17 wazirai kufuatia kuteguliwa kwa mabomu- Mbagala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

17 wazirai kufuatia kuteguliwa kwa mabomu- Mbagala

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Jun 9, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  WATU 17 wamezirai na wengine kuwa katika hali ya mstuko mkali katika zoezi la kuteguliwa kwa mabomu yaliyobaki katika kambi ya Jeshi WATU 17 wamezirai na wengine kuwa katika hali ya mshtuko mkali kufuatia zoezi la kuteguliwa kwa mabomu yaliyobaki katika kambi ya Jeshi mbagala.

  Watu hao walipatwa na mshtuko mkubwa hali iliyowafanya wakimbizwe hospitali kwa matibabu ya haraka kufuatia kulipuliwa kwa mabomu mara kwa mara huko Mbagala.

  Watu hao ambao ni wakazi karibu na eneo la kambi hiyo walizimia na wengine kuwa katika hali mbaya na wa;ipelekwa hospitali ya Temeke kwa matibabu zaidi.

  Kufuatia zoezi lililodumu takribani lisaa limoja katika kambi hiyo, baadhi ya wakazi wa maeneo hayo walikimbia nyumba zao kutokana na hofu ya kupoteza maisha yao.

  Wakazi wa maeneo hayo walionekana wakiwa katika makundi makundi wakijadiliana jinsi ya kukabiliana na hali yoyote itakayotokea iwapo zoezi hilo la kutegua mabomu litaenda vibaya.

  Wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakiilalamikia serikali kwa utaratibu wake kwa kutotoa msimamo na tamko rasmi kuhusiana na ulipuaji wa mabomu hali inayowafanya wachanganyikiwe kwa kutoelewa hatma yao ya kuishi maeneo hayo.

  Awali Jeshi la Ulinzi nchini lilitangaza kuteguliwa kwa mabomu hayo hakutakuwa na athari yoyote na matokeo yakawa kinyume kwani mtu mmoja alijeruhiwa na mmoja kupoteza maisha kutokana na kuteguliwa kwa mabomu hayo.

  Kushtushwa kwa wakazi hao kumekuja baada ya jana Wizara ya Ulinzi kutegua na kuyalipua mabomu yaliyobaki katika kambi hiyo zoezi ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa.

  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke Bi. Asha Mahita amesema kuwa amepokea wagonjwa hao 17 na kusema wengi wao ni walipatwa na mshtuko mkubwa hali iliyowafanya wazirai na kupoteza fahamu.

  Bi. Mahita alisema kuwa wagonjwa hao wanaendelea vizuri na wanaweza kuruhusiwa kuondoka muda wowote.
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Pole yao
   
 3. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nawapa Pole sana.

  Hivi haya mabomu watamaliza lini kuyategua? Maana imekuwa routine sasa!
   
Loading...