ya afya na taaluma ya udaktari na wakati huohuo inasema wanafunzi wasome masomo ya sayansi. Nashindwa kuelewa mantiki yake.
   
 15. paty

  paty JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,253
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  dah yaani sisi tumerogwa na aliyeturoga amekufa hakuna wa kutegua tego , tuna kwenda tu kama mang'ombe yanayoswagwa na maraisi wa nchi za magharibi ooooooh mbalu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. s

  swrc JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na hapo uelewe figure hiyo ina maslahi ikiwa ni pamoja na 10 per cent. CHAMA CHA MAJAMBAZI, CHAMA CHA MAFISADI, CHAMA CHAMA DHAIFU.
   
 17. m

  majebere JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  hebu nenda pale muhimbili kawaulize wagonjwa haya maswali halafu uone watakufanya nini. Mnakaa kushabikia upuuzi na kuleta maswali ya kizembe tu, kwanza wagonjwa watibiwe huku majadiliano yanaendelea au elitaka wagonjwa wasubiri mpaka hao madaktari watimiziwe shida zao?
   
 18. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  This can happen only in Tanzania
  [h=6]"THINK;
  A country where there is no even a single working CT Scan Machine...Is it true we cannot afford it, and we loose around 6% of Head Injury patients and discharge 99% of the same patients without a proper management.
  Relate this with a Tz Minister driving a 280million V8 Prince (Equalling to approx 1 Phillips CT Scan Machines + Transport)

  Siemens ------------------200000 usd approx
  Toshiba -------------------180000 usd approx
  Beckam coulter------------250000 usd approx
  Sharp------------------------200000 usd approx
  GE----------------------------300000 usd approx
  phillips ----------------------140000 usd approx

  The computer tomography machine (CT-Scan Machine) costs depending upon the technology systems"
  [/h]
   
 19. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  na watu wachache,walioumizwa,wanaoteseka ama waliokufa kwa mikono ya serikal na vyombo vyake,bila kosa,either kwa maslah na matakwa ya wachache,kwa kipigo,kimafia au ajali na magonjwa ya kichawi!damu ya mtu haipotei,ndo malipo apa apa dunian.Hakika wamerukwa akili na busara.
   
 20. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nizaidi ya upofu
   
Loading...