1991-1994 Kijana mpole kutengeneza milipuko (bombs)& Bunduki hatimaye kushindwa kuishi ndoto zake

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,732
7,611
Awali ya yote niwatakie afya njema wana jamvi na Mungu awabariki bila kuwachosha niende kwenye mada.

Mwaka 1991 Baba yangu aliomba uhamisho kufanya kazi karibu na kijijini kwao ili aweze kuwa karibu na Mama yake kumtuza (maana Bibi yangu huyu) alifiwa na Mmewe (Babu yangu) kwa maana hiyo Bibi alibaki ni Mjane na Baba yangu ndiye aliyeachiwa jukum la kumtunza mama yake (bibi yangu).

Tulianza maisha mapya katika mji mdogo uliokuwa karibu na nyumbani kwa bibi takribani kilomita 7 kufika kijijini kwetu na Mara kwa Mara tulikwenda kumsalimia Bibi na tulienda kwa mjomba wangu (Kaka wa mama) ambaye alikuwa mwindaji kwa kutumia bunduki gobole.

Kipindi hicho ktk inchi jirani kulikuwa na vita wakimbizi walimiminika wengi kila sehemu na katika Shule tuliyokuwa tunasoma kulilipuka ugonjwa wa Kipindupindu na homa ya uti wa mgongo, homa ya manjano, ikabidi shule ifungwe na shirika UNHCR likaanza kutoa misaada ya madawa na vyakula katika jamii yote wakimbizi na raia.

Mimi nilipelekwa kwa mjomba kijijini ili kuendelea na masomo maana kulikuwa na shule ambayo wao waliendelea na masomo hakukuwa na mlipuko na tayali watu walipata chanjo na kuanza kutunza mazingira kuhofia kupata milipuko ya magonjwa.

NAANZA MAISHA KWA MJOMBA

Baba aliniacha kwa mjomba na kunipa noti 4 za shilingi 50 ambayo ilikuwa ni shilingi 200.

Siku iliyofuata jioni saa 10:30 nilitoka shuleni nikafika nyumbani na kupata kampani ya watoto wa kucheza nao ambao wote walikuwa na manati za kuwindia ndege walinisihi niongozane nao hadi mashambani kwenda kuwinda tulikwenda na mda wa kurejea majumbani ulifika tukaanza kurejea tukiwa njiani niliona mashimo nikauliza humu kuna nini?

Walinijibu kuwa kuna wanyama wanaitwa Nungunungu wanajichimbia ndani kuwafikia ni ngum maana ardhi ni ngumu sana.

Tulirudi nyumbani na kesho yake ilikuwa ni siku ya ijumamosi hakuna shule nilifikiri kuhusu hao wanyama na walisema kuwa nyama yao ni watamu sana.

Baadae nilifikiri kuhusu michezo ya kitoto kulipua vibaruti vidogo niliyokuwa nimezoea kutumia baruti ya njiti za kiberiti nikawa nawazo vipi nikitengeneza baruti kubwa na unga uliopo ktk njiti za kiberiti.

NAUNDA BOMU

Mchana ulifika tukala chakula nikachukua sufiria mbovu nikaanza kuikata na kuigonga kutengeneza bokis na niliyumia 150 kununua viberiti na kiberiti enzi hizo ilikuwa ni shilingi 5 nikanunua viberiti 30 nakuchuna unga wote nikauweka ktk bokis ikaonekana unga ni kidogo na nikachukua misumari nikachanganya na unga nikaiba petrol kwa mjomba ilikuwa ktk generator nikaweka ktk lile bokisi la chuma cha sufuria nikagonga kabisa na kufunga isipite hewa popote.
Nikachukua ile shilingi 50 iliyobaki nikanunua mafuta ya taa nikachukua kitambaa cha cotton kidogo na kukiloweka ktk mafuta ya taa na kutoboa bokisi ile yenye baruti, misumari na petrol nikaingiza kitambaa ktk ndani ya bokis tukaenda mpaka kwenye shimo tuka dumbukiza bokis kama mita 1.6 tukawasha moto kitambaa tukakimbilia mlimani kusubiri majibu.
Ikapita zaidi ya dakika 10 ilikuwa moshi ukionekana kwa mbali tukadhani zoezi lime kwama mpaka tukadhani twende tuchimbe tutafte bokis letu huwenda moto umezima nikaamuru watoto wenzangu wote twende sehemu ya tukio
AISEEEEEEEEEE KABLA HATA HATUJAPIGA HATUA ULITOKEA MLIPUKO MPAKA WATOTO KUZILAI KABISA SEHEMU YOTE IKAWA VUMBI KUBWA ZAIDI YA 25m² ZA ENEO KULIKUWA SHIMO MPAKA LEO PAMEITWA JINA LANGU LA UKOO
WATU WALIOKUWA VIJIJINI WAKAJA, Wanajeshi waliokuwa wanalinda Usalama katika kambi ya Wakimbizi nao walifika na Defender wakiwa wa tatu Ila Mjomba hakuwa mbali aliwahi kufika pale na kukuta mizoga karibu ya 30 ya Nungunungu akahamishia polini kuficha kwa maana alijua kwa milipuko ule serikali itafika mda mchache ujao.

Wanajeshi waliuliza ni kitu gani kimejiri waliambiwa na mjomba kuwa hata yeye hajui tuliingiwa na hofu Polis na Wanajeshi walienda pale Mara kwa Mara ila hawakung'amua kitu mwishowe Polis walimkamata mjomba kwaajiri ya ushahidi ila hakukuwa na chochote walichong'amua Akatoa Hongo (rushwa ) akatoka.

Niliboresha zaidi miaka ya 94 nikatengeneza vibunduki 2 vidogo vya risasi tano kwa kutumia bomba za miguu ya vitanda na spring za vitanda na risasi ikiwekwa nondo iliyochongwa.
Kipindi hicho mtu anaye taka kuua kichuguu ananipa 1000 natengeneza bomu tuna hamisha kabisa nikawa maarufu nikiwa mtoto wa miaka 12 ila polisi wakaanza kutafta mtu aliyetengeneza silaha zinazosadikiwa kuwepo kijijini hapo mjomba akaanza kutafutwa jinsi atakavyokamatwa

Na mwaka 1994 November, 05 mjomba akaumizwa kimapenzi na akaamua kujiondoa Duniani kwa kujipiga Risasi akajifumua ubongo na gobole ndio ikawa mwisho wangu.

Polis wakafika nyumbani kwa mjomba na kufanya upekuzi na kukamatwa kwa bunduki 3 za mjomba ila 2 nilizounda Mimi kwa ustadi mkubwa na likakamatwa Bomu la kuvunjia vichuguu moja

BABA YANGU ALIKUWA HAJUI CHOCHOTE NDIPO NDUGU YAKE MMOJA ALIKUWA AKIFAHAMU KWA UFASAHA AKAMUELEZA JINSI NILIVYOWEZA KUFANYA MAMBO MAKUBWA


BABA AKATISHA NDOTO YANGU

Chakushangaza Baba akanikasirikia na kunihamisha kwenda mbali kwa Shangazi yangu aliyekuwa mjini ili nikamalize elimu ya msingi huko ktk shule iliyokuwa ikimilikiwa na Kanisa Catholic

Baba alinisisitiza niachane kabisa na mawazo ya kutengeneza silaha kwani nitafia jera niliacha ikawa siri yangu Leo baada ya miaka 26 naweka wazi.

NDOTO ZANGU ZA KUWA MHANDISI WA SILAHA NA KUMILIKI KIWANDA CHA KUTENGENEZA SILAHA ZILIYEYUKA

Maoni; Serikali iendeleze vipaji bila kujali ni kitu gani hatuwezi kuendelea bila kuunda vya kwetu tukawauzia wengine na kuliingizia pato Taifa pamoja na nguvu ya kijeshi.
Katika Dunia ya sasa huwezi kuwa na nguvu ya kibiashara bila kuwa na mfumo imara wa kiulinzi.
 
Nchii vipaji Vingi vinapotea kuna dogo tulikua tunacheza nae cha ndimu anacheza na sisi tumemzidi umbo na kimo. lakini alikua hakabiki bila lafu mbaya na onyo la vipepsi. huyu dogo alikua anatoka familia duni sana hata njumu ilikua mtihani kaishia kuwa mkatamkaa nikimuona nasikitika sana siku hizi mtu mzima. hali bado mbaya nikimuona nakumbuka mbali sana.
 
Nchii vipaji Vingi vinapotea kuna dogo tulikua tunacheza nae cha ndimu anacheza na sisi tumemzidi umbo na kimo. lakini alikua hakabiki bila lafu mbaya na onyo la vipepsi. huyu dogo alikua anatoka familia duni sana hata njumu ilikua mtihani kaishia kuwa mkatamkaa nikimuona nasikitika sana siku hizi mtu mzima. hali bado mbaya nikimuona nakumbuka mbali sana.
Umenikumbusha mbali sana wakati nikiwa dogoo nilipohamishwa toka msimbazi mseto primary kwenda Moshi kuna binti alikua ana mbio kwenye Yale mashindano ya umiseta anatoboa kitaifa nikamkuta Mwaka Jana yupo A-town anafanya umachinga barabarani Na kusumbuana Na migambo yaani inauma mnooooo
 
Umenikumbusha mbali sana wakati nikiwa dogoo nilipohamishwa toka msimbazi mseto primary kwenda Moshi kuna binti alikua ana mbio kwenye Yale mashindano ya umiseta anatoboa kitaifa nikamkuta Mwaka Jana yupo A-town anafanya umachinga barabarani Na kusumbuana Na migambo yaani inauma mnooooo
Angekuwa na ndg walio na kinafasi juu sasa hivi angekuwa anakula bata majuu.
Inchi hii hatuwezi kuendelea bila kuwa na wavumbuzi wetu wenyewe ktk mambo ya ki sayansi.
 
Daaah! Kwenye upande wa nungunungu me naona hili ni tango poli nungunungu hachimbi shimo bana anaechimba shimo ni fuko
 
Daaah! Kwenye upande wa nungunungu me naona hili ni tango poli nungunungu hachimbi shimo bana anaechimba shimo ni fuko
Huyo ndiyo zake mdau!!
Anafiksi sanaaa!
Pitia thread zake! Janja mingi!
Also huko anaposema nimekaa lakin hata hilo shimo halipo achilia mbal kusema wanakula nungu nungu!!..
 
Daa bomu la buku kuangamiza kichuguu zama hiz ndg ungepata wateja weng sn kwa ajili ya kuangamizana ss wenyew
 
Daaah! Kwenye upande wa nungunungu me naona hili ni tango poli nungunungu hachimbi shimo bana anaechimba shimo ni fuko
Mkuu nungunungu wanaishi ktk mashimo labda kama wana utofauti.
 
Huyo ndiyo zake mdau!!
Anafiksi sanaaa!
Pitia thread zake! Janja mingi!
Also huko anaposema nimekaa lakin hata hilo shimo halipo achilia mbal kusema wanakula nungu nungu!!..
Wapi niliposema mji au wilaya?
 
Back
Top Bottom